KOFFI OLOMIDE LAWAMANI KWA KUTOHUDHURIA HARUSI YA PAPA WEMBA

WEMBAPAPA3

 

Shumbu Wembadio Papa Wemba akiwa na Mkewe Marie-Rose Amazon

Lutumba Simaro, Nyoka Longo Jossart, Felix Wazekwa, Werrason, JB Mpiana na Wengineo ni miongoni mwa wanamuziki maarufu waliowaongoza watu wengine maarufu katika harusi iliyofana ya mwanamuziki Papa Wemba na Marie-Rose Amazon, minong’ono na lawama zimetanda jiji la Kinshasa kwa wapenda burudani baada ya Mwanamuziki nguli na mkongwe mwezie Koffi Olomide kutoonekana ukumbini wala kanisani bila sababu ya msingi.

Shumbu Wembadio Papa wemba alifunga ndoa na Bibie Merry Rose Amazon katika ndoa ambayo imekuwa gumzo katioka jiji zima la Kinshasa. Akijitetea kuhusu uamuzi wa kutoshiriki kwenye harusi hiyo Koffi amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hakualikwa na hakupatiwa kadi ya mualiko wa shughuli hiyo. Kwa mujibu wa waandaaji wa shughuli hiyo wanasema mualiko ulitolewa kwa wanamuziki wote na wengine wakisikika wakisema kuwa kwa ukaribu wa Koffi ambaye ameshawahi kufanya kazi na Papa Wemba hakupaswa kungoja mualiko ili aonekane kwenye shughuli hiyo.

Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa na Mtakatifu Joseph huko Matonge na baadaye kufuatiwa na tafrija katika hoteli ya Fleuve Congo Hôtel inasemwa ilikuwa ni mahala ambapo wanamuziki wengi maarufu walikutania kama Lutumba Simaro, Nyoka Longo Jossart, Felix Wazekwa, Werrason, JB Mpiana na wengine wengi, sio rahisi kuwapata magwiji hawa kwenye mkusanyiko wa kawaida labda kwenye misiba ambapo pia huwa kila mmoja anafika kwa muda wake.

Regards

 

Pius Pius Mikongoti

Advertisements

3 Responses to KOFFI OLOMIDE LAWAMANI KWA KUTOHUDHURIA HARUSI YA PAPA WEMBA

 1. Nzowa says:

  Tangu niingie hapa nimekuwa mgonjwa wa hii blog. hongera Mopao Pius na Lubonji hakuna kama Spoti na Starehe.

 2. lubonji says:

  Karibu sana Nzowa!!!
  Tupo Pamoja

 3. wilson malias says:

  Alichofanya koffi sio fair

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: