NI KWELI KOFFI OLOMIDE KAKOPA KWA JB MPIANA DOLA 30.000 $ ?

 

NI KITUGANI KINACHOENDELEA KATI YA JB MPIANA NA KOFFI OLOMIDE ? BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UPATE MAELEZO ZAIDI!!!

Tofauti zinazo jitokeza hivi karibuni kati ya Wasanii hao wawili yatujia vigumu kabisa kujua kiini chake.

Kwanza ifahamike kwamba ma SUPERS STARS haoWote wawili ni Majirani, wanaishi JIJINI KINSHASA kwenye Mitaa ya kifahari mahala panapo julikana kwa jina la ” Montfleury “.

Yasemekana Mzozo wa siku hizi Umeibuka kutokana na kitendo cha JB MPIANA kushindwa kumpa Mualiko Jirani yake KOFFI OLOMIDE, wakati alipo andaa SHEREHE kabambe yakumhenzi Bintie DAIDA kwa ajili ya B’Day yake yakutimiza miaka 18, Tarehe 14-07-2014, Wakati wapo Wasanii na Watu wengine Maarufu waliopata fursa ya kuudhuria napia kuwa mashahidi kwa Tukio hilo ambalo liliacha Gumzo JIJINI KINSHASA. Pamoja nakuwepo na waalikwa wengi,  Watu walipatwa na mshangao pale walivyo muona Kama Mgeni Rasmi ( WERRASON ),walikuwepo pia ( ADOLPH DOMINGUEZ, FALLY IPUPA )…

Siku Chache Baadae, KOFFI OLOMIDE  kwa Upande wake,kaandaa pia SHEREHE kwa Ajili ya B’Day ya Binti yake DIDI-STONE ambae katimiza umri wa Miaka 15.

JB MPIANA huku akiendelea na Shughuli zake, kakaa kimya bila kujali yale yanayopita kwa Jirani, Mtu wakwanza ambae Tumemsikia kwenye Vyombo vya Habari,ni KOFFI OLOMIDE,kamtupia mwenzie kwa kusema : ” KWAKWELI MIMI KUNAWAKATI MWENGINE YANIJIA VIGUMU  KUWAELEWA  KABISA WATU WENGINE, MTU KASHINDWA KABISA KAZI YA MUZIKI,ANACHOKIJUA KWA SASA NI MAJUNGU PEKEE, WALA SI MIMI NILIE MCHUKULIA MKEWE!!! CHUKI YA NINI JAMANI !!!  MIMI SIPO HUKO KABISA “.

Hapa yatubidi tukumbushia kidogo, Wakati bado wanaelewana , KOFFI OLOMIDE, Tumemsikia akimtolea sifa Nyingi sana JB MPIANA siku ya B’Day yake Tarehe 02-06-2014, Namnukuu : ” TUNAPO CHUNGUZA VIZURI KWENYE KAZI YA MUZIKI INCHINI CONGO, MA STARS KATIKA FANI YA MUZIKI WAPO WAWILI, NAO SIWENGINE BALI NI MIMI NA JB MPIANA “.

SASA NANI KAJAKUWASHA MOTO ?

Mtu ambae kajiingiza kwenye Mzozo huo ni Chizi wa Mfalme WERRASON anaejulikana kwa jina la SANKARA DE KUNTA. Yeye kamkingia Ubavu JB MPIANA,kwa kumtolea khashfa KOFFI OLOMIDE pale alivyo tamka kwamba, HUYO MZEE NIMPUUZI TUU, WALA HANA LOLOTE, MWACHENI HUYO KAISHA KABISA, KWANZA MADENI YAMEMZIDI ,HADI KAENDA KUKOPESHA KWA JB MPIANA, KIUMBE ALIE MWEMA WA WATU KAMGEA DOLA 30.000.

Maneno hayo, yamemkera vibaya sana KOFFI OLOMIDE, Kwenye video nilio iambatanisha na Post hii, MOPAO MOKONZI katoa maneno ya khebei kwakusema : ” SINA LAKUSEMA,MIMI NAWASIKILIZENI TUU, NA KAMA UNALO LAKUONGEA, BASI NENA YALE YALIO NA UKWELI,SI LAZIMA KWAKO WEWE KUJIFICHA  MGONGONI  MWA MTU MWENGINE. NAKUOMBA NENDA KWENYE TV,NA UONYESHE KWA MAANDISHI YANAYO THIBITISHA MATAMSHI YA HUYO MSEMAJI WENU, AMBAE KADAI  KWAMBA NIMECHUKUA KUTOKA MIKONONI  MWAKO PESA. KWELI KAMA WEWE NI MWANAUME WA UHAKIKA, BASI FANYA HIVYO ILI UKWELI UDHIHIRIKE !!!

 

LUBONJI WA LUBONJI

Advertisements

4 Responses to NI KWELI KOFFI OLOMIDE KAKOPA KWA JB MPIANA DOLA 30.000 $ ?

 1. Hadj Le Jbnique says:

  kazi imeanza,lakini kwanini kila siku ni wewe koffi,yani unagombana na kila mtu,mwanzo uligombana na Jb na ukachangia kwa kiasi kikubwa kutia petroli kwenye kutoelewana kwa werra de la forret na papa cherii Jb mpiana,badae ukagombanana werra,ukaanza kujipendekeza kwa jb na kufikia mpaka kudai unatamani kufanya nae kazi kwa kuwa ana kipaji kikubwa kama wewe,leo tena unadai hajui muziki,sankara de kunta kakupatia kwelikweli,sasa pambana na huyo kichaa wa werra

 2. Hadj Le Jbnique says:

  zawadi aliyoitoa jb mpiana kwa Daida ni kitu cha Range halafu kitu kizuri ni kwamba Daida anaongea English safi,utamuona hapo akiimba wimbo mzuri sana kwa kiingereza,Good job Jb mpiana,pia Daida kawataja papaa Werra,Papaa Adolphe Dominguez na papaa Fally ipupa akiwashukuru kwa kushow love kwenye sherehe yake

 3. Hadj Le Jbnique says:

  koffi eti nae akamjibu jb hapa..

 4. Hadj Le Jbnique says:

  kiufupi party ya daida ilikua babkubwa ndio mana koffi roho ilimuuma kutoalikwa…pata picha uone hapa watu waliohudhuria,utamuaona werra,adolphe,fally na waheshimiwa mbalimbali pamoja na daida na marafiki zake wakifurahi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: