HATIMAE FERRE GOLA KAJIELEZA ” SINA UPINZANI NA WERRASON “

August 20, 2014

 

KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI ” WILLY “, FERRE GOLA KAONGELEA MAMBO MENGI KUHUSIANA NA GROUP LAKE,KUJIONDOA KWA BAADHI YA WANAMUZIKI, NA MZOZO ULIOPO KATI YAKE NA WERRASON. ( KWA MAELEZO ZAIDI BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI ).

FERRE GOLA : KWANZA SALAMU ZANGU ZIWAFIKIE MASHABIKI WANGU, NAPIA WAPENZI WOTE WA MUZIKI AMBAO WANATUFWATA KWA WAKATI HUU. UMUHIMU WA MTU KUFANYA MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI UPO WAKATI PALE LIPO NENO AU JAMBO JIPYA LA KUONGELEA.

WALA MSIWACHUKULIE WATU WANAO FWATILIA MAMBO TUYAFANYAYO SISI KAMA WAJINGA, SIONI HAJA YAKUJA KWENYE TV WAKATI SINA JIPYA LAKUZUNGUMZIA. TAKRIBAN MIEZI SITA AU SABA SIJAONEKANA KWENYE TV.

MTANGAZAJI : Bado twasubiria kutolewa kwa Single ya Mdhamini wako, Mda mrefu umepita sasa,Ipo Tarehe kamili ambayo Single hiyo itatolewa Rasmi?

FERRE GOLA : Tumesha maliza kazi kubwa ya Single ” PRIMUS PETITE YA QUARTIER “, Tatizo lilijitokeza lipo kwa upande wa Mdhamini wetu, kaomba Wimbo uwe mfupi wa Dakika 6 Kwa ajili ya matangazo ya Kibiashara,wakati sisi tulikua tayari tumesha tengeneza Wimbo wa Dakika 9. kwa maana hiyo,tumelazimika kurudi tena Studio ili tuyafanye marekebisho kama yaliyo hitajika.Kwa wakati huu tupo katika maandalizi ya Video Clip.

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Siku zahivi karibuni, Tumegundua kwamba wapo Vijana wengi walio jiondoa kwenye Group lako,Tatizo ninini hasa? Kosa latokana na wewe, au lipo kwa wale Vijana  ambao Wewe ndie umewalea katika Muziki,na kwasasa hawaridhishwi na utendaji wako wa kazi !!!

FERRE GOLA : Kama nilivyo kuambia hapo awali, Takriban Miezi saba sijapita kwenye Runinga,hakuna Mtu kanisikia napiga kelele kutokana na hili wala lile,yamaanisha Mambo yangu si mabaya. Ntakupa Mfano wa Album ” BOITE NOIRE “, Unapo chunguza Hit Parade Mbalimbali,utagundua Imeshikilia nafasi nzuri, Ipo kabisa kileleni, Kama si nafasi ya kwanza basi ni yapili nakadhalika… Sioni kitugani kitakacho nifanya nilalamike.

MTANGAZAJI : Kitendo cha Vijana hao kujitengua kwenye Orchestra yako,hakikupi shida? mbona wamesha ondoka wengi?

FERRE GOLA : Kumbuka mwanzoni nilivyotoa Album yangu ya kwanza ” SENS INTERDIT “,nafikiri nilikua Mwenyewe,peke yangu . Kwa wale Vijana walio jiondoa, ntakalo lisema ni kwamba,” NAWATAKIA KILA LA KHERI HUKO WAENDAKO “.

MTANGAZAJI : Hayo huyanenayo niyamoyoni kweli?

FERRE GOLA : Ndio, nayatoa moyoni mwangu kwa uhakika, Mimi bado mchanga, ndo kwanza naanza,Mwaka 2006,huoni kabisa niponipo!!! Jamani !!! Walio jiondoa,nawatakia maendeleo mema huko waliko. Wapo baadhi yao ambao bado tunaendelea na mawasiliano,wananipigia simu kunijulia hali!!!

MTANGAZAJI : Kwamfano Mtu kama CHIKITO hua anakupigia simu?

FERRE GOLA : Ndio, CHIKITO mara nyingi tunawasiliana naye

MTANGAZAJI : Yaani kumbe hajadanganya, kaniambia hua anakupigia simu na mnaongea mara kwa mara!!!

FERRE GOLA : CHIKITO ni Mwanamuziki pekee aliejiondoa na ambae hadi leo bado mawasiliano haijakatika.Hua ananipigia simu na kunifaarifu jinsi gani maendeleo yake yalivyo kwa sasa. Hata wakati yuko Inchini Angola,tuliendelea kuwasiliana.

MTANGAZAJI : Inamaana CHIKITO kesha jiondoa kabisa kwenye Group lako!!!

FERRE GOLA : Kanipigia Simu siku mbili zilizo pita, Anahitaji nimkabidhi Hati yake ya kusafiria,Nikamwambia nakumuelewesha kwamba, wakati ulivyo jiunga na Group, hujaja na Pasipoti,na Unavyo amua kujiondoa ni haki yako, basi Nenda kamavile hujawa na PASIPOTI. Tuliongea kiustarabu kila Mtu kamuelewa mwenzie.

MTANGAZAJI : Si unaweza ukamgea hiyo PASIPOTI kama zawadi,yule ni Mwanao, kwanza alikua akikuita  BABA ” PAPA HERVE ” .

FERRE GOLA : Wala sioni haja yakuongelea maneno mengine ilimradi tuu nikuridhishe wewe!!! hivi unacho ongelea hapo Ni Mwanamuziki au Wanamuziki !!!

MTANGAZAJI : Ninacho hitaji kufahamu ni kwamba Hujapatwa na huzuni wowote,wakati wamejiondoa Vijana wako? ntawataja CHIKITO, NICODEM, R-KELLY !!!

FERRE GOLA : Sikiliza, kuna itilafu kidogo katika usemi wako, Wapo Wanamuziki waliojiondoa na wapo pia wale ambao niliwaachisha kazi.

MTANGAZAJI : Kweli ? Wapo walio fukuzwa kazi wakajidai kujiondoa? basi yapo mengi tulikua hatuyajui kabisa!!!

FERRE GOLA : Mikokotano si kazi yangu hasa, kwakifupi, nawatakia kila la kheri,iwe wale waliojiondoa,au wale niliowaondoa mimi.Hivi waweza nikumbusha ni Nyimbo gani walizo zitunga hao waliojiondoa?

MTANGAZAJI : Walikua wakichangia kwenye Nyimbo za Orchestra yako

FERRE GOLA : Kwani Orchestra yangu inajina gani?

MTANGAZAJI : JET SET

FERRE GOLA : Wala sikwali, Umeshawahi kunisikia wapi nikasema Jina la Orchestra yangu ni JET SET ?

MTANGAZAJI : Sasa naomba uniambie, Orchestra yako inaitwaje ?

FERRE GOLA : Inaitwa FERRE GOLA!!!

MTANGAZAJI : FERRE GOLA MUSICA

FERRE GOLA : Tayari umeshaongezea neno Musica ( kacheka )!!!

MTANGAZAJI : Yamaanisha Pindi tunapo ongelea Orchestra yako, Tunakuzungumzia kwanza wewe!!!

FERRE GOLA : Kwani Wewe wafikirije ? Kwajumla, sioni tatizo lolote wakati Wanamuziki wanaamua kujiondoa kwenye Group,hali hii wala si leo ndo imeanza kujitokeza,limeshakua jambo la kawaida!!!

MTANGAZAJI : Kujiondoa kwao wala hakukupi Shida yeyote!!!

FERRE GOLA : Shida yanini sasa ? Tizama kwenye Album ” BOITE NOIRE “, Wengi kati ya Wanamuziki walio changia wapo wala sioni tatizo kabisa. Mimi hua nawapenda Vijana wangu wote, hata kwawale walio ondoka,nilikua pia nawafurahia.

MTANGAZAJI : Unayo yasema hapo si kwania mbaya !!!

FERRE GOLA : Baadhi ya Wanamuziki wote waliopitia kwangu,wamejengeka vizuri kabisa,nimewafua vilivyo,ninao uhakika wanao uwezo wakujitetea vilivyo popote pale wanapo hitajika.

MTANGAZAJI : Lipo Swali nataka lijibiwe kwa uwazi, Imewahi kutokea siku ukaitisha mkutano,ukakaa na Vijana wako na mkayaongelea hasa Matatizo yao khususan yale yanayo ambatana na maswala ya Pesa ?

FERRE GOLA : Bila kujisifu, Mimi niko miongoni mwa wale wachache ambao wanajua kuwatunza vilivyo Wanamuziki. Wote niliwahi kuwanunulia Magari aina ” MERCEDES-BENZ ”

MTANGAZAJI : Kumbe yanayo zungumzwa ni kweli!!!

FERRE GOLA : Wala sikwamba najigamba, Hapana,Kwenye miaka miwili au mitatu iliopita,Vijana wangu wote niliwagea zawadi ya Gari.na wale walioondoka wameondoka pia na MAGARI YAO .

MTANGAZAJI : Ni kweli?

FERRE GOLA : Ndio, Wengi wananijua kwa upande huo, Mimi sio Mtu bahiri. Orchestra yangu ipo sawa, tunajijenga vizuri, Siku za hivi karibuni Mtatuona mimi na Group langu nzima kwenye vipindi vyenu. Kwa sasa tupo kwenye matayarisho ya Album Mpya,Jina litatolewa baadae.

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Upo uvumi uliozagaa kana kwamba Umewaruhusu Vijana wako waweke Nyimbo zao kwenye Album ambayo kwa sasa bado ipo Jikoni.

FERRE GOLA : Mbona swali lako mwenyewe sinalo jibu? hayo wayatoa wapi ?

MTANGAZAJI : Siri yavujishwa na wahusika wenyewe !!!

FERRE GOLA : Yapo mambo mengine hayastahili kutolewa ovyo Inje ya Group, ipo Mikakati ya kisiri ya Orchestra ambayo hutolewa kwa wandishi wa Habari kwa Mda unaohitajika.

MTANGAZAJI : Watu wanakuchulia wewe kama mpinzani wako Mkuu ni FALLY IPUPA, Ikawaje leo hii ukahamishia upinzani wako kwa BOSS wako wa zamani WERRASON ?

FERRE GOLA : Hayo ndo maswali uliyo yatayarisha kwakuniuliza leo?

MTANGAZAJI : Wala simimi, ni Watu wanao hitaji ufafanuzi zaidi kutokana na hayo tunayo yasikia na kuyaona siku hizi.

FERRE GOLA : KINACHO HITAJIKA KUFAHAMIKA HAPA NI KWAMBA ” MIMI SIMTU KABISA WA MALUMBANO ” NA WALA SINA UPINZANI NA MTU YEYOTE ULE .

MTANGAZAJI : Kweli huna Matatizo na Mtu yeyote ?

FERRE GOLA : Ndio ukweli wangu huo,sina tatizo na Mtu.

MTANGAZAJI : Wewe ni Mtu mwenye Kinyongo ?

FERRE GOLA : Hapana!!!

MTANGAZAJI : Unao uhakika kwa hayo majibu yako? huoni kama Watu manyumbani kwao watashindwa kukuelewa?

FERRE GOLA : Sina Kinyongo na Mtu, labda yawezekana,Mimi ni Mwanadamu wa kawaida kama wengine, yaweza ikatokea Mtu kaamka vibaya akawa mwenye kununa, ila jioni kicheko kikamrudilia!!! na ndivyo maisha yalivyo.

MTANGAZAJI : Habari kuhusu Album ” 13ème APOTRE ” ya MOPAO MOKONZI KOFFI OLOMIDE, makubaliano yalikuaje?

FERRE GOLA : Kuna siku nilikua matembezini, Barabarani nikamuona Mzee KOFFI OLOMIDE, kwa heshima nikamfwata na kwenda kumtolea Salaam, kafurahi kuniona ndipo kapendekeza nijumuike naye kwa kuchangia kwenye Album yake. na nikampa ahadi kwamba ntakapokua na Mda ntapitia kwenye Studio ili nipate kuchangia kwenye Album hiyo. NILICHO KIFANYA NIKUTIMIZA KAULI YANGU.

MTANGAZAJI : Watu wanasema KOFFI OLOMIDE yuko nyuma yako,kakusapoti kwa hayo uyatendayo, Kuna Timu imeundwa Mkiwa WEWE FERRE GOLA, FABREGAS, na KOFFI OLOMIDE, huku pande nyingine lipo Group la akina WERRASON,JB MPIANA na FALLY IPUPA !!! hayo umewahi kuyasikia?

FERRE GOLA : Kwanza natoa Samahani sana kwa Wote wanaonisikiliza kwa wakati huu, Kwakweli mimi siyajui nasipo kabisa kwa hayo yote ulioyazungumzia, Wenda kwasababu hua siku hizi mwenye kusafiri sana Inje ya Inchi, taarifa hizo sina. kilichokua cha ukweli ni kwamba ” NIMECHANGIA KWENYE ALBUM YA KOFFI OLOMIDE “. zaidi ya hayo mimi siyajui .

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Wewe ni kijana mwenye sauti ilio nyororo, Mbona hatujakuona sana ukifanya Featuring na WASANII wakigeni ? au Huna Meneja mzuri anaeweza kukutangaza vilivyo?

FERRE GOLA : Willy Swali hilo huo unalipenda sana!!! Mbona natoka kufanya Featuring na KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO MOKONZI

MTANGAZAJI : Wasanii wakimataifa kutoka Inchi nyingine

FERRE GOLA : Kila Mtu anayo mikakati yake.

 

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

 

 

Advertisements

%d bloggers like this: