HATIMAYE PAPA WEMBA KAFUNGA NDOA NA MAMA “AMAZONE “

WAHENGA WANASEMA ” KAWIA UFIKE ”

BAADA YA MIAKA 44 YA MAISHA YA KAWAIDA KWA PAMOJA NA KWA UAMINIFU, MWANAMUZIKI MKONGWE INCHINI CONGO JULES PRESLEY SHUNGU ( PAPA WEMBA ),JANA TAREHE 09-08-2014 KAFUNGA NDOA YA KIDINI NA MKEWE MARIE-ROSE LUZOLO,MAARUFU KWA JINA LA ” AMAZONE ” KWENYE KANISA KATOLIKI ” SAINT JOSEPH ” JIJINI KINSHASA.

WANANDOA HAO WANATARAJIA KUSHEHEREKEA HARUSI YAO KWA MDA WA SIKU TATU, YAANI JANA TAREHE 09, LEO TAREHE 10.SIKU HIZO MBILI, SHEREHE NI KWA AJILI YA WATU MAALUM ( WANANDUGU NA MARAFIKI ).

TAREHE 12 -08-2014 LITAANDALIWA TAMASHA KUBWA KUHUSIANA NA SHEREHE YA HARUSI  HIYO, NA WATU WOTE WANA KARIBISHWA, KHUSUSAN KWA WALE WAPENZI WA RUMBA NA MZEE FULA NGENGE.

KUTOKANA NA TAARIFA ZILIZO TOLEWA NA  MR  JEAN – FELIX BEJE BESALA,AMBAE NDIE MKURUGENZI WA GROUP VIVA LA MUSICA,WATU WENGI MAARUFU KUTOKEA SEHEMU MBALIMBALI, ( AFRICA,ULAYA NA MAREKANI ) WAPO TAYARI JIJINI KINSHASA KWA NIA YAKUA MASHAHIDI WA TUKIO HILO MUHIMU.

MUALIKO UMETOLEWA PIA KWA BAADHI YA WASANII MBALIMBALI WA AFRICA ILI WAJE KUHUDHURIA NA KUFANYA SHOO KADHAA MBELE YA WANANDOA. VIKIWEMO VIKUNDI ” BANA POTO POTO “, ” MATITI MABE “, ” EXTRA MUSICA ” …

WAKIWA TAYARI WAMESHA ZAA WATOTO SITA,PAPA WEMBA NA AMAZONE WALIFUNGA KWA MARA YA KWANZA NDOA YAO YA ASILI KWENYE MIAKA 1970.

SWALI LAKUTAKA KUJUA KWANINI KAAMUA KUFUNGA NDOA YA KANISANI BAADA YA TAKRIBAN MIAKA 40 KUPITA? JIBU LA PAPA KURU YAKA NI KWAMBA : ( MIMI NI MUUMINI WA KANISA KATOLIKI,NAPENDELEA NITAMBULIWE HIVYO NA DHEHEBU HILO ). TAYARI KWENYE MIAKA KADHAA ILIOPITA TULIPATA FURSA YA KUBARIKIWA NA PAPA WA ROMA BENEDICT XVI.

YAANI TUNAHITIMISHA SAKTAMENTI YA NDOA KAMA ILIVYO PENDEKEZWA NA NENO LA MUNGU.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: