MPYA HIYO YA EXTRA MUSICA ( ROGA ROGA ) WIMBO Fièrement Congolais

August 10, 2014

 

MALIZIA WEEKEND YAKO NA EXTRA MUSICA, WIMBO Fièrement  Congolais

WIMBO MAALUM KWAAJILI YA MDHAMINI WAKE AMBAE NI KAMPUNI YA SIMU ” AZUR ”

LUBONJI WA LUBONJI

Advertisements

HATIMAYE PAPA WEMBA KAFUNGA NDOA NA MAMA “AMAZONE “

August 10, 2014

WAHENGA WANASEMA ” KAWIA UFIKE ”

BAADA YA MIAKA 44 YA MAISHA YA KAWAIDA KWA PAMOJA NA KWA UAMINIFU, MWANAMUZIKI MKONGWE INCHINI CONGO JULES PRESLEY SHUNGU ( PAPA WEMBA ),JANA TAREHE 09-08-2014 KAFUNGA NDOA YA KIDINI NA MKEWE MARIE-ROSE LUZOLO,MAARUFU KWA JINA LA ” AMAZONE ” KWENYE KANISA KATOLIKI ” SAINT JOSEPH ” JIJINI KINSHASA.

WANANDOA HAO WANATARAJIA KUSHEHEREKEA HARUSI YAO KWA MDA WA SIKU TATU, YAANI JANA TAREHE 09, LEO TAREHE 10.SIKU HIZO MBILI, SHEREHE NI KWA AJILI YA WATU MAALUM ( WANANDUGU NA MARAFIKI ).

TAREHE 12 -08-2014 LITAANDALIWA TAMASHA KUBWA KUHUSIANA NA SHEREHE YA HARUSI  HIYO, NA WATU WOTE WANA KARIBISHWA, KHUSUSAN KWA WALE WAPENZI WA RUMBA NA MZEE FULA NGENGE.

KUTOKANA NA TAARIFA ZILIZO TOLEWA NA  MR  JEAN – FELIX BEJE BESALA,AMBAE NDIE MKURUGENZI WA GROUP VIVA LA MUSICA,WATU WENGI MAARUFU KUTOKEA SEHEMU MBALIMBALI, ( AFRICA,ULAYA NA MAREKANI ) WAPO TAYARI JIJINI KINSHASA KWA NIA YAKUA MASHAHIDI WA TUKIO HILO MUHIMU.

MUALIKO UMETOLEWA PIA KWA BAADHI YA WASANII MBALIMBALI WA AFRICA ILI WAJE KUHUDHURIA NA KUFANYA SHOO KADHAA MBELE YA WANANDOA. VIKIWEMO VIKUNDI ” BANA POTO POTO “, ” MATITI MABE “, ” EXTRA MUSICA ” …

WAKIWA TAYARI WAMESHA ZAA WATOTO SITA,PAPA WEMBA NA AMAZONE WALIFUNGA KWA MARA YA KWANZA NDOA YAO YA ASILI KWENYE MIAKA 1970.

SWALI LAKUTAKA KUJUA KWANINI KAAMUA KUFUNGA NDOA YA KANISANI BAADA YA TAKRIBAN MIAKA 40 KUPITA? JIBU LA PAPA KURU YAKA NI KWAMBA : ( MIMI NI MUUMINI WA KANISA KATOLIKI,NAPENDELEA NITAMBULIWE HIVYO NA DHEHEBU HILO ). TAYARI KWENYE MIAKA KADHAA ILIOPITA TULIPATA FURSA YA KUBARIKIWA NA PAPA WA ROMA BENEDICT XVI.

YAANI TUNAHITIMISHA SAKTAMENTI YA NDOA KAMA ILIVYO PENDEKEZWA NA NENO LA MUNGU.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 


KOFFI OLOMIDE KASEMA BOSSI WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO NI YEYE

August 10, 2014

HUU NI UJUMBE WA KOFFI OLOMIDE

 

SALAMU ZANGU ZIWAFIKIE POPOTE MLIPO, NI MIMI KOFFI OLOMIDE QUADRA KORAMAN.

WAPO WATU WALIO NIJIA NA KUNITAARIFU KWAMBA,IPO NJAMA MBAYA INAYOUNDWA KWA AJILI YA KUNIDHURU.

WATU MNAPO KOSA LAKUZUNGUMZA WAKATI MKIALIKWA KWENYE TV, BASI JINA LA KOFFI OLOMIDE HALIONDOKI MIDOMONI MWENU.ETI KOFFI NA HILI,KOFFI NA LILE !!! ( KACHEKA SANA ).

BASI MNACHOTAKIWA KUFAHAMU NI KWAMBA, TAJIRI KIONGOZI WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO NI MIMI.HAYO NINAYO YATAMKA,WALA SI KOSA LANGU,MSINILAUMU KWA HILO,ANAEPASWA KULAUMIWA NI BOB MUNDABI,AMBAE KWA SASA NI MAREHEMU,NDIE ALIE TANGAZA RASMI KUA KOFFI OLOMIDE NDIE LEADER WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO.

ASIE KUBALIANA NA MANENO HAYO, BASI RUKHSA KWAKE AENDE AKAMUULIZE BOB MUNDABI.MIMI SIKO TENA HUKO.

WAPO BAADHI YA WATU AMBAO WANAJIDAI KAMA WAO NI MA LEADER,NA UTAKAPO CHUNGUZA KIUNDANI, UTAGUNDUA KWAMBA HAWAJAWAHI KUTUNGA HATA WIMBO MMOJA,WALA KULETA DANSI MPYA YEYOTE. KAZI YAO KUU NIKUNILETEA KHASHFA ILI WASIKIE NATAJA MAJINA YAO, SIWEZI KUJISHUSHIA HADJI KWAKUWARIDHISHA WAO HATA KIDOGO.

KWA SIKU YA LEO, NIPO KWENYE MAANDALIZI YA ALBUM 13 ème APÔTRE, NA WALA SINA MDA WA MALUMBANO.

MIMI NI KOFFI,FANYENI MTAKAVYO, WALA HAMTONIFIKIA. KWANZA YUPO YULE MMOJA AMBAE KAZI YA MUZIKI IMEMSHINDA KABISA,KESHA IKUMBATIA FANI YA MAVAZI. KAWA MWEUPE KAMANINI, HADI WATU HUFIKIA KUMCHANGANYA WAKIFIKIRIA KAMA YEYE NI CHOTARA,KUMBE SIVYO!!!

KATIKA DHIARA YANGU YA HIVI KARIBUNI INCHINI ANGOLA,WATU WAHUKO WALINIPACHIKA JINA LA ” PATRAO ” IKIMAANISHA ” BOSS “.FURAHA YANGU ITAKUAJE SIKU MOJA ITOKEE MOJA WA WANAMUZIKI WA CONGO ASIFIWE KAMA MIMI.

KWAKWELI MIMI SIELEWI KABISA, MTU KASHINDWA KABISA KAZI YA MUZIKI,KAZI ALIYONAYO KWA SASA NI MAJUNGU.KAMCHUKIA JAMAA KWAKUA KAMCHUKULIA MKE.JAMANI MIMI SIPO HUKO KABISA.

NIACHENI NICHAPE KAZI ZANGU,NIPENDE USINIPENDE,HUO NI UAMUZI WAKO. UMESHINDWA KABISA NA KAZI,UNAKUA KWENYE MITINDO YA MAVAZI.

UONGO HAUNA FAIDA,BALI UKWELI WAZAA MATUNDA MEMA.

WEEKEND NJEMA KWA WOTE.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 


%d bloggers like this: