VIDEO CLIP MPYA YA FERRE GOLA ” VIVE LES MARIES “

 

 • HERVE  BATARINGE, Maarufu kwa Jina la FERRE GOLA, kazaliwa jijini KINSHASA Tarehe 03-03-1976.
  Wazazi wake ni wenyeji wa Mkoa wa BAS CONGO.
  FERRE GOLA kaanza Muziki  kama baadhi ya Vijana wengi Inchini Congo kwenye Band za mtaani,
  WERRASON Ndie kagundua Kipaji chake, na ilikua  kwenye Tamasha Jijini Kinshasa.
  Ndipo kaja kumpendekeza  kwenye Group WENGE MUSICA ASILIA KABLA YA MGAWANYIKO.
  Siku yake ya kwanza Kwenye Group WENGE MUSICA BCBG 4×4, Aina yake ya Uimbaji na Sauti yake ilivyo Nyororo, Ikamfanya ADOLPH DOMINGUEZ AMPACHIKE JINA LA ” CHAIR DE POULE ” Ikimaanisha UIMBAJI ULIO SISIMUA NYOYO HADI MWILI UKAINGIWA NA BARIDI.
  KWENYE GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE katunga nyimbo 3. wimbo wa kwanza ni VITA IMANA unapatikana kwenye Album ” SOLOLA BIEN ” iliyotolewa mwaka 1999, Wimbo wa pili Upo kwenye Album ” À LA QUEUE LEU LEU ” iliyo tolewa mwaka 2002 ambayo ina CD 2. kwenye CD ya kwanza kaweka wimbo CHETANI ( WIMBO ULIOMPA JINA LA SHETANI ) na kwenye CD ya pili kaweka wimbo ” VICTIME D’AMOUR ” .
  Baada ya kujiondoa  NA WENZIE KWENYE GROUP WENGÉ MAISON MÈRE MWAKA 2004 NA KUUNDA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE, wakatoa ALBUM ” MIRACLES “. kwenye ALBUM hiyo ambayo pia ilikua na CD 2. kwenye CD ya kwanza kaweka wimbo ” AMOUR INTÉRÊT ” NA KWENYE CD YA PILI kaweka wimbo ” 100 KILOS “.
  Mwishoni mwa mwaka 2005, kajiunga na KOFFI OLOMIDE (QUARTIER LATIN) Mwaka 2006 ilipo tolewa Album ” DANGER DE MORT “, kaweka wimbo ” INSECTICIDE “.
  Mwaka 2006 Kaanza career Solo, na katoa album yake ya kwanza ” SENS INTERDIT ” ALBUM STUDIO 2007 INANYIMBO 12,
  Mwaka 2009 KATOA ALBUM STUDIO ” QUI EST DERRIÈRE TOI ” INAYO CD 2 NA KILA CD INANYIMBO 9 .
  Mwaka 2013 KATOA ALBUM STUDIO ” BOITE NOIRE ” INAYO PIA CD 2. CD ya kwanza inanyimbo 12, na CD ya pili nyimbo 10.
  FERRA GOLA Katoa Single 2 . yakwanza LUMBUKUKU iliotolewa mwaka 2008, na ” AVANT GOUT ” ILIOTOLEWA MWAKA 2011
  KAFANYA FEATURING NA WASANII KADHAA!!! WAKIWEMO   :
  La vie à zéro Feat Didier Milla (2005)
  Terre sacrée Feat Doudou Copa (2007)
  Déception feat Alpatchino (2008)
  Kayembe Temba Feat Simaro Lutumba (2009)
  Dj laisse-moi la place Feat Djungle (2009)
  Love moi Feat Bill Clinton Kalondji (2010)
  Mademoiselle Feat Bolinga (2011)
  Tshekele Pete Feat Phill Darwin (2011)
  Unhappy ft Zik Berry
  Caresse Feat Singuila (2013)
  J’ai tout donné Feat Dry du groupe Sexion D’Assaut (2013)
  Ko Ko Ko Feat Lino Versace (2014)
  Songa Flesh Feat Black Bazar (2014)
  *** MWAKA HUU YUKO KWENYE MATAYARISHO YA MAXI SINGLE ” BLACK BOX ” MTAKUWEPO NA NYIMBO 5.
  TUZO ALIZO ZIPATA FERRE GOLA KATIKA CAREER YAKE.
  • 2005: Kapewa Tuzo la Group Bora la Africa ya Kati Kwenye KORA AWARDS, Wakati bado akiwa  na Orchestra  LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.
  • 2011 : FERRE GOLA kachukua Tuzo la Gold Disc Kutokana na Mauzo ya ALBUM Qui Est Derrière Toi . ZAIDI YA CD 11000 ILINUNULIWA.
  • 2011 : Kapewa Tuzo 3 Kwenye TROPHY AFRO-CARIBEEAN. ZIKIWEMO TUZO LA MWANAMUZIKI BORA, WIMBO ” ZAZOU ” UKATEULIWA WIMBO BORA. NA UKAPEWA TUZO LA BEST CLIP
  • 2011 : Kapewa Tuzo LA MWANAMUZIKI WA KIUME MWENYE SAUTI BORA AFRICA YA KATI.Kwenye  Ndule Awards
  • 2013 : L’album BOITE NOIRE Ikachukua nafasi ya kwanza Kwenye   iTunes  ‘World Music’
  • 2013 : Kapewa Tuzo 2 kwenye Ndule Awards ( MWANAMUZIKI BORA na TUZO la WIMBO BORA ” KITI YA LIBAYA “
  • 2014 : Kapewa Gol Disc kutokana na Mauzo ya ALBUM Boite Noire , ZAIDI YA CD 80.000 IMENUNULIWA .
  • FERRE GOLA NI MWANAMUZIKI PEKEE AMBAE KAHAMIA KWENYE ORCHESTRA NYINGINE KWA MALIPO. KWA MUJIBU WAKE MWENYEWE, KASEMA HADI UHAMISHO WAKE UWE KAMILI NA YEYE KUJIUNGA  NA GROUP QUARTIER LATIN,PALIKUA NA MAKUBALIANO KATI YAKE NA KOFFI OLOMIDE YALIYO MLAZIMU MKONGWE HUYO ATOE KITITA CHA DOLA ELFU 17 ( 17000 USD )KAMA MALIPO YA UHAMISHO.

  LUBONJI WA LUBONJI

5 Responses to VIDEO CLIP MPYA YA FERRE GOLA ” VIVE LES MARIES “

 1. glady says:

  Kwa muziki wa kizazi cha nne namkubali sana ferre gola, kuna baadhi nyimbo sichoki kuzikiliza, vita imana, 100kg lekeleke na nyingine nyingi, ferre anasauti ya ajabu.

 2. lubonji says:

  Tupo Pamoja !!! Glady

 3. kennedy kituka simon says:

  ukweli huu ni mwanamziki ambae tuna mkubali sana katika wasani wakikongo kwa sasa hua napenda sana rumba zake.

 4. At this time it appears like Drupal is the best blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

 5. Currently it seems like Drupal is the preferred blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: