TUONGELEE WENGE MUSICA BCBG 4×4 KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA ( SEHEMU YA SITA )

TUNAENDELEA NA SIMULIZI YA KUSAMBARATIKA KWA ORCHESTRA WENGE MUSICA  4×4  TOUT TERRAIN NA MPIGA GITA BURKINA FASO MBOKA LIYA.( SEHEMU YA SITA )

KWENYE SEHEMU HII TIZAMA KUANZIA DAKIKA YA 58 ” HADI 01H08.

 

BURKINA FASO : Ukorofi ukaja kujitokeza kutokana na Tamaa, natoa mfano wangu mwenyewe, ( KWENYE WIMBO WANGU WA SERGE PALMI, SERGE PALMI NI KIJANA AMBAE MAKAZI YAKE NI JIJINI BRUSSELS, KWAKUTAKA WIMBO WANGU HUO UPEWE JINA LAKE, KALAZIMIKA KUTOA KITITA CHA HELA TAKRIBAN DOLA ELFU TANO ( 5000 USD ). CHA AJABU KWA PESA HIZO, JB MPIANA KACHUKUA DOLA ELFU MBILI ( 2000 USD ) NA KAJA KUNIGEA MIMI PESA ZILIO SALIA, YAANI DOLA ELFU TATU ( 3000 USD ) HUONI KAMA HIYO NIDHULUMA  ?

MTANGAZAJI : Umejuaje kama Kutokana na Wimbo wako huo wa SERGE PALMI ,JB MPIANA kapewa Dola Elfu Tano Pahali pa Dola Elfu Tatu alizo kugea?

BURKINA FASO : Kwani wewe wafikiri kuna siri ? wala usijidanganye, katika mambo yetu haya, hakunaga na Siri!!!

MTANGAZAJI : Ukaelewaje kitendo hicho alicho kifanya JB MPIANA kwa kuchukulia kiasi cha hela zako Dola 2000

BURKINA FASO : Kwangu mimi nilichukulia kua Jambo la kawaida tuu,Binafsi sina tabia ya Tamaa,Unapo nilinganisha na wao,utagundua kwamba wao ni Watu wenye Tamaa na hupenda kuishi maisha ya Juu na ya kifahari, wakati uwezo hawana.Kuna methali isemayo : Roho ya Tamaa mwishowe humpeleka Mtu kwenye hali ya kufilisika.

Mimi nayafurahia Maisha yangu ya leo,Pia namshukuru Mungu kunijaalia kwa kunipa kipaji kinacho niwezesha kuhudumia Familia yangu. Kama Wewe hujaridhika na kile ulichonacho na hupendelea vyote vinavyo patikana Duniani viwe vyakwako, basi Rukhsa kwako!!! Unacho takiwa kukumbuka ni kwamba, Walikuwepo hapa Duniani Matajiri wakubwa zaidi yako, Waliondoka na kuviacha vyote hapahapa. Akina MOBUTU ambao walikua na Utajiri wakupindukia, wako wapi leo?

MTANGAZAJI : Kweli kabisa kwa yale uyanenayo, Watu Tunaondoka na kuviacha Vyote Hapa Duniani.Tulikuja bila Kitu na Ndivyo tutakavyo rudi. Sasa lipo Swali, Watu wanataka kujua : MENGI KUTOKANA NA MAFAANIKIO YAKO,KUANZIA WAKATI BADO MPO KWENYE GROUP WENGE BCBG 4×4 TOUT TERRAIN, HADI BAADA YA KUSAMBARATIKA KWA GROUP HILO, NA WEWE KUHAMIA WENGE BCBG, YASEMEKANA ULIKUA UKITUMIA SANA MAMBO YA KIUSHIRIKINA, WASEMAJE HAPO!!!

BURKINA FASO : Ntakacho kisema kwa hapo, ni kwangu Mimi kukubali Ndio, hua natumia Dawa, ILA SASA NILAZIMA UFAHAMU KWAMBA DAWA NIITUMIAYO MIMI SI YA KAFARA, BALI NI UWEZO KUTOKA KWA BABA MUNGU.

Ufundi wangu Kwenye GITA, wala sijaenda Shule, ni kipaji nilichopewa na MUNGU. Ntakacho ongezea hapo ni kwamba nilibahatika kufanya kazi na wapiga Gita WAKONGWE NA  MASHUHURI INCHINI CONGO, HIVYO IKANIPELEKEA NIJIIMARISHE VIZURI KABISA KWENYE KAZI HIYO.

MTANGAZAJI : Kwahiyo unatuambia kama kweli hujawahi kugusa Dawa ?

BURKINA FASO : Wala sijui kitu kinachoitwa Dawa maishani mwangu

MTANGAZAJI : Umewahi alakini kufanya kazi na Watu wanaohusudu Dawa, Wale ambao uliwataja kuwa Wafwasi wa Shetani.

BURKINA FASO : Wala sijawaita wao Mashetani kwakisa eti nimewakuta na Dawa, Hapana kabisa,Ninacho jitahidi kukuelewesha ni kwamba, Unapo wauliza wale Watu ambao ni wacha Mungu ni zipi Dalili za watu wa Shetani ? Watakujibu kua : WAFWASI WASHETANI UTAWAJUA KUTOKANA NA MANENO YAO,MWENENDO WAO,KADHALIKA NA VITENDO VYAO. Hayo yaweza kukusaidia kumjua Mtu upande gani anako elemea. Ama Kushoto au Kulia. KWAKIFUPI SIWEZI NIKAKATAA KATU KAMA MAMBO HAYO YAKISHIRIKINA HAYAPO!!! ILA BINAFSI SIJAWAHI KUMKUTA MTU YEYOTE AKITUMIA KAFARA. BALI NAONA KAMA NYOYO ZAO NA VITENDO VYAO HUENDANA KABISA NA VYA WAFWASI WA SHETANI.

Itakuaje wewe wajua fika kama Mimi kama Mfanyakazi wako, Mpiga GITA SOLO Namba Moja,niko kwenye mahitaji, Pindi ninapo kupigia simu hutaki kupokea,Nikueleweje?

MTANGAZAJI : Ni Mtu gani uliekua ukimpigia Simu na akakataa kupokea?

BURKINA FASO : Ntakupa mfano wa MUKULU ( JB MPIANA ), Yeye hujua hali yangu halisi kipesa ilivyokua Mbaya,Nikampigia Simu ili nipate Msaada kutoka kwake, huku yeye kakataa katu kupokea Simu!!!

MTANGAZAJI : Kwa wakati ule Wewe ni Mmoja wa Wanamuziki wake

BURKINA FASO : Ndio nikitembelea Gari Bovu kabisa JIJINI KINSHASA, Vijana wa JIJI hilo ndio waweza kukuhadithia vilivyo. Gari lenyewe nikalipachika Jina la ” POURQUOI OZONGELI SOUVERAIN OSALELI YUDA ” ikimaanisha ” KWANINI WARUDILIA KUMFANYIA KAZI SOUVERAIN ( JB MPIANA ) WAMTUMIKIA YUDA ESKARIOTE ” ( kacheka sana Kalipiga Gita likiendana na Maneno niliyo yataja hapo juu ) tizama Vidéo anzia kwenye Dakika 1:03:27.

TUMEACHANA VIBAYA SANA MIMI NA JB MPIANA, KANIFUKUZA KAMA MBWA!!!

MTANGAZAJI : Wewe uliamua kwa hiari yako mwenyewe kwenda kwa JB MPIANA baada ya Mgawanyiko wa Group WENGE MUSICA 4×4. JB MPIANA kakusaidia kwa kiasi kikubwa, Pesa unazo, Umaarufu unao, Magari unayo, Umesafiri kwenye Inchi Mbalimbali kutokana na JB MPIANA, Huwezi ukamsaliti. NIKIPI KILICHO TOKEA HADI UKAJIONDOA ?

BURKINA FASO : Sidhani kama nimemtukana na wala sijaongelea Ubaya wowote unao husiana naye.

MTANGAZAJI : Waonekana mwenye Hasira ulivyo ongelea swala la JB MPIANA kukataa kupokea Simu yako

BURKINA FASO : Wala sivyo,kuna kitu kimoja ambacho watakiwa kuelewa, MWANAMUZIKI ANAYO HAKI YA KUJIELEZA POPOTE PALE TENA KWA WAKATI WOWOTE ULE. Chukulia Mfano wa hapa Ulaya,utawaona WANAMUZIKI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI (MANCHESTER, LONDON, LIVERPOOL, wakipanda Jukwaani kwa pamoja wala hilo si tatizo kabisa!!!

MTANGAZAJI : Cha maana ilikua ni kwako wewe kumtaarifu Bosi wako kama wahitaji kwenda kufanya Kibarua sehemu fulani tena kwa kipindi kadhaa, sidhani kama anaweza kukataa!!!

BURKINA FASO : Mambo gani hayo ya kijinga waniletea wewe!!! Rukhsa yanini nimuombe? kwani nilikua na Mkataba naye?KWANI NI YEYE ALIENIFUNZA UTUMIAJI WA GITA ?

MTANGAZAJI : Ulikua mmoja wa Wanamuziki wa Group Lake

BURKINA FASO : Sawa,Sijakataa !!! Niwajibu wa Bosi mwenyewe ili Watu wazidi kumheshimu,ni vyema awe mwenyewe wakwanza Mtu mwenye kutekeleza kanuni na Utaratibu wa Kampuni. Nikama leo hii anavyo dharaulika Rais wa Congo, kwakua kashindwa kwanza kujiheshimu mwenyewe.

Wengi hawamtakie Mema,Maombi yao kwanza ni janga la Njaa litatuliwe, Watoto waende Shule, hivyo, iondolewe picha mbaya sana inayo zagaa kuhusu Vijana wa mtaani wa JIJI LA KINSHASA, maarufu kwa jina la ” SHEGE “. Wala sidhani kama Mwenyezi Mungu kawaleta Duniani Vijana hao kwa madhumuni ya kuteseka, Watu husahau kabisa kwamba Taifa la kesho litajengwa na Vijana hao. Kwa leo hii wanachukuliwa kama Vibaka, Walalahoi, na Watu Wengine wanawachezesha kama Mpira kwa Maslahi yao binafsi. hapa ntawataja JB MPIANA NA WERRASON. ILA IPO SIKU VIJANA HAO WATAAMKA NA UMMA UTAWAELEWA.  NA HUO NDIO UTABIRI WANGU.

MTANGAZAJI : Baada ya Mgawanyiko Wa Group WENGE MUSICA 4×4, kikosi chenu kilikua na WANAMUZIKI BORA ZAIDI,akina PRINCE ALAIN MAKABA, BLAISE BULA… IKAWAJE NAO WAKAJA KUJIONDOA ?

BURKINA FASO : Kweli kabisa, Tulikua na Kikosi kizuri na kamili kabisa, Kwenye GITA walikuwepo PRINCE ALAIN MAKABA,MIMI MWENYEWE MBOKA LIYA, PATIENT KUSANGILA, JIJINI KINSHASA WALIONGEZWA PIA VIJANA KADHAA AMBAO  WALIKUA WAPIGA GITA WAZURI. ILA kuhusiana na hawa vijana, Ntasema kilikua kikosi cha pili, kwakua Mazoezi tulikua tukifanya nao Nyumbani kwake JB MPIANA. Alikuwepo pia TITINA AL CAPONE.

MTANGAZAJI : Kweli Group lenu lilikua na Mchanganyiko wa Vichwa.

BURKINA FASO : Kwa upande wa Waimbaji,walikuwepo JB MPIANA, BLAISE BULA, AIMELIA, ALAIN MPELA.

MA REPPA WALIKUA TUTU GALLUGI NA ROBERTO WUNDA. GROUP LETU LILIKUA NA KIKOSI KIZURI SANA.

TATIZO LIKAJA KUTOKANA NA TAMAA, SISI WENGINE TUKIWA NA MIPANGILIO YA MAENDELEO KATIKA MAISHA, KUMBE MWENZETU YUKO NA NJAMA ZAKE YAKUTAKA KUWATIMUA MASTAFU WOTE WALIO TOKANAYE KWENYE GROUP WENGE BCBG 4×4.ORIGINAL.

MTANGAZAJI : Hapo ninani unaye muongelea ?

BURKINA FASO : Si Mwengine bali ni JB MPIANA, YEYE KESHATUONA KAMA PINGAMIZI KUBWA,HASA KUHUSIANA NA MASWALA YA PESA,NDO USIPIME KUMUULIZA!!! KWA HIYO NI BORA KWAKE YEYE KUWAONDOA WALE WOTE AMBAO WANAO UWEZO WAKUMUULIZA BILA WOGA WOWOTE MASWALA YOTE YANAYO ENDANA NA GROUP, YAKIWEMO YALE YANAYO HUSIANA NA “PESA”. KADHALIKA HATA HUKO KWENGINE KWA JAMAA YAKE NA RAFIKI YAKE MAMBO YAKAWA VILEVILE.

MTANGAZAJI : Rafiki yake Gani huyo?

BURKINA FASO : WERRASON, JB MPIANA NA WERRASON NI MARAFIKI WAKUBWA, NA MAMBO YAO WANAYAFANYA KWA MPANGILIO MMOJA… ITAENDELEA …

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

 

 

 

4 Responses to TUONGELEE WENGE MUSICA BCBG 4×4 KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA ( SEHEMU YA SITA )

 1. glady says:

  Nasubiri iendelee lubonji.

 2. lubonji says:

  Ndio!!! Glady, vizuri utizame sehemu nyingine ya kwanza hadi ya tano kwenye Blog MUZIKI NA LUBONJI, Asante

 3. glady says:

  Sorry lubonji, siipati hiyo blog, pls nisaidie niipate.

 4. lubonji says:

  ingia Facebook Andika ” Muziki na Lubonji ” Utaiona bila shaka Glady

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: