UTATA KUTOKANA NA KIFO CHA MSAIDIZI NA PIA KIJANA WA KARIBU WA WERRASON ” HUGUES KITAMBALA “

Lafoule-Aklam10411355_673128669424300_4366357132382617624_n (1)

 

Alhamisi Tarehe 26 Juni 2014, Kifo kimemkuta HUGUES KITAMBALA, wakiwa mazoezini kwenye Ukumbi wa ZAMBA PLAYA, sehemu ambako WERRASON na Group lake la WENGE MUSICA MAISON MERE,hufanyia mazoezi.

Habari zilizo tufikia kuhusiana na Mkasa huo,zazungumzia kwamba, HUGUES KITAMBALA, kadondoka akiwa jukwaani na kufariki papo hapo.

HUGUES KITAMBALA licha yakua ” KATIBU MKUU WA FOUNDATION WERRASON ” alikua pia kijana wa karibu sana na WERRASON,akijihusisha na maswala binafsi ya STAR huyo wa Muziki.

Takriban miaka 10 sasa yuko kwenye ushirikiano wa karibu na WERRASON. Kwa uhakika, huwezi ukampata WERRASON moja kwa moja bila kupitia kwa HUGUES, kwa mara nyingi ni yeye aliekua akipokea simu ya bosi wake.

Kama kawaida ya AFRICA, kila kifo hakikosi sababu, Baadhi ya ndugu na marafiki wa marehemu wamshutumu WERRASON kana kwamba ndie chanzo cha kifo cha kijana huyo!!!

Swali Kwanini alaumiwe WERRASON ?

Jibu kutokana na swali hilo latolewa na Kaka Mkubwa wa Marehemu kwajina anaitwa WILLY MUBIALA,yeye kasema, 1. anashindwa kuelewa kifo cha mdogo wake huyo,ambae hakuwa mgonjwa na wala hakua na tatizo lolote. kwake yeye chanzo cha kifo cha HUGUES,kitafutiwe kwa WERRASON na WENGE MUSICA MAISON MERE. kwakua Mdogo wake HUGUES kafariki akiwa jukwaani. 2. Ikawaje kabla ya HUGUES KITAMBALA kudondoka na kufariki Dunia, ni REPA ” BERCY MWANA ” aliekua wa kwanza kudondoka akiwa pia jukwaani ila kwa bahati nzuri yeye hajafa ?. 3. Haelewi kwa nini Pindi HUGUES kafariki kakimbizwa moja kwa moja Hospitalini na mwili wake kuhifadhiwa kwenye Chumba cha maiti pasipokua na idhini ya FAMILIA. 4. Kilichokua cha kushangaza zaidi, ni pale Umaiti ulipo mkuta HUGUES  akiwa JIJINI KINSHASA, Ikawaje pahali pakuwapa tarifa Familia kubwa ilioko JIJINI KINSHASA, Mkawaita kwanza watu wanaoishi UFARANSA ?,kwakweli Bado kuna maswali mingi ambayo Majibu kamili  yahitajika .

HUGUES KITAMBALA kaacha Mchumba na Mtoto mmoja.

Pande ya WERRASON wanasemaje kuhusiana na shutuma hizo ?

Msemaji Mkuu wa WERRASON anaejulikana kwa jina la SANKARA DE KUNTA, kasema, kama wanaongelea uchawi, basi mfaamu ya kwamba Tokea GROUP WENGE MUSICA 4×4 ilipo  sambaratika na kuundwa upya Group WENGE MUSICA MAISON MERE mwaka 1997, hapajawahi kutokea maafa yeyote, Na kama kweli ni uchawi, basi WERRASON angewapitisha kwanza Ndugu zake, Kaka yake Mkubwa JONATHAN ambae yuko CANADA, kaka yake FRERE PATRICE,Mdogo wake GUY, watoto wake, EXAUCEE NGIAMA na GLADYS NGIAMA, Mbona hao wote wako hai? acheni kufwatana na mambo ya Internet inazidi kuwapoteza watu.

MAZISHI YA HUGUES KITAMBALA INATARAJIWA KUWEPO KESHO JUMAMOSI. SALAMU ZETU ZA POLE NA RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE FAMILIA NA NDUGU WA MAREHEMU, PIA KWA WERRASON NA WENGE MUSICA MAISON MERE.

LUBONJI WA LUBONJI

3 Responses to UTATA KUTOKANA NA KIFO CHA MSAIDIZI NA PIA KIJANA WA KARIBU WA WERRASON ” HUGUES KITAMBALA “

  1. glady says:

    Sad story, r.i.p hugues kitambala

  2. We absolutely love your blog and find most of your post’s to be what precisely I’m looking for. can you offer guest writers to write content in your case? I wouldn’t mind producing a post or elaborating on a few of the subjects you write with regards to here. Again, awesome web log!

  3. I’ve bookmark your site and also add rss.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: