Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema wa Wenge

Ingawa wimbo huu maarufu toka kwa Wenge ya JB Mpiana unajulikana kama utunzi wake JB Mpiana kiukweli kabisa Wimbo huu ni utunzi wake kijana machachari Zulema ambaye ni bonge la kipaji ambacho kiukweli kwangu naona kinapotea.

Zulema ni muimbaji mzuri ambaye kwa kipidi kirefu amekuwa akisumbuliwa na uteja kwa utumiaji wa madawa ya kulevya. JB Mpiana aliamua kumsaidia Zulema kama mdogo wake na kuna kipindi alipelekwa kwa wataalamu na kupatiwa ushauri nasaha ana alitangazwa kuacha matumizi ya madawa hayo.

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Nakutakieni siku njema, Post hii imerudiwa kwa heshima ya Ndekwa Mwana Bebg nakati ya Dare salaam hesmima mingi kwako Mukulu wa Bakulu, Gilbert wa Mikumi Pamoja sana, Mamaa Gladys, Papaa James Maselle, heshima kwako, Mwambungu nakati ya Tunduma, Steve BCBG pamoja mzazi, Frank Le Jeebeenique, Mukulu Hadji Le Jeebeenique miss u brother.

Advertisements

6 Responses to Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema wa Wenge

 1. glady says:

  Huu wimbo Ni shida, ninaupenda Sana, hasa alipoimba jb na afande Ni hatari, naomba utuwekee wimbo mwingine alioumba hiyo zulema ili tumjue vizuri, naomba utafute video engobo gros ya jb mpiiana pls uiweke hapa.

 2. Ndekwa Mwangata says:

  Wengee ni Zawadi toka kwa Mungu……Shukrani kwako pia Papaa Pious

 3. Hadj Le Jbnique says:

  Papaa Pius tupo pamoja sema niko busy kidogo ndio nakosa muda wa kuandika japo napita sana humu na kushiriki kwa njia ya kusoma tu,anaetaka kumjua zuli zulema vizuri atizame video hii kuanzia 8:20,akifanya unyama…

 4. Hadj Le Jbnique says:

  zulema anaendelea kufanya unyama hapa ..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: