BREAKING NEWS: King Kester Emeneya afariki dunia

Wimbo Zinzi wake King Kester Emeneya

Habari zilizotufikia punde zinasema kuwa mwanamuziki King Kester Emeneya amefariki dunia. Habari zilizopatikana kutoka kwenye chanzo cha habari zinasema kuwa Emeneya amefariki leo huko Ufaransa alipokuwa akiishi na familia yake bila kueleza kwa undani chanzoo cha kifo hicho.

 Jean Emeneya Mubiala Kwamambu alizaliwa November 23, 1956 huko Kikwit Bandundu, amefariki leo February 13 2014 huko Paris, Ufaransa.  

Emeneya alizaliwa huko Kikwit nchini Congo alikulia huko na alijiunga na bendi ya Viva la Musica mwaka 1977 akiwa mwanafunzi wa   political science katika chuo kikuu cha Lubumbashi. Katika miaka ya 80 mwanamuziki Emeneya alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa Africa na mnamo December 24 1982 aliamua kuanzisha bendi yake ya Victoria Eleyson.

Emeneya Djo Kester alikuwa ni mbunifu na ni mwanamuziki wa kwanza toka Africa ya kati  (central African musician) kuchanganganya muziki wake na ala za ki electronic (synthesizers) katika albamu yake iliyotamba ya Nzinzi ambayo iliuza zaidi ya kopi Milioni moja. Baada ya mafanikio hayo Emeneya hakuishia hapo kwani mwaka 1993 alitoa albamu yake iliyoitwa kwa kiingereza “Every Body” ambayo ilisambazwa na kampuni maarufu ya Sonodisc, Albamu hii ilifanya vizuri sana ndani na nje ya nchi ya Congo DRC na mwaka 1997 baada ya kimya cha takribani miaka 7, King Kester aliamua kurejea Congo. Inakadiriwa watu karibu 80,000 walihudhuria onyesho lake la kwanza aliporejea DRC, rekodi ambayo haijavunjwa kulingana na media za Congo.

Ama kwa hakika  Emeneya ni mmoja ya wanamuziki nguli walio na mafanikio ambao Afrika kwa ujumla imewahi kuwa nao. Tangu mwaka 1991 marehemu Emeneya alikuwa akiishi Ufaransa na familia yake, mpaka kifo kinamkuta Emeneya alikuwa na nyimbo zaidi ya 1000 elfu moja na ameshatumbuiza kwenye maonyesho makubwa kwenye mabara yote matano.  Huyu ni mwanamuziki wa tatu CONGO inampoteza kwa mwaka jana na mwaka huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: