HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA. SEHEMU YA TATU

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza jinsi Ferre Gola alivyoingia Wenge Musica akiwa ni mwanamuziki wa mwisho kuwa recruited kabla ya bendi hiyo kuvunjika na pia sehemu ya pili kuangalia maisha yake ndani ya BCBG mpaka alipoamua kutoka kivyake na kuanzisha bendi yake…. Leo ni sehemu ya Tatu kama inavyoletwa kweu na msimulizi wako mahiri Lubonji wa Lubonji.

Mwanamuziki Ferre Gola akiteta jambo na mke wa mfanyabiashara maarufu Macheni hii ilikuwa alipokuja nchini kutoa burudani.

FERRE GOLA na Group Les Marquis de maison Mère, wakafaanikiwa kutoa Album yao MIRACLE, Utazikuta nyimbo Amour ya Intérêt na 100 kilos utunzi wa FERRE GOLA,
Ecole utunzi wa JUS D’ÉTÉ MULOPWE, TRAHISON wa BILL CLINTON KALONDJI.
ALBUM MIRACLE ilipokelewa vizuri sana, mashabiki, wapenzi wa muziki pia wajuzi wa maswala ya muziki wakawaweka kwenye nafasi ya kwanza kabisa kwa wanamuziki wa kizazi kipya huko CONGO (5th generation).
Ingawa mambo yao yawaendea vizuri kutokana na SHOO zao kujaa watu wengi, kushangiliwa kwa nguvu, na pia kupata mashabiki wengi, kadhalika Album yao kupokelewa vilivyo, Baadhi ya wandishi wa Habari wakasema:” VIJANA HAWA WANAVIPAJI VYA HALI YA JUU, WANAWEZA KUSONGA MBELE KABISA, ILA WANATATIZO MMOJA KUBWA SANA, NALO NIKUTOKUWA NA LEADER KATI YAO. NA NDILO LILILO WAPONZA.”

MGAWANYIKO WA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE

Hali yakutoelewana ikazidi kukua,mikokotano huku na huku, kila Mmoja kajidai ndie yu LEADER, wengine wajidai ndio wakali kuzidi wengine ,mizozo ya hapa na pale ikazidi kujitokeza.
Hali hiyo ya Utata ikaleta chuki na dharau, ndipo mgawanyiko ukatokea.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakawa pande mmoja, huku JUS D’ÉTÉ MULOPWE na salio la Group pande zao.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakachukua uamuzi wa kurudi mjini KINSHASA kujifiriria na kupata ushauri ili wajiendeleze kimuziki, Kwa upande wake JUS D’ÉTÉ kaamua kubaki PARIS na kujichukulia kama kiongozi pekee wa Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

MJINI KINSHASA MAELEWANO KATI YA BILL CLINTON NA FERRE GOLA YAKATOWEKA.
Wa kwanza kuchukua ndege na kurudi KINSHASA alika BILL CLINTON, katua kwenye uwanja wa ndege wa NDJILI tarehe 15 February 2005, siku nne baadae yaani tarehe 19 February 2005 FERRE GOLA naye katua MJINI KINSHASA. Huku Mashabiki wakisubiria kuwaona pamoja kwenye Press conference, FERRE GOLA kapata tetesi ya kwamba BILL CLINTON hatokuja kushirikiana naye kwenye Press conference ,na tayari ameshakua na kundi lake na kalipa jina la ” LES MARQUIS SAMOURAÏS”. FERRE GOLA kwa upande wake, kalizimika kuunda kwa haraka kundi lake kalipa jina la “ MARQUIS DES BEAUX – GARÇONS “.

MKONGWE KOFFI OLOMIDE KAINGIA UWANJANI :
KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO kamtaka kwa hali na mali FERRE GOLA ili ajiunge na Group lake la QUARTIER LATIN. Kafanya juu chini kwa kuwarubuni ndugu wa karibu wa FERRE GOLA ili wamshawishi ajiunge naye,na hajafaanikiwa. Basi ikabidi amtafute Jamaa wa karibu sana na FERRE GOLA ambae FERRE GOLA hua kampa heshima zote, Jamaa anaishi barani Ulaya, Jina lake JÉRÔME MONTIGIA, huyu ndie kafaanikisha ujio au uhamisho wa FERRE GOLA kujiunga na Group QUARTIER LATIN ya MOPAO MOKONZI. Ndipo FERRE GOLA kafanyiwa mkataba maalum, na baadhi ya vipengele vya mkataba huo ni kwamba FERRE GOLA atapeya DOLA elfu 15000, na mkataba ni waku renew kila baada ya mwaka mmoja, kwa makubaliano ya pande zote mbili.

KOFFI AMKABIDHI FERRE 15,000 USD

Kitendo cha KOFFI OLOMIDE kumkabidhi FERRE GOLA kitita cha DOLA elfu 15000, kilileta gumzo kubwa hasa kwenye vyombo vya habari, kwa sababu ni jambo ambalo halijawahi kutokea. Ndipo walivyo weka kwenye vichwa vya habari (LE TRANSFERT LE PLUS CHER (THE MOST EXPENSIVE TRANSFER ).

WAPAMBE WA WERRASON WAJA JUU :
Kitendo alicho kifanya KOFFI OLOMIDE kumchukua FERRE GOLA,kiliwaudhi saana wapambe,wapenzi na watu wa karibu wa WERRASON. Kwa madai yao, wanasema ya kwamba, KOFFI OLOMIDE ndie aliye washawishi kina FERRE GOLA, BILL CLINTON, JUS D’ÉTÉ, SERGE MABIALA, JAPONAIS na kadhalika watoroke na waunde Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE. Nia yake halisi ni kumdhuru na kumuathiri WERRASON aumie na aanguke kimuziki, kwa hali hiyo hatokua na mpinzani.

MJINI PARIS, Waliandamana hadi kwenda kwenye nyumba ya KOFFI OLOMIDE huku wakitoa matusi makali dhidi yake. kwa bahati nzuri hapaja tokea madhara yeyote.
Kwa upande wake KOFFI OLOMIDE kajitetea kwa kusema hana jambo lolote na WERRASON ambae kamchukulia kama Ndugu, na wala hajamchukua FERRE GOLA kutoka kwa WERRASON bali kwenye Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

AJIRA YA FERRE GOLA KWA KOFFI OLOMIDE MOPAO MOKONZI
mwishoni mwa mwaka 2005, FERRE GOLA kajumuika na KOFFI OLOMIDE na kundi lake kwenye SHOO nyingi Mjini KINSHASA, ULAYA, na sehemu mbalimbali ulimwenguni. FERRE GOLA akiungana na Group QUARTIER LATIN, wakaingia STUDIO na kutoa SINGLE ” BOMA NGAI NA ELENGI ” (BONA NGA N’ELENGI). Uhondo na utamu utaupata utakapo sikiliza marudio ya wimbo “SISI SILIVI” usikilize hapo chini.
Baada ya hapo, FERRE GOLA katia kwenye ALBUM DANGER DE MORT wimbo wake maarufu INSECTICIDE.

 

MZOZO WAJITOKEZA KATI YA FERRE GOLA NA KOFFI OLOMIDE
Tukiwa tayari Mwaka 2006, maelewano kati ya FERRE GOLA na tajiri wake KOFFI OLOMIDE yakawa sio mazuri. FERRE GOLA akawa anagoma kufika mazoezini, hadi kufikia kutotokea kabisa kwenye SHOO zilizo fanywa kwenye ukumbi wa BATACLAN na ELYSÉE MONTMARTRE MJINI PARIS.
Kitendo hicho hakijamfurahisha KOFFI OLOMIDE, akawatuma wajumbe wamshauri kijana ili apate kujirekebesha na aendelee na muziki.
Tarehe 07 AUGUST 2006, KOFFI OLOMIDE na kundi lake walikua MJINI BRUSSELS (BRUXELLES) kwa ajili ya SHOO kwenye ukumbi wa MARIGNAN, huko pia FERRE GOLA hajaonekana huku akitoa sababu ya kwamba anaumwa. Sawa sababu inaeleweka, ila kwa mshangao Mkubwa kesho yake kaonekana kwenye sehemu maarufu MJINI BRUSSELS inayoitwa ATOMIUM akiimba kwenye KERMESSE iliyo andaliwa na wa KONGOMANI waishio hapo.

Subira za KOFFI OLOMIDE ziliisha, ndipo kamtafuta jamaa JÉRÔME MUTINGIA, alie faanikisha ujio wa FERRE GOLA QUARTIER LANTIN ili aingilie kati kwa kumshawishi FERRE GOLA atekeleze mkataba walio saini kati yao.
KWA NINI FERRE GOLA KASUSA KUFANYA MAZOEZI ? ITAENDELEA…

 

Advertisements

2 Responses to HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA. SEHEMU YA TATU

  1. Anonymous says:

    PICHA YA MAREHEMU ONYESHA PICHA

  2. I’ve bookmark your website and also include rss.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: