Fally Ipupa apata ajali

Habari zilizotufikia asubuhi hii zinasema kuwa Mwanamuziki Fally Ipupa amenusurika kifo baada ya gari lake aliyokuwa akiendesha aina ya  Bentley kupata ajali kwa kugongana na gari jingine huko Boulevard Barabara ya uhuru almaarufu kama 30 Juin huko Congo DRC.

Habari zinasema kuwa hakuna aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo iliyohusisha magari mawili ila abiria wamejeruhiwa akiwamo mwanadada aliyekuwa ndani ya gari ya Fally na kukimbizwa hospitali ya Ngaliema Falvien. Awali habari zilitapaa kuwa Fally amekimbizwa hospitalini hapo na kufanya watu kadhaa kufurika lakini ikathibitishwa na mashuhuda kuwa Mwanamuziki huyo kipenzi cha wengi yu buheri wa afya isipokuwa majeraha aliyopata mkononi mwake ambao awali ulisadikiwa kuwa umevunjika.

Spoti Starehe inawatakia wapone haraka na kurejea kwenye burudani.

jyk9bW1389213892

Wasamaria wema wakiwa eneo la ajali na kuwasaidia majeruhi.

JzyJhm1389213849

Sehemu ya gari ambayo Fally aligongana nalo usiku wa kuamkia leo.

kzCLPV1389213782

Mwanamama ambaye alikuwa kwenye gari iliyogongana na gari ya Fally akiwa kwenye gari ya wasamalia wema kukimbizwa Hospitalini.

GqQFFb1389212400

Gari ya Fally Ipupa aina ya Bentley ambayo ilipata ajali usiku wa leo huko Congo.

ciPbjw1389212507

Gari ya Fally aliyokuwa akiendesha mwenyewe ikiwa imefunguka Airbags baada ya ajali ya usiku wa leo.

Advertisements

2 Responses to Fally Ipupa apata ajali

  1. papa richard malewa says:

    Wadau muziki wa dansi unakufa jamani hapa Tanzania hasa zaidi Dar es Salaam. Hatuwezi tukaacha haya mambo yaende hivi hivi tatizo ni moja tu hakuna promo za maredio na zaidi TVs. Papa Pius tumieni kalamu yenu angalau hasa kwenye kipindi hiki kigumu kuwafanya Wanamuziki wa dansi wote waungane kutoa kilio chao maana angalau tungepata kituo kimoja itoe channel moja tu kwa ajili ya Muziki wa dansi basi tungepata pa kuponea. Hatuwezi kuacha wabana pua watu wasioweza kuimba live wala kupiga vyombo wanatawala kila kitu. Huku ni kuua utamaduni wa wa Watanzania. Vizazi vijavyo vitakuja kutujua sisi vipi kama haya mambo ya hip hop kubana pua ndiyo yanachukua kasi. Unaweza kuona Waganda vijana wao ndio wanapiga Muziki wa kileo lakini unaipata ladha na vionjo vya kiganda. Sisi tatizo letu hili tulitatue. Na nyinyi wanamuziki wa dansi msiwe wa kulalamika tu hoo hatupati promo shirikieni na hawa watoto lakini wekeni ladha ya muziki wetu mbona akina Choki zamani mlikuwa mnafanya kolabo na hawa vijana. Mwangalieni Fally Ipupa Di Caprio anaweka Pops lakini ladha ni Kikongo. Shime Shime jamani pelekeni matatizo yenu Kwa Waziri na hata Raisi mbona yeye aliwahi kusema hawezi kwenda kwenye majukwaa ya Muziki lakini akipata muda anasikiliza Sikinde Ikulu. Shime Shime Shime Wadau tuokoe Muziki wetu huuu alama ya Utambulisho wetu hapa duniani.

  2. numerous terrific details and inspiration, the two of which I will need, because of give such a beneficial details here.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: