Wa Combattants wasababisha show ya JB Zenith kuhairishwa.

image

Wa Combattants wakiwa katika maandamano jijini Paris Kupinga onyesho la Jb Mpiana Zenith

Lile onyesho lililokuwa likisubiriwa kwa hamu la Wenge BCBC katika uwanja maarufu wa Zenith limeshindwa kufanyika juzi jumamosi tarehe 21 Dec 2013.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shabiki na mwanablog wetu Lubonji wa Lubonji aliyeko huko Ufaransa zinasema kuwa siku ya Jumamosi Wa Combattants waliandamana kwa wingi Jijini Paris haijawahi kuonekana wa Africa kwa wingi tena kwa pamoja kama siku hiyo!!! Lengo likiwa wanataka onyesho lisiwepo” kilisema chanzo chetu.

Hali hiyo iliulazimu uongozi wa jeshi la polisi kuingilia kati na kuamuru kusitishwa kwa onyesho hilo kupitia Police Order No. 2013-01253 prohibiting one CONCERT at the ZENITH DE PARIS

Ha kuna njama yeyote, kwa uchunguzi wangu!!! hawa jamaa wana washutumu wanamuziki kua vibaraka vya serekali ya Joseph Kabila Kisa kingine kutokana na kauli yao wenyewe wanadai ya kwamba Joseph Kabila sio Mkongomani kwa maana hiyo hana budi kuacha madaraka na arudi kwao Rwanda!!!

akihojiwa jana na mwaandishi wa habari MAMI ILALA huko KInshasa JB MPIANA kasema amefanya gharama nyingi na hajui vipi atasawazishwa!!! hajaelewa kinachoendelea!!!

Wa Combattants kwa upande wao walitishia kabisa kufanya kweli yaani kulichoma moto Ukumbi wa Zenith de Paris ingawa JB MPIANA aking’ang’ania kufanya SHOO.

Wa Combattants ni mchanganyiko wa watu wenye kabila mbalimbali huko Congo na rika mbalimbali pia!!Utawakuta wasomi na wahuni kadhalika, “hao wahuni wanajulikana na Polisi mjini Paris, na ndo tishio kubwa hua hawaogopi mtu!!! niwatu wavurugu saana!!! wanapelekwa rumande leo na kuachiwa huru kesho au baada ya siku, wanasema hua wanajisikia vizuri kukaa jela….” kiliongeza chanzo chetu.

Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi uliopita kwa awamu zote mbili JB Mpiana pamoja na wanamuziki wengine walishiriki kumfanyia kampeni Rais Jose Kabila kwa kumtungia nyimbo jambo likilofanywa na wanamuziki wengine pia akiwemo Werasson, Tshalla Muana, Wazekwa na wengineo jambo lililowakasirisha Wa Combattants waopinga uhalali wa Rais Kabila.

Haijajulikana ni lini onyesho

Advertisements

4 Responses to Wa Combattants wasababisha show ya JB Zenith kuhairishwa.

 1. Jirani Mwema says:

  Nakumbuka Mwezi wa pili 2013 mlifurahia sana maana hata muelekeo wa uandishi ulionesha hivyo kama “Papy Kakol achezea kichapo toka kwa Combattant”. Heee heee usitukane Mkunga na uzazi ungalipo !

 2. Jirani Mwema says:

  Watajibeba wakarudishe gharama zao kwa Kabila waliompigia debe

 3. Anonymous says:

  Lakini kwa upande mwingine huu ndiyo ulofa, unyani, ujinga wa waafrika wa jamii hizi waliopo huko France. Mnaishi kama watumwa wa kujitakia wenyewe, mnaosha vyombo na vyoo vya wazungu, mnafagia mabarabara yao, kutwa kukimbizana na stamps za kununulia bidhaa za wamaskini, mnaosha vibibi na vibabu vya kizungu.

  Wazungu hao hao ndiyo wanaopora madini yenu na wapo huko huko Ulaya mbona hamuendi kuandamana na kuzuia uzalishaji kwenye viwanda vyao? pumbafu kabisa, na wengi wenu ninyi mliletwa ulaya kwa ujanja ujanja wa Wanamuziki hawa hawa. Kama mna uchungu na Kabila nendeni msituni mkashirikiane na M23 kupigana na Serikali ya Kabila. Mafala kabisa, watumwa mnaokula makombo na cowards wakubwa nyie.

 4. Anonymous says:

  Mbona Wera kamsapoti Kabila na Zaneth Show Kafanya Iweje Mukulu? Embu wekeni sawa hapa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: