Josky Kiambukuta hatunaye tena?

Habari zilizotufikia zinasema kuwa Mwanamuziki Josky Kiambukuta (64) amefariki dunia huko Ubelgiji.
Ingawa bado kuna utata juu ya habari hizi lakini habari zilizoenea mitandaoni zinadai Kiambukuta amefariki kutokana na shinikizo la damu. Kama ikithibitika hili litakuwa pigo la pili ndani ya mwezi mmoja hasa baada ya kumpoteza Tabu Ley siku kadhaa zilizopita.
image

Kiambukuta (Pichani) alitamba sana na kibao Chandra ambacho kinawika mpka leo aliwahi kufanyakazi na bendi kadhsa ikiwemo Bana OK, OK Jazz, L’Orchestre Continental, L’African Fiesta Sukisa.

Miaka ya mwanzoni mwa 60 Kiambukuta alifanyakazi na Luambo Luanzo Makiadi aka Franko mpaka miaka ya 80.

Baada ya Kifo cha Franko mwaka 89 waliendelea kupiga takribani miaka minne hadi mwaka 1994 wapokorofishana na kuparanganyika ambapo yeye pamoja SIMALOO LUTUMBA, DOMBE OPETUM, MAKOSSO, ZINGA NGOLE, Augustin NDILU, Papy BALAY, ENDO, Flavien MAKABI, KAJOS, Olivier SHIMANGA, Maurisson NDEKE « Sadam », ELBA TOP A, na CHAKEMBO. Kwa pamoja walianzisha bendi yao ya Bana Ok ambayo kwa kiasikikubwa ilifanikiwa na baadaye walitimkia Ufaransa ambako alikaa huko akiendelea na muziki na shughuli nyingine mpaka mauti yalipomkuta.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: