Kama Sio Koffi nani mwingine?

Unapozungumzia muziki wa Congo huwezi kumenga Koffi Olomide ingawa kuna wanaodai kuwa huyu jamaa sio Mcongoman kuwa ametokea Gabon na wengine wakisema mmoja wa wazazi wake anatokea Brazaville ndio asili yake lakini Koffi amekulia na kuzaliwa DRC. Koffi ametokea safari ndefu mpaka kufika alipofika leo lakini katika safari yake hiyo Koffi amekuwa akifanya vizuri kila stage anayopiga na amekuwa hawaaangushi mashabiki wake.

Wimbo huu original yake unaitwa Aspirine ulukuwa kwenye Albamu ya V12 ambayo ilitoka October 9 mwaka 1995 chini ya Producer Sonodisc, ilikuwa na nyimbo 11 kama Andrada, Parking Ya ba Baba, Chantou, Fouta Djallon, État Civil, Dossier du Jour, Aspirine, Nouveau Testament, Bambino
, Miss Toutsi na Zokere. Ni albamu ambayo wapenzi wa Rhumba mtakubaliana na mimi kuwa Rhumba za humu si mchezo.

Naikumbuka safu ya waimbaji walikuwa Suzuki Luzubu, Willy Bula ambaye ni kaka yake kabisa na Blaise Bulla, Babia Ndonga Chokoro, Bodogo Balongana , Eric Tutsi, Sam Tshintu, Makenga, Koffi Olomidé. Nilikuwa nampenda sana mpiga Solo wa Quartier Latin hii Beniko Popolipo ambaye amesekika vizuri mnoo na kwenye kwenye Bass kulikuwa na Binda Bass kama sikosei na atalaku alikuwa Bivens Bienvenue huku Koffi mwenyewe akichombeza kwa mbali. Hii ilikuwa ndio Concert yangu ya kwanza kumuona Mwanamuziki wa Congo ilikuwa ni Nairobi Makuti Club na mimi ikanikuta huko, sitoisahau safu hii na toka hapo nikawa na mapenzi makubwa na Koffi.

Kwa sasa Koffi ametangaza kustaafu muziki na kujikita kwenye biashara, yuko Studio akimalizia Albamu yake ya 20 tangu aanze muziki na atamuachia Cindy kuiongoza bendi huku yeye akibaki Mkurugenzi muendeshaji. Koffi anabishara na hasa hotel yake yenye hadhi ya nyota tano Hotel Delpiro na kampuni ya mambo ya utalii ndio vitamfanya awe busy navyo.

NAkuacha na kibao Aspirine kilichoimbwa tena na Cindy, hii ilikuwa Zenith mwaka 2009. Shukrani za Kipekee ziende kwa shabiki wangu Lwanyantika Masha mnazi na mdau wa Koffi na Werasson natumai tuko pamoja mkuu.

Advertisements

2 Responses to Kama Sio Koffi nani mwingine?

 1. I hardly create comments, however I looked
  at through some comments here Kama Sio Koffi nani mwingine?
  | Spoti na Starehe. I do have 2 questions for you if
  it’s okay. Is it simply me or does it look like some of these responses
  appear like they are written by brain dead folks? 😛 And, if you
  are writing on other online social sites, I would
  like to keep up with you. Would you make a list of every one of all your social community pages like
  your Facebook page, twitter feed, or linkedin profile?

 2. Very wonderful weblog and excellent and articles or blog posts.valuable layout, as share good things with excellent suggestions and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: