Exclusive: Papa Wemba na JB Mpiana wakiwa Studio, Nini kinakuja?

Baada ya kimya kirefu mwanamuziki Shumbu Wembadio Ekumay Papa Wemba anatarajia kutoa albamu yake mpya hivi karibuni na itazinduliwa rasmi tarehe 26 February 2014. Katika Albamu hiyo kuna kibao maalumu ambacho Papa Wemba amemshirikisha JB Mpiana kimeimbwa mahususi kwa ajili ya Mkubwa Patric Bolognia ambaye kama unafatilia muziki JB Mpiana kwenye Soyons Serieux anawimbo unaitwa Bolognia nao ameutunga maalum kwa tajiri huyu kijana.

Utasikia mtangazaji anamuuliza JB Mpiana na Papa Wemba kuwa wote wawili wanasauti ya juu sasa itakuwaje kwenye wimbo huo si wataua? JB Mpiana anajibu anamwambia hiyo ni sawa na timu ya mpira kuweka washambuliaji wawili unaweza fikiria idadi ya magoli itakuwa mengi.

JB Mpiana alisafiri na kuingia Ufaransa saa nne usiku akaenda Studio na kuingiza sauti kesho yake akageuza.

Wimbo huu umekuwa gumzo kila mtu akitamani kuusikia siku ukitoka, ikumbukwe kuwa PApa Wemba aliwahi kuimba na Koffi Olomide kwenye Musouksouk na Wake Up albamu ambayo ilibamba vilivyo na Kolabo yao ilikuwa nzuri sana isiyochosha kusikiliza kwani Koffi anaimba sauti ya Bass na Papa Wemba sauti ya Kwanza, hii inafanya watu kutamani kusikia hii kolabo la Papa Wemba na JB Mpiana itakuwaje?

Ngoja tungoje tusikie.

2 Responses to Exclusive: Papa Wemba na JB Mpiana wakiwa Studio, Nini kinakuja?

  1. netgear n300 dgn2200 manual says:

    What’s up, just wanted to tell you, I liked this blog post.
    It was funny. Keep on posting!

  2. Wonderful information, excellent and worthwhile style, as share superior things with great thoughts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: