Djodjo Ngonda; Wimbo Ulioleta utata wa uhalali wa kuutumia kati ya BCBG na WMMM

Wimbo huu ulikuwemo kwenye Albamu ya Pentagone ambayo ni moja ya albamu zenye mafanikio makubwa kwa Wenge Musica, Albamu hii ilijaa nyimbo nyingi zikiwemo Pentagone Wenyewe, Heritier Itere, Etepe Buengo, Filandu, No Comment Shengen, Cometes de L’an 2000, Dizoizo na nyingine kama nimesahau.

Wimbo huu wa Djodjo Ngonda uliwahi kuimbwa tena na WMMM ya Werasson na pia uliwahi kuimbwa sana kwenye maonyesho ya JB Mpiana na Wenge BCBG yake, jambo lililowachanganya wengi wa wafatiliaji wa mambo ya Muziki kuwa nani hasa mmiliki au mwenye uhalali wa kutumia wimbo huu.

Kwa Utunzi, Wimbo huu umetungwa na Maitre Ficare Mwamba ambaye alikuwa akipiga gitaa Wenge Musica. Ulifanyiwa arangement na Werasson na hata Wimbo ukianza anaonekana yeye mwanzoni hapo, ninaposema arangement namaanisha kuupangilia, we unaweza kutunga wimbo wako mtu akausikiliza akasema No, tuu imbe kwenye Key hii na Gitaa liiingine kihivi, hapo iwepo ghani au la.

Baada ya kupanguka kwa Wenge Musica na akina Werasson kujitoa Maitre Ficare Mwamba yeye alibaki na aliitendea haki vilivyo albamu ya TH – Toujou Humble ambayo ilikuwa double CD jambo lililompa JB Mpiana uhalali na uwezo wa kuutumia wimbo huu, Kwa upande wa Werason kuwa arranger wa wimbo ule alijiona ana uhalali wa kuutumia na ndio maana akatoa na remix yake ambayo ni hii hapa chini.

Nakusikilizisha na kukurudisha nyuma kumbukumbu zako kwenye wimbo huu wa Djodjo Ngonda. Najua ntakua nimekugusa sana kaka yangu na shabiki mkubwa wa BCBG brother Gabriel Nderumaki wa Daily News, tuko pamoja sana kaka yangu.

Advertisements

5 Responses to Djodjo Ngonda; Wimbo Ulioleta utata wa uhalali wa kuutumia kati ya BCBG na WMMM

 1. Farid 4x4 says:

  Asante sana Captain Pius kwa kutukumbusha makambo ya pentagone 1996

 2. Farid 4x4 says:

  Hahahahaha hio video ya Werassone nimeipenda sana mwishoni kuna mtoto wa miaka miwili ametoa show si ya kawaida

 3. safi sana nimeipenda hiyo.Je vipi kuhusu masuntra ya fere gora?

 4. tech speaker says:

  cool post! I truly appreciate your efforts and I am waiting for your next post. Hey, that is a clever way of thinking about it. No complaints on this end, simply a magnificent piece. On a scale from 1 to 10, You are an 11.

 5. I never discovered any attention-grabbing page post like yours. I am reading your blog while camping. No complaints on this end, simply a amazing piece. I bet you sweat glitter.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: