Annie wa Werrason ndani ya Kibuisa Mpimpa

Wengi wetu tunaijua kama Kibuisa Mpimpa lakini ilikuwa sokoni kwa jina la Operation Dragon na jina la biashara ni Kibuisa Mpimpa, BadoAlbamu hii kwangu inabaki kuwa ni Albamu Bora kabisa kupata kupigwa na Wenge Musica Maison Merre ya kwake Werasson Ngiama Makanda tangu walipotengana na Wenge Musica BCBG. Ilikuwa ni kazi ya kwanza tangu Werasson Kutoka Solo, Hii ni Albamu ambayo bado inafanya vizuri sokoni mpaka sasa ikiwa imetoka CD Mbili yenye jumla ya nyimbo 17 ikiwa na vibao kama Opération Dragon, 13 Ans, Un Prince au Congo, Fair-Play, Fleur d’amour, Waka Waka, Destin ya moto, Ntima Mbote, Croix Rouge, Kibuisa Mpimpa, Blandine, Tavé, Le Grand Monsieur, Obiang, Le Vent du Soir, Annie, Nakoyamba yo. Albamu hii iliweza kuziba midomo wote ambao walidhani Werasson asingeweza kutoka peke yake huku ikiwa ni Albamu Bora kwenye tuzo za Kora 2001.

inawezekana labda kwa sababu waimbaji na watungaji bora walikuwa bado ndani ya bendi naikumbuka safu nzima ya Maison Merre ya Kibuisa Mpipa ikiongozwa na Ferre Gola kichaa ambaye si tu alitunga bali alishiriki ku arrange nyimbo nyingi kwenye albamu hii ,Aimelia Lias Doming’ong’o ambaye ndio kwanza alitoka kwa JB na alitamba sana kwenye albamu ya Titanic, Adjani Sesele, Baby Ndombe ambaye kwa kiasi kikubwa alifanya kazi aliyoifanya Blaise Bulla BCBG wakati huo, Burkina Faso Kasongo Mboka Liya moja ya wapiga gitaa ninaowakubali sana na anaweza kucheza na Rhythim Gitaa vizuri na pia ni mtunzi mzuri, Flamme Kapaya ambaye anapiga gitaa pia na ameweza kuibeba WMMM mpaka waleo, Jdt Mulompwe huyu ni mmoja wa vijana ambao vipaji vyao Werasson alivitumia vizuri hasa katika safu ya uimbaji, Serge Mabiala si tu muimbaji na mtunzi bali ni music Aranger pia na alishiriki vizuri kwenye albamu hii,  alikuwemo pia Didier Lacoste huyu kwangu nasema hana bahati ya kufahamika na wengi ila ni muimbaji mzuri sana.

Pia kulikuwa na mghani atalaku Bill Clinton Kalonji ambaye kwa kiasi kikubwa alipunguza tambo za Tutu Kaluji wa BCBG kwa ghani zake naye pia ni muimbaji na mtunzi mbali na kuwa ataku, Pia alikuwepo atalaku mwingine handsome boy Sukari nyingine ya warembo kijana Celeo Scram ambaye alijitoa WMMM na sasa anatoka kivyake ambaye anaimba vizuri sana na pia ni mtunzi ambaye alilalamika kubanwa na Werasson, Pia alikuwepo Japonais maladi ambaye naye kuna wakati aliondoka na sasa amerejea ingawa anawakati mgumu wakigombea madaraka kundini huku akishiriki vyema kwenye gitaa, pia mpiga drums Papy Kakol aliitendea haki albamu hii hasa kwenye tamasha la Kora ni moja ya maonyesho ambayo WMMM waliyatendea haki vilivyo, na wengineo kama Shora mbonda, Sankara de Nkunta, na mpiga bass ambaye namkubali sana Mimicha mabye alikuwa akipiga Percussion:e bass na Thierry Synthe.

Advertisements

One Response to Annie wa Werrason ndani ya Kibuisa Mpimpa

  1. Hi there! This is my first visit to your blog! We are a group of volunteers and starting a new project in a community in the same niche. Your blog provided us valuable information to work on. You have done a extraordinary job!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: