Rachereau Tabu Ley afariki Dunia

image

Marehemu Tabu Ley enzi za Uhau Wake
image

Pichani Marehemu Tabuley akiwa kitandani Hospital huko Bruxelles.

Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Racereau au Tabu Ley amefariki Dunia leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa toka chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Tabu Ley amefariki Dunia leo asububi huko Bruxelles Ubelgiji.

Tabu Ley aliwahi kutamba sana na hasa kipindi alichofunga ndoa na Mbilia Bell ndoa ambayo ilivunjika baada ya muda.

Katika uhai wake Tabu Ley aliwahi kupiga Zingzong na wanamuziki kadhaa na kufanya maonyesho ya pamoja na wakongwe kama Koffi Olomide ambaye aliwahi kufanya onyesho la wazi (Live Concert) akiimba nyimbo za Tabu Ley (Koffi Chante Tabu Ley).
Kibao maarufu kilichotamba mpaka sasa ni Muzina ambao unatamba mpk wa leo.

Pia kuna wimbo kama Twende Nairobi ambao aliimba na Mbilia Bell. Mpaka kifo chake Tabuley alikuwa ametunga zaidi ya 200 na anasemwa ndio mwanamuziki wa kwanza wa Afrika kuuza nakala milioni moja kwa Single Albamu.

Tabuley aliwahi ingia matatani na Aliyekuwa Rais wa Zaire enzi hizo, ugomvi uliosababisha gwiji huyo kuishi uhamishoni.

Tutawaletea taarifa kadri tunavyozipata. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

2 Responses to Rachereau Tabu Ley afariki Dunia

  1. Prince George Jr. says:

    R.I.P Tabu ley

  2. I have bookmark your website and in addition include rss.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: