Fally Afanya kweli Abidjani

November 21, 2013

Katika muendelezo wa Fally Word Tour 2013, Mwanamuziki Fally Ipupa weekend hii alikuwa na onyesho huko Abdijan Cote Devoir. Ikumbukwe kuwa Abidjani ni moja ya ngome za wanamuziki wa Congo ambao wanapendwa sana huko.

Fally ndiye mwanamuziki wa Congo anayeongoza kwa kuwa na show nyingi kwa mwaka huu akiwa booked mwaka mzima kwa show za nje ya Congo. Maanamuziki huyu ambaye ni kipenzi cha wadada “Sukari ya Warembo” kwa sasa anatamba na albamu yake ya Power 101 yenye nyimbo kama Sweet Life ndani yake ambazo zinatamba vilivyo.

Ziara hii ya Fally ambayo itahitimishwa huko Dubai mwisho mwa mwaka huu imepewa jina la Power Tour 2013 ambapo atatembelea nchi sio chini ya saba, jambo linalomfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi za nje kuliko wote wa Congo kwa mwaka huu.

Fally Ipupa akiwasili kwenye ukumbi/Uwanja kufanya Sound Check kabla ya onyesho jioni yake.

MAshabiki wakishangilia huku wengine wakichukua kumbukumbu na simu zao za mkononi onyesho likiendelea.

Safu ya Wanamuziki wa Kiume wa Fally wakionyesha umahiri wao wa kucheza Power 101.

Baba Yuko kazini

Ukisikia Muziki si lelemama angalia hii ndio utajua.

Ni kawaida wanamuziki kubadili mavazi kila baada ya kuda fulani kwenye onyesho moja kunaongeza utamu, uhai na vionjo kwenye onyesho husika, Pichani Fally akiimbisha mashabiki moja ya nyimbo wazipendazo.


%d bloggers like this: