Allain Mpella kupiga na Wenge BCBG Zenith Dec 21?

Allain Mpella Afande

Kuna tetesi kuwa Allain Mpela akawemo kwenye jopo la wanamuziki ambao watatumbuiza Zenith Jumamosi ya Dec 21 huko Zenith.

Katika interview na kituo kimoja cha Television wiki iliyopita Afande Mpela ambaye aliwahi kutamba vilivyo na kundi la Wenge BCBG alisema kuwa akipata mualiko wa kushiriki toka kwa aliyemuita kaka yake JB Mpiana angependa kushiriki, “…nitashiriki bila tatizo kama Rais kaka yangu JB Mpiana ataniomba nifanye hivyo….” alisema Mpella.

Afande atakumbukwa daima kwenye onyesho la Zenith miaka takribani 15 iliyopita jinsi alivyokonga nyoyo zamashabiki akishirikiana na kina Titina Al Capone , Tutu Caluji , Aimelia Demingongo , Chai Ngenge , Seguin Mignon ambao kutoa Seguin hao wengine kwa sasa hawapo kundini.

Licha ya kuwepo na mikwara ya hapa na pale ya kutokuwepo kwa onyesho hilo bado mashabiki mamia kwa maelfu wanalizungumzia onyesho hilo hasa baada ya kukosa utamu huo kwa takribani miaka minne na ushehe.

wakizungumza juu ya ushiriki wa Mpella mashabiki mbalimbali walimtaka JB Mpiana kumhusisha nguli huyo hasa baada ya bendi hiyo kuondokewa na vinara wake ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa na na mchango mkubwa kwenye bendi hiyo. “akitaka awashike amchukue Mpella maana yule ana mashabiki wake na hasa akina dada wanampendaga sana” alisema Julie Westone Mcongoman anayeishi Tanzania alipozungumza nami mbali tu kuwa ni shabiki wa Mpiana anaimbwa sana na nguli.

Kwa upande mwingine inasemekana kuwa Allain Mpella anataka kutumia nafasi hiyo kujisafisha mbele ya mashabiki hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa bendi yake iko mazoezini huko Makanza Ngiri Ngiri kwa ajili ya uzinduzi wa albamu yake mpya.

Nakuonyesha Zenith iliyopita umuone mpella akifanya vitu.

Advertisements

2 Responses to Allain Mpella kupiga na Wenge BCBG Zenith Dec 21?

 1. Kembo wa Kemba says:

  Allain Mpella Kitoko Makasi
  Mimi napenda Mpella sana sana na ye na Tanzanie yoote nampenda sana yeye. Napenda Yeye akuwe Zenith show.
  Azante sana sana.

  Kembo Nr.

 2. Hadj Le Jbnique says:

  Confirmed,Alain mpela atakuwepo kushow luv siku hiyo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: