Fally Ipupa Kiboko, Yuko Booked Mpaka mwakani

November 8, 2013

Pichani Fally Alipokuwa akiongea na wanahabari juu ya Tamasha la MTV All Star Kwa Zulu Natal huko Durban Afrika ya Kusini alipotumbuiza jukwaa moja na akina Dbanji, Snoopy Dogy na wengineo Gonga hapa.

Baada ya kutoa albamu yake ambayo inatamba kwa sasa ya Power 101 Mwanamuziki Fally Ipupa ameendelea kutamba na kupanda chati kila kunapokucha huku akiwa na sho nyingi kuliko mwanamuziki yeyote wa Congo kwa Sasa. Muziki una nguvu ya kuunganisha maadui, Tarehe 25 na 26 Mwanamuziki Fally Ipupa alikuwa Mashariki mwa Kongo huko Kivu ya Kaskazini ambako alikuwa na shoo kubwa ya kufa mtu, Baadaye atapiga shoo moja huko Kinshasa mwanzoni mwa mwezi huu kabla ya kwenda Abidjan, Côte d’Ivoire tarehe 15 mwezi huu na inatazamiwa kutakuwa na maonyesho kama mawili na baadaye mwezi ujao Fally atakuwa Guinea huko Malabo hii ni December 14 na 15.

Baada ya hapo mwanamuziki huyo kipenzi cha wadada anatazamiwa kwenda nchini Cameroun katika jiji la Younde ambapo anatazamiwa kuwa na maonyesho kadhaa na baadaye atakwenda jiji la maraha Dubai ambapo atakuwa na maonyesho matatu kati ya tarehe 20, 21 na 22. Fally atapumziki na kufanya shopping zake mpaka usiku wa tarehe 28 December ambapo atasafiri kwenda Libreville, Gabon ambako atakuwa na onyesho tarehe 29 onyesho ambalo limepangwa kuhudhuriwa na watu wengi ikiwa ni mwisho mwa mwaka na hii itakuwa zawadi ya mwaka mpya kwao.

Fally ndiye mwanamuziki wa Congo aliye na mikataba mingi ya Show nje ya Congo kuliko mwanamuziki yeyete kwa sasa.


Wacongoman wa Tshengen wagawanyika onyesho la JB Mpiana Zenith

November 8, 2013

Swali la kuwepo kwa show ya Jb Mpiana ama kutokuwepo ndilo lililotawala midomo ya jumuiya ya Wacongoman wanaoishi Shengen. hii inafuatia kuwepo kwa taarifa kuwa kundi la Bana Congo ambao walishiriki kupiga marufuku maonyesho uya baadhi ya wanamuziki wa Congo huko Ufaransa, Belgium na Ujeruman kuripotiwa kugawanyika kufuatia taarifa za hivi karibuni kuwa wapo ambao bado hawataki kuwepo kwa onyesho hilo.

Duru za kimuziki kutoka Ufaransa ambako ndio nyesho hilo la Zenith la Desemba 21 litafanyika wanasema kuwa katika Mkutano na wanahabari huko Ufaransa majuzi Waandazi walitanabaisha kuwa sehemu kubwa ya mapato ya show hiyo itatumika kuchangia kwa waathirika wa vita huko Mashariki mwa Congo ambapo waathirika wakubwa walikuwa kina mama na watoto. Kwa mujibu wa taarifa upande wa Bana Congo (de Combattants) wanaopinga wanasema kuwa hakuna faida ya kuwa na show kama hiyo kwa kumuona kuwa JB Mpiana ni mmoja wa wasaliti.

“Baadhi ya de Combattants wanakubaliana na maelezo ya dhumuni la onyesho lililoelezwa na Producer wa onyesho hilo na muandaaji hasa ikizingatiwa kuna zaidi ya takribani miaka minne tangu mwanamuziki huyo mwenye wapenzi wengi toka afanye onyesho huko” kilisema chanzo cha habari alipozungumza nami. “…. kwa upande mwingine wengine wanakataa wakibaki na msimamo wao ule ule.

Mamlaka ya Zenith imeshatangaza kuwepo kwa show ya JB Mpiana na Ticket za Show kuanza kunadiwa huku mashabiki toka Ufaransa, Ubelgiji, Norway, Sweden, Ujerumani na kwingineko wakitazamiwa kushiriki.


%d bloggers like this: