GS1 Yakabidhi Barcode kwa Professor Jay

IMG_0315

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.

IMG_0319

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajube wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.

IMG_0323

Profesa Jay akionyesha kwa wanaandishi wa habari (hawapo pichani) mfano wa hundi/bango alilokabidhiwa likiwa na Barcode kwa Bidhaa yake.

IMAG0735

Pichani Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.

 

Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode.

Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.

Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.

Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.

Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.

2 Responses to GS1 Yakabidhi Barcode kwa Professor Jay

  1. Anonymous says:

    pich ya mlisho mgass

  2. kiese ngumbu says:

    mmbo powa na prof jay,na kumba musik,yake,kusema ana pendewa na demu kali,ina changaza watu yote,baliye muzaraha ju ya vicky. Aksanti

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: