CD Baby mkombozi wa Kuuza nyimbo kirahisi mtandaoni.

image

Suala la kuibiwa kazi za wasanii ni kilio cha kila siku toka kwa wasanii, lakini wengi wetu tunachelewa kwa sababu inawezekana uvivu wa kutafuta njia mbadala au mawazo mgando ya kufata utaratibu uliopo bila kuwaza ni jinsi gani unaweza kutanua soko lako.

Wasanii wakubwa wote hawategemei kuuza CD au DVD zao mitaani na kwenye Traffic Lights kwani kuna mfumo ulionyooka ambao nawawezesha wao kufatilia mauzo ikiwa ni pamoja na kuuza wenyewe Online kwa kutumia nyenzo kama iTune Store, CD Baby na nyinginezo.

Njia ya kuuza miziki Online inafanya uwe na uwanda mpana zaidi wa soko kwani unaweza kumuuzia shaiki wako aliyeko nje ya nchi kwa urahisi bila kwenda dukani au kutoka nyumbani kwake bali kwa kubofya tuu.

CD Baby ni kampuni ambayo inajishughulisha na kuuza nyimbo kupitia mtandao wa kijamii ikiwamo Facebook na mingineo, hii ni njia rahisi ya kuwafikia hao mashabiki wako (funs) wako kwani kwa ulimwengu wa sasa katika kila vijana wasomi wa mijini kumi at least nusu yake wanajihusisha na mitandao ya kijamii hasa facebook.

Hii ni njia rahisi sana ya kuwafikia mashabiki na kuongeza soko kwa kutumia mitandao hii ya kijamii kwa wasanii wetu. Dunia kwa sasa haiitengi Tanzania kuwa kijiji bali tunatakiwa kwenda na mabadiliko ya sayansi na Technolojia ili kuweza kukabilia na changamoto ya soko huria ambalo linaifanya dunia kuwa kijiji kwa kutumia teknojia hii ya mawasiliano.

Malalamiko ya wasanii wetu kuhusiana na wizi wa kazi zao kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na usambazaji mbovu wa kazi zao, jambo linalopelekea uchakachuaji kufanyika, wengi wa wasanii wanalalamika kupunjwa na mfumo wa usambazaji wa sasa ambapo msanii ananafasi ndogo ya ufatiliaji wa taarida za usambazaji na masoko.

Pamoja na kuwa na changamoto kadhaa kwenye mfumo husika ambapo wengi wa mashabiki hasa wa mitandaoni huishia kupakua (download) hizi nyimbo bila kulipa gharama zozote mtandaoni. jambo hili si tu linarudisha nyuma kimalipo bali linafanya uhuhishaji na urasimishaji wa sekta nzima kuwa mgumu kwani asilimia kubwa ya mapato ya nyimbo husika hayaendi kwa mwanamuziki mwenyewe na husihia mikononi mwa wajanja wachache ambao wanadownload hizi nyimbo na kutengeneza CD mitaani na kuiza.

Changamoto hii ni kubwa kwani kwa CD Baby inamtaka mwanamuziki kutotoa wimbo wake kwenye mitandao bali kuipeleka kwao kwa kwa utaratibu wa sasa wazalishaji huwa wanasambaza hizo nyimbo mpya ikiwa kama kuzitambulisha kwa mashabiki ambao mwisho wa siku hawanunui CD.

Suluhisho la hili ni kwa wanamuziki na wazalishaji wa Muziki wenyewe kutosambaza nyimbo zao na kutumia wauzaji walioidhinishwa na kunakuwa na Radio Version ambayo itatumika kama Promo kwa redio na kama mtu anaipenda basi aende kwenye maduka yaliyorasmi na ama mitandao ya kijamii kama hii ya CD Baby na kununua huko.

Ili uweze kuuza kupitia CD Baby unatakiwa kuwa mwanachama wa CD Baby ambapo utajiandikisha na kufungua duka lako kwenye mtandao. Unatakiwa kujaza Contact info zako, pili unajaza njia za malipo.

Nini Kinatakiwa?

Kwanza mwanamuziki anatakiwa kuwa na Barcode. Barcode inawezesha wimbo wako kuweza kupatikana na inatumika kama namba maalumu ya utambulisho wa wimbo wako. Barcode kwa wanamuziki wa Tanzania zinatolewa na GS1 Tanzania Pekee. Hawa ndio watoaji Pekee wa Barcode kwa bidhaa  za Tanzania. mbali na CD Baby kutoa huduma hii ya Barcode ambayo utalipia dola 20 kwa kila Albamu, bado inashauriwa kuchukua Barcode kwa GS1 Tanzania ambao pamoja na mengine utapatiwa Barcode ambazo si zitakutambulisha duniani bali zitakutambulisha kwa kuwa zina kiambishi cha nchi ambacho ni 620.

Unaweza kuwasiliana na Gs1 Tanzania kwa barua pepe: info@gs1tz.org au Simu Namba 0713666616 na 0713720725 kwa maelezo zaidi.

 

Account yako inaweza kutumikaje?

Sell your music on iTunes Kwa kuwa na account na CD baby utaweza kuuza nyimbo na CD zako kwenye iTunes, Amazon MP3, CDBaby.com, na nyingine nyingi zinazouza nyimbo kwenye mtandao. 

Wiki ijayo tutaangalia CD Baby inavyoweza kusambaza Wimbo na CD Yako kwenye mitandao mingine ikiwemo Amazon, Google Music, Itune, Rhapsody na kwingineko.

Imeataarishwa na Pius Pius Mikongoti, Afisa Muandamizi wa GS1 Tanzania watoaji wa huduma za Barcode.

11 Responses to CD Baby mkombozi wa Kuuza nyimbo kirahisi mtandaoni.

 1. phiniasbiseko@yahoo.com says:

  Leo umechemka sana,sasa hii habari ya cd baby na muziki wetu kipenzi,wapi na wapi? Tupe info za congo bwana!Spoti na Starehe <comment-reply@wordpress.com> wrote:

  a:hover { color: red; } a { text-decoration: none; color: #0088cc; } a.primaryactionlink:link, a.primaryactionlink:visited { background-color: #2585B2; color: #fff; } a.primaryactionlink:hover, a.primaryactionlink:active { background-color: #11729E !important; color: #fff !important; }

  /* @media only screen and (max-device-width: 480px) { .post { min-width: 700px !important; } } */ WordPress.com

  piusmickys posted: ” Suala la kuibiwa kazi za wasanii ni kilio cha kila siku toka kwa wasanii, lakini wengi wetu tunachelewa kwa sababu inawezekana uvivu wa kutafuta njia mbadala au mawazo mgando ya kufata utaratibu uliopo bila kuwaza ni jinsi gani unaweza kutanua soko lako.”

 2. mussa selemani simba says:

  i like it

 3. I Am Very Grateful As I Appreciate Cd Baby Via Barcode To Be The Saviour Of Music Artists. I Pray To God That I May Consult The Office For The Purpose Of Music, As A Young Coming Artist.

 4. Sem fighter says:

  Goldve fighter ft ngapama

 5. Gene Laramie says:

  numerous wonderful data and inspiration, the two of which I have to have, thanks to supply such a helpful facts here.

 6. michael j maroda says:

  na nyimbo nataka kuachia cjui kufungua account

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: