Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema.

Ingawa wimbo huu maarufu toka kwa Wenge ya JB Mpiana unajulikana kama utunzi wake JB Mpiana kiukweli kabisa Wimbo huu ni utunzi wake kijana machachari Zulema ambaye ni bonge la kipaji ambacho kiukweli kwangu naona kinapotea.

Zulema ni muimbaji mzuri ambaye kwa kipidi kirefu amekuwa akisumbuliwa na uteja kwa utumiaji wa madawa ya kulevya. JB Mpiana aliamua kumsaidia Zulema kama mdogo wake na kuna kipindi alipelekwa kwa wataalamu na kupatiwa ushauri nasaha ana alitangazwa kuacha matumizi ya madawa hayo.

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Nakutakieni Weekend Njema, Natumai Meree Gladys nakati ya Moshi utakuwa umefarijika sana na sauti ya Afande ambaye anasikika uzuri humu. Kiukweli kila mtu ameutendea haki wimbo huu na Verse yake kiujumla. Sikiliza unipe maoni yako.

Advertisements

9 Responses to Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema.

 1. Mimi pia nimeburudika hapo.

 2. PHINIAS BISEKO says:

  dah jamaa zulema yupo fiti,basi madawa yanawaharibu vijana wetu kimuziki.

 3. glady says:

  kwa mtindo huu itabidi tuzindue ! ! ! ! ha ha ha ha huu wimbo me naupenda sana tena sana hasa alipoimba emilia na afende yaani balaa leo umenifurahisha. kesho tutupie wa live papito remix video

 4. Frank clement says:

  kaka mbona kila siku ni habari za wasanii walewale jb, werasson, kofi olomide, fere gola na falii pupa. Nijuavyo mimi kongo zote mbili DRC na Brazaville xina haxina ya wasanii kama extra musica xangul, G7, Defao, Awilo, Dou dou Copa, Guy guy fall, na wengine kibao kiasi nikisema niwataje wote nahitaji page kama tatu, hivyo basi habari tunazipenda lakini tunaomba ulete za wasanii wote si hao hao kila siku, nadhani ukifanya hivyo blog yetu itakuwa bola zaidi na zaidi

 5. PETRO MZOPOLA says:

  Endelea kuweka v2 vywa maana pamoja xana.

 6. Hadj Le Jbnique says:

  Ni kweli ni vizuri kupata habari za wasanii wengine pia lakini wengine wanakua hawana jipya kimuziki wapo kama hawapo,mfano mtu kama defao yupo nairobi muda sasa,hana kitu kipya cha maana,G7 nao baada ya kufanya vizuri wakapotea hawana jipya,halikadhalika awilo na guy guy,kuna wengine hawako tena kabisa kwenye music,yupo mmoja alihit mbaya huko nyuma kila disco lilipiga nyimbo zake but now guess what?the guy he deliver pizza na pikipiki ATLANTA USA,kazi nzuri ukifanya haihitaji darubini,itaonekana tu na kuwa recognize

 7. Papa Kasapira says:

  Thanx papa micky maana nilikuomba utuwekee hili dude longtime merci mkuu

 8. RICHARD MALEWA says:

  Hiki kilikuwa “KITU MURUA” Kabisa. Ila naona kijana alitumika kutunga ila wakongwe ndio walichukua chati kubwa, JB Mpiana, Aimelia Lyase Demingongo, Afande Mpela, Le Professorial Julens Kibese, Shai Ngenge RIO,

 9. Anthony Ondeng says:

  KWA MARA YA KWANZA NIMEWEZA KUFUATA NGOMA AMBAZO NAZIPENDA KWA LUGHA AMBAYO NAELEWA. SHUKRAN. KWENYE MZIKI WA PAPITO REMIX, NANI SAUTI KWA 5.07 ANAINGIA PALE?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: