WIMBO GRACE À TOI GERMAIN : Nung’uniko la HUBA la JB Mpiana

Mapenzi yanauma, Mapenzi yanatesa, mapenzi yanasumbua, mapenzi yanakondesha, kipindi JB Mpiana anatunga na kutoa wimbo huu ndio kipindi ambacho mapenzi yalimtesa sana, hebu fikiria mkeo wa ndoa anachukuliwa na mtu unayemfahamu, anaenda naye sehemu ambazo mlikuwa mkikatiza wote, anakaa na marafiki wengine ambao walimuita shemeji akiwa na wewe na sasa wanamuita shemeji akiwa na mtu wa karibu yako?

Hii ni hali tete sana kimahaba kwa mtu maarufu kama JB Mpiana na hayo ndio yaliyomkuta kwa mkewe Kipenzi Amida Shatur mama na Daida pale mkewe kipenzi alipochukuliwa na tajiri Didi Kinuani  Mkurugenzi na mmiliki wa Groupe Dikin kampuni yenye makampuni chini yake pamoja na mambo mengine wanauza madini. Lakini kwa sababu ya upendo wa kweli Mamaa Amida alirudiana na JB Mpiana pamoja na kuwa alifanikiwa kuzaa mtoto na Didi mtoto aliyepewa jina la DIAM ikiwa ni kifupi cha majina yao, mtoto mwenyewe ndio huyo aliyebebwa na JB pichani chini akiwa na familia nzima.

19436

Ijumaa ya leo naomba nikuache na tafsiri ya Wimbo Grace A Toi Germain utunzi wa Suveree Mukulu Bin Adamu Jean Bedel Tshituka Mpiana Papa Cheri Papa Matikakana Baba ya Bana Sultan. Shukrani za Kipekee kwake Kamarade Lubonji wa Lubonji kwa mtohoo huu merci mingi sana kwako Suveree.

Au sommet du mont blanc Je re-salue November… : Kileleni mwa Mlima (Mont Blanc pokea salaam zangu November…
Amour eloko oyo esalema pona banso : Upendo kitu kilichoumbwa kwa ajili ya wote
Eclaquer nga porte na zolo mawa nanga : Leo hii Pendo lanifungia mlango usoni maskini mie!!!
Natikali isolée na couloir ya déception : Najikuta nikiwa mpweke nikijazwa na majonzi,Simanzi na masikitiko
Bolingo eboyi kosekisa nga : Pendo lanikosesha raha na tabasamu
Mawa efandeli nga na matama :Huzuni wajichora chavuni mwangu
Efungoli robinet ya pinzoli : Na kufungua Bomba la machozi
Soki ezalaki mayi ya Regideso : Ingekua machozi yangu ni maji ya Bomba ya (REGIDESO)Shirika la maji huko Congo
Mbele baye kolongola compteur : Basi kama tayari Bomba limesha fungwa kutokana na uwingi wa mtiririko wa maji
Bolingo po’nini Yo okomi Moselu na maboko manga Lokolaaaa ngolooo ?: Pendo kwanini watereza mikononi mwangu kama Samaki?
Germain Souries-moi : Germain Nionyeshe Tabasamu lako
Je t’en supplie (Je t’en supplie) : Tafadhali
Ba scenes ya ba amoureux Nakoma komona lokola bilili ya télévision(Germando) :Kwangu mimi kuwaona wawili wapendanao ni jambo ambalo silijui tena,Hua natizama kama picha kwenye TV (Germando)
Germain Souries-moi Je t’en supplie :Germain Nionyeshe Tabasamu lako Tafadhali
Koyenga yenga lokola kipekapeka Oyo azangaka fololo : Nikiwa nahaha mitaani kama kipepeo kinacho tafuta Uwa!!!
En me promenant nalokotaki la photo d’un jeune très sympa : kutokana na Mihangaiko hayo nimebahatika kuokota Picha ya Kijana Maridadi
j’avais bien voulu que djo ango asekisa nga : Ningependelea Kijana alieko kwenye Picha anionyeshe Tabasamu lake (anichekeshe)
photo ezalaka sourde pe muette : Kumbe picha hua haisemi wala haisikii
ordinateur ya nzambe par la prière epesaki nga identité naye nyonso : Baada ya kuingia kwenye maombi nikaenda kwenye computer ili nipate kujua vitambulisho vyake.
Germain Germando Rue de l’amour (Rue de l’amour) : Jina lake Germain Germando Unakaa kwenye Mtaa wawapendanao
Tu vis dans un oasis qui s’appelle affection : Unaishi kwenye OASIS inayoitwa Upendo
C’est pourquoi je t’aime (je t’aime) Germain Germando : Nikwamaana hiyo nakupenda (Nakupenda) Germain Germando
Rue de l’amour (Rue de l’amour) : Mtaa wa wapendanao
Germando T’es la musique de mon affection : Wewe ni wimbo niupendao
de nature aux couleurs d’un martin pêcheur Germando en… :Mwenye aina na rangi ya Kingfisher Germando…
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
Dedication : Heiin kombo nanga oyebi Adjola suba motema humm : Helin Jina langu walijua Adjola Suba moyo humm
kombo nanga oyebi iii Jacky Lomata Ya Germando : Jina langu walijua!!! Jacky Lomata kaka yangu Germando, Bébé mobondo Jean Tekbwe
Nzambe sala likamuisi Nzambe euh sala likamuisi oooh : Mungu Tenda maajabu Mungu fanya maajabueee!!!
Yanga Amida akoma à zéro mètre nanga : Naomba Mpenzi wangu Amida awe sana karibu nami,Daida Soraya Junior Fari
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
(Afande) nafikiri ni Portuguese language anayejua tafsiri yake haya!!!
Eyukera sentre amore Christian Bashila
Eyukera sentre amore Riva Menga
Eyukera sentre amore Max Mwanza
Eyukera sentre amore Renaud Busiko
Eje kamunere vaka Fanfan Longa
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
Mwana ya moto ata omelisi ye libele na butu :Mtoto asiekua wakwako utampa ziwa (kumnyonyesha) usiku kutwa na akapatwa na usingizi
na tongo tango akolamuka akotuna wapi baboti baye :Asubuhi atakapo amka ataanza kulia wapi walipo wazazi wake
Hernestine Mambweni ata yo okendeee : Hernestine Mambweni Hata kama waondoka…
Quand j’avais atteint l’âge de raison,Senado me disait : Nilivyo timiza age of reason
Senado kaniambia :
L’orgueil est la seule force de l’imbécilité :Jehuri ndio nguvu pekee za kijinga
Adida Royz
Bababi bobo bababi bobobo bobo bobo ubo
Grâce à toi Germando (Charles Kabuya) Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa

Ijumaa Kareem kwako Papaa Farid Al-Shukairy Mukulu wa Bakulu Merci mingi Papaa kila nikivaa Kanzu na Kofia nakukumbuka asante sana,  MaMeree Gladys nakati ya Moshi, heshima kwako, Hadji Le Jeebeeneeque umepotea sana mkuu, Sadiq Tiger Werasonique damu, Papaa Richard Malewa, Dj wangu Kipaso heshima kwako na mashabiki na wasomaji wote wa Blog yetu.

4 Responses to WIMBO GRACE À TOI GERMAIN : Nung’uniko la HUBA la JB Mpiana

 1. Anonymous says:

  hapo shwari mukulu papa pius.Namkubali JB Mpiana.Alifanya vizuri kumrudia mke wake amida shatur

 2. PHINIAS BISEKO says:

  Nakuomba mkubwa pius, ujaribu kugusia habari za wasanii wengine wanaofanya vizuri ka roga roga,alain kounkou.Tupe habari zote za wasanii wa congo braza na kin.

 3. glady says:

  mistari mizuri sana.

 4. Hadj le jbnique says:

  Nipo kamanda wangu,sema mishe mishe tu za hapa na pale lakini tuko pamoja. Nikipata…chance kama hivi siachi..Kupita…here..is ..always a place to be yani hunaga

  Kuhusu wimbo ni kweli papa sherii jb mpiana kipindi hiki alikua..na..hard time sana,na nyimbo zake nyingi mkizifuatilia kipindi hicho karibu..zote zilikua ni za kulialia tu na mafumbo kwa amida shatur.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: