Weekend njema na Blandine ya Le Roi De La Forret Ngiama Makanda.

Kwangu Kibuisa Mpimpa na Solola Bien zinabaki  kuwa ni moja ya albamu bora kabisa Werasson na WMMM kutengeneza tangu aachane na Wenge Musica.

Anaitwa LE ROI DE LA FORRET” NOEL NGIAMA WA MAKANDA a.k.a.WERRASON hii ilikuwa kipindi chake cha mwanzo cha kujitawala alipotoka na album yake ya Kibuisa Mpipa kama sijakosea maana hii ilikuwa ni Bonus Truck. Wakati huo bado akiwa na wataalamu wake kama akina Ferre na bado hajakimbiwa na wanamuziki wengi ambao kwa sasa wanatamba sana.

Wimbo huu aliuimba kwa mahadhi ya Congo Rhumba, Ikumbukwe kuwa albamu hii ni mapishi ya Producer hatari mtaalamu  L. NZIMBI huyu ndiye mpishi wa albamu ambayo mpaka leo inauza ya FEUX DE L’AMOUR” yakwake Jemedari SOUVERAIN LEADEUR YA BA WENGEE JB Mpiana ambayo aliitoa kama solo enzi kundi la Wenge Musica BCBG halijaparanganyika.

Huu ni moja ya nyimbo ambazo mimi binafsi Werasson amenifurahisha na kama ningepata nafasi ya kukutana naye na kumshauri ningemshauri a stick kwenye nyimbo hizi za taratibu.

Kitu inaitwa Blandine wakati huo wa Kibuisa Mpipa, Ni wimbo ambao huku kwetu hauku heat lakini ni moja ya nyimbo ambazo nazipenda sana kwa Werrason, Kwa ufupi angalia nyimbo zinazombeba zaidi Werasson ni nyimbo hizi za taratibu zenye mahadhi ya Congo Rhumba ambayo Mkongwe JB Mpiana ni champion kwenye hizo najua ma werasonique mtabisha kwa hili lakini ni wazi na halipingiki.

Truck hii nilimsikilizisha Papaa Mabamba Abiud Maregesi weekend hii na akaniomba niiweke tena, Nimefanikiwa kumbadilisha huyu jamaa imani na mapenzi ya muziki pia ni maalum kwa Mukubwa Stephen Masere, Lubonji wa Lubonji heshima kwako sana, pamoja na Ma-Werasonique wooote Sadiq Tiger, Papaa Maendeka, Boss Chizenga, Moto Mkubwa Halid Mmanzi, Mdau wangu Steven na wapenzi wote wa Blog hii, Mukubwa Hadji Heshima kwako kiongozi na mnazi wa Wenge bila kukusahau Richard Malewa na mamaa Gladys Titanike nakati ya Kibo Poutry Moshi One Love Mameree.

Ijumaa Karim

Advertisements

3 Responses to Weekend njema na Blandine ya Le Roi De La Forret Ngiama Makanda.

  1. glady says:

    blandine ni nyimbo isiyochosha kusikiliza na pia hapo na unapogundua sauti ya werra kwa wale wanaosemaga werra haimbi bali anaongea, ila kwa kwa upande wangu mimi jb mpiana ni bora zaidi na wale wanaosema jb ameshuka wanakurupuka, na hizo albamu mbili ulizozitaja hapo juu kwangu ni bora kuliko album nyingine zote za werra

  2. phiniasbiseko@yahoo.com says:

    Duh na mimi  unifagilie bwana,siyo  kila siku akina jbnique na werrasonique.pia jaribu kuangalia na nyimbo za wasanii wengine kama awilo, ala

  3. Farid 4x4 says:

    Yaa Ngiama Wera yo ozali wapi yaya

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: