Happy Anniversary kwetu

387285_10150993246120154_773730153_22252945_2020409680_n

Tarehe 24 August 2001 nilifunga ndoa na mke wangu mpenzi Isabella Ghaty, mpaka leo tarehe 24 August 2013 ni takribani miaka 12 tumetimiza. Ni Miaka 12 ya ndoa iliyotanguliwa na miaka mingine sita ya kufahamiana hivyo kufanya maiaka 18 ya urafiki ambayo mi naijali sana.

Nasema naijali kwa kuwa urafiki ndio hudumisha upendo na kama hakuna urafiki ni sawa na kujenga nyumba kwenye mchanga bila misingi imara ni wazi msingi usipokuwa imara lazima ipo siku nyumba hii itaanguka au kama kunatokea dhoruba ni rahisi mjengo huu kuathirika.

Ni miaka 18 yenye historia, kwa vijana tuliooana kwenye umri mdogo chini ya miaka 25 ni wazi tunapitia majaribu mengi kama kwenye wimbo wa Voyage ya Mboso Dominguez amesema Safari isiyo na taa kwani hujui cha kesho ila mnakwenda tuu, mambo mengi yamepitia ikiwemo machungu na mazuri, katika safari ambayo tulishuhudia kumpoteza mtoto wetu Kipenzi Loreen ambaye aliugua na kufariki ghaflam ni machungu ambayo huwezi muadithia mtu lakini kwa kudra zake mola tumeyapita yote na bado tuko pamoja.

Namshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema kama wewe Mamaa Ghaty kwani sijuti kukujua na wala sijuti kukuoa natumai Mungu aliye mwema atatuongoza mpaka kifo kitakapotutenganisha. Pia kwa namna ya pekee twamshukuru kwa wanetu Glory na Geebril, twamuomba waongoze na kuwapa hekima ili waweze kufuata nyayo za wazazi wafanikiwe katika maisha yao.

Nawaacha na Kibao Voyaje ya Mboso toka kwao Wenge Musica BCBG chini ya utunzi wa Adolph Dominguez.

Kwa kifupi katika wimbo Voyage (Safari ) Mwimbaji Adolphe Dominguez anaongela Safari na hatari zake kwa wapendanao!!!

Nini toweli ngai nayoo : kitugani kinacho leta ugonvi kati yetu?
Awa natikali Likombe yaya : Tizama ninavyo baki mpweke Kaka yangu!!!

Wapi O remplacer Ngai Voyage : Safari, Lini ukaja kuchukua nafasi yangu kwenye ndoa…

Mbala ya sima nako Refuser : mara nyingine sintokubali (usafiri)
Voyage!!! Ponini usalaka boye!!! : Safari!!! kwanini hufanya hivyo!!!

Okotika moto na Soucis!!! : wafanya mtu kabaki na majonzi
Désespoir na kati ya motema : Moyo wangu wakata tamaa!!!
Soki Likambo nani ako Consoler!!! ikitokea neno, nani yule atakae nifariji!!!

Soki Likambo nani akosalisa : nikipatwa na shida ni yupi atakae nisaidia!!!

Tuna Meje Kanuse ndenge azangaki Mc Mpanda kaka mpo na voyage : Muulizeni Meje Kanusi alivyo mkosa mpenzi wake Mc Mpanda kutokana na Safari.

Marie France Shungu azangaka Béa!!! kaka mpo na Voyage : Marie France Shungu nae kaachana na Béa kutokana na Safari!!!
Tuna Jeannot Canon ndenge azangaki Sabartino kaka mpo na voyage!! :
Muulizeni pia Jeannot Canon alivyo achana na Mpenzi wako Sabartino kisa ni Safari.

Usikose ijumaa nitaumalizia, Shukrani za Kipekee kwa kaka Lubonji wa Lubonji kwa Tafsiri hizi mwanana.

5 Responses to Happy Anniversary kwetu

 1. Papa Richard Malewa says:

  Hongereni sana naona mnazidi kufanana siku zinavyozidi kwenda. Mwenyezi Mungu awabariki kwenye 12th Anniversary ya NDOA YENU.

  BIG UP

 2. glady says:

  kaka hongera sana miaka 12 ya ndoa na miaka 8 ya urafiki si mchezo, nawatakia baraka na maisha mema na MUNGU awalinde na ya walimwengu, voyage ni kibao na kipenda sana tena bila kujua tafsiri yake, asante kwa kutupa tafsiri kaka.

 3. Shaibu Mwambungu says:

  nakutakieni kheri nyingi katika safari yenu hiyo ya maisha ya kindoa ni mfano unaopaswa kuigwa na vijana Hongereni sana

 4. From my tiny lessening of view I would tend to disagree like that. There are not evidences nor definite proofs of that but I will leave the more experts forum bloggers to run by it better than I could following my needy words. Too many become old we understandably regard as being others and the others’ ideas without having a sure union of the situation or of what these people may be going thru. We’re often too superficial and this makes us throw our judgements without reflecting upon the subject enough. This is my 2 cents. IMHO.

 5. Susan Crawn says:

  I undoubtedly delight in just about every small bit of it and I have you bookmarked to examine out new stuff of the website a should read through blog site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: