Christian Bella Mkali wa Bongo Rhumba

Kipimo kikubwa cha mwanamuziki hasa wanaoimbia kwenye bendi ni pale wanapotaka kutoka peke yako (Solo). Nasema ni kipimo kikubwa kwani hata waliona majina makubwa wamejikuta wakibwagwa na soko na mashabiki na wengine wameishia kubadili fani. Nani asiyejua Kilichompata Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Titina Alcapolne na wengineo wakubwa wanje kwa humu ndani kuna watu kama Ndanda Kosovo Kichaa, ambaye kwa wakati fulani jina lake lilikuwa juu akaamua kutoka kivyake lakini hakufanikiwa.

Nimeanza na kukukumbusha hilo kwani kwa mwanamziki kama Christian Bella angeweza kuwa Ferre Gola wa Tanzania na kama napata nafasi ya kuongea naye ningemwambia akomae kwenye nyimbo za taratibu tuu, Bella ni mmoja wa wanamuziki ambaye si tu anakipaji kikubwa cha utungaji bali hata cha kuimba bila kukinaisha. Sio kila mwanamuziki anaweza kuimba wimbo mrefu akakuvutia lakini nachelea kusema kuwa Bella ameonyesha kuwa anaweza.

Aina ya muziki anaopiga kiukweli huwezi kufananisha na wengine kwani anauwezo wa kujitengenezea mashabiki wake tuu, Tanzania hakuna bendi ya muziki wa dansi inayopiga Rhumba kiukweli, na ndio maana kwenye albamu ya Dunia Kigeugeu ya FM Academi nyimbo kama Acha Tamaa zilishika na bado watu wanazipenda mpaka wa leo kwani ni aina ya nyimbo ambazo ni nadra sana kuzisikia. Binafsi natamani sana niendelee kumsikia mtu kama Bella akiendelea na Marhumba haya ya ukweli atupe burudani mashabiki wa Rhumba.

Bella anaweza kabisa kuendelea aina hii ya muziki ambayo itakuwa ni style yake, kiukweli nimemiss kusikia hivi vitu toka kwenye bendi za densi za nyumbani Bongo Rhumba ni style ambayo Bella, au Rogert Hega au Ige Muyamba wanaipatia sana sijui ni kwanini tu hawatii mkazo humo.

Ukisikiliza wimbo huu ambao ameshirikiana na mtaalamu mwingine wa masauti Banana Zollo utakubaliana na mimi kuwa Bella ni kiboko. Nakutakia Jumatatu tulivu.

2 Responses to Christian Bella Mkali wa Bongo Rhumba

  1. Anonymous says:

    nimewahi kupata clip yake mmoja hapa, huyu kijana ako sawa kama ataendlea na mziki huu wa rhumba. Shida ni kwamba kupata muziki wake hapa kwetu ni shida.ningefurahi sana kama ningelipata dvd zake za live perfomance.

  2. Anonymous says:

    nimewahi kupata clip yake mmoja hapa, huyu kijana ako sawa kama ataendlea na mziki huu wa rhumba. Shida ni kwamba kupata muziki wake hapa mobasa( kenya) ni shida.ningefurahi sana kama ningelipata dvd zake za live perfomance.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: