Happy Anniversary kwetu

August 26, 2013

387285_10150993246120154_773730153_22252945_2020409680_n

Tarehe 24 August 2001 nilifunga ndoa na mke wangu mpenzi Isabella Ghaty, mpaka leo tarehe 24 August 2013 ni takribani miaka 12 tumetimiza. Ni Miaka 12 ya ndoa iliyotanguliwa na miaka mingine sita ya kufahamiana hivyo kufanya maiaka 18 ya urafiki ambayo mi naijali sana.

Nasema naijali kwa kuwa urafiki ndio hudumisha upendo na kama hakuna urafiki ni sawa na kujenga nyumba kwenye mchanga bila misingi imara ni wazi msingi usipokuwa imara lazima ipo siku nyumba hii itaanguka au kama kunatokea dhoruba ni rahisi mjengo huu kuathirika.

Ni miaka 18 yenye historia, kwa vijana tuliooana kwenye umri mdogo chini ya miaka 25 ni wazi tunapitia majaribu mengi kama kwenye wimbo wa Voyage ya Mboso Dominguez amesema Safari isiyo na taa kwani hujui cha kesho ila mnakwenda tuu, mambo mengi yamepitia ikiwemo machungu na mazuri, katika safari ambayo tulishuhudia kumpoteza mtoto wetu Kipenzi Loreen ambaye aliugua na kufariki ghaflam ni machungu ambayo huwezi muadithia mtu lakini kwa kudra zake mola tumeyapita yote na bado tuko pamoja.

Namshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema kama wewe Mamaa Ghaty kwani sijuti kukujua na wala sijuti kukuoa natumai Mungu aliye mwema atatuongoza mpaka kifo kitakapotutenganisha. Pia kwa namna ya pekee twamshukuru kwa wanetu Glory na Geebril, twamuomba waongoze na kuwapa hekima ili waweze kufuata nyayo za wazazi wafanikiwe katika maisha yao.

Nawaacha na Kibao Voyaje ya Mboso toka kwao Wenge Musica BCBG chini ya utunzi wa Adolph Dominguez.

Kwa kifupi katika wimbo Voyage (Safari ) Mwimbaji Adolphe Dominguez anaongela Safari na hatari zake kwa wapendanao!!!

Nini toweli ngai nayoo : kitugani kinacho leta ugonvi kati yetu?
Awa natikali Likombe yaya : Tizama ninavyo baki mpweke Kaka yangu!!!

Wapi O remplacer Ngai Voyage : Safari, Lini ukaja kuchukua nafasi yangu kwenye ndoa…

Mbala ya sima nako Refuser : mara nyingine sintokubali (usafiri)
Voyage!!! Ponini usalaka boye!!! : Safari!!! kwanini hufanya hivyo!!!

Okotika moto na Soucis!!! : wafanya mtu kabaki na majonzi
Désespoir na kati ya motema : Moyo wangu wakata tamaa!!!
Soki Likambo nani ako Consoler!!! ikitokea neno, nani yule atakae nifariji!!!

Soki Likambo nani akosalisa : nikipatwa na shida ni yupi atakae nisaidia!!!

Tuna Meje Kanuse ndenge azangaki Mc Mpanda kaka mpo na voyage : Muulizeni Meje Kanusi alivyo mkosa mpenzi wake Mc Mpanda kutokana na Safari.

Marie France Shungu azangaka Béa!!! kaka mpo na Voyage : Marie France Shungu nae kaachana na Béa kutokana na Safari!!!
Tuna Jeannot Canon ndenge azangaki Sabartino kaka mpo na voyage!! :
Muulizeni pia Jeannot Canon alivyo achana na Mpenzi wako Sabartino kisa ni Safari.

Usikose ijumaa nitaumalizia, Shukrani za Kipekee kwa kaka Lubonji wa Lubonji kwa Tafsiri hizi mwanana.


Tafsiri ya Wimbo Dis moi Amour

August 26, 2013

NA LUBONJI WA LUBONJI

Nawaleteeni Tafsiri ya Wimbo Dis Moi Amour ambao unapatikana kwenye albamu ya TH ya Wenge BCBG chini ya JB Mpiana, ni moja ya Rhumba ambazo kiukweli bado zinapendwa sana mpaka wa leo, Shukrani za kipekee kwa Le Suveree Lubonji wa Lubonji ulipotea sana kaka karibu tena natumai umekuja na mengi toka likizo yako.

Wimbo huu ni umeungwa na Kuimbwa na JB Mpiana Mukulumpa Le Maréchal Mukulu.

Seul Les Enfants savent aimer sans calcul. Dis moi Amour I love you:
Watoto pekee ndio wanao uwezo wakumpenda mtu bila hesabu yeyote.

Niambie mapendo I love you…
Comme une graine de diamant dans le deser ,amour je t’avais long temps cherché sans succès!!! sans succès!!! :
Kama vile kutafuta mchanga wa alimasi jangwani, pendo nakutafuta siku nyingi bila mafaanikio

oh ce soir mon coeur me souffle certaine melodie pour toi Amida ,moi ma claté ta beauté un Chef d’œuvres divin :
oh usiku wa leo,moyo wangu wapata pigo na msukumo wa kuimba wimbo huu kwa ajili yako Amida mtoto mwenye uzuri na urembo kutoka kwa Mungu.

Embrassé moi, serre moi dans te bras, mais dis moi pourquoi, tu m’envoûtes si tant,
mon jardin des roses, Amida tu exaltes le parfum du paradis!!! voilà que tu me rends si fou de toi!!! :

Nibusu,nikumbatie,niambie kwanini wanivutia sana namna hiyo, wewe ni bustani yangu ya pink flower, Amida wanukia marashi ya mbinguni,tizama wanifanya niwe kichaa kwa ajili yako.

Je t’aime, i love you,na kupenda sana oooh l’amour toujour, l’amour :
Nakupenda,oooh mapendo kila mara mapendo!!!

Tu fais le bonheur des uns, tu fais le bonheur des autres :
Mapendo !!! waleta furaha na raha kwa wamoja, wajaza majonzi na machozi kwa wengine.

Amour mystère dis moi ton identité eeee!!! qui es tu uuuuuu!!!
Mapendo wewe ni fumbo pia ni siri jitambulishe basi!!! wewe ni naniiiii!!!

Amour dis moi quel est ton Pays, pour que je vienne et que je construise un Paradis plein de toi!!! :
Mapendo niambie inchi yako ni ipi ili nije na nijenge paradise iliojaa wewe peke yako.

entourer d’une muraille de sécurité pour autre amour :
Bustani yenyewe nitaijengea ukingo mrefu wakuzuia pendo zingine zisije kupenya!!! .

Contre les charlatans de l’amour!!! contre les trafiquants de l’amour!!!:
ukingo utakao zuia walaghai wa pamenzi, pia waongo wa mapenzi!!

Amène moi ce soir!!! Amida!!! à la planète Venus!!! Amida, la planète des amoureux!!! Amida!!! conduis mois s’il te plait!!! Amida!!!:
twende wote usiku wa leo!!! Amida!!! kwenye sayari Venus!!! Amida!!! sayari ya wapendanao!!! tuongozane njia tafadhali!!! Amida!!!

Kataja majina kadhaa kwa kuwa dedication : MIMI KALUDJI,NÉNÉ MAKITAKANA,NELLY BOMEI, JACINTHE MWANANGANI, SHANY SHATUR, GRACE NJEKA, LILLY LA RÊVE MATITI…
Asanteni Bana Wenge Musica!!!


Sebene la Ngwasuma Balaa

August 26, 2013

Ni Moja ya bendi za Tanznaia ambayo imekaa kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu na kujipatia mashabiki wake ambao wengine wanaifata hata iende wapi, majina kama Madenge, J Single, Abdul Tall, Ndama aka Akayesu, Julie Weston Ilunga aka Babaa B na wengineo, ni majina utayasikia kila siku bendi hii ikipiga hata iwe tunduma au Mlimba. Hii ni kuonyesha ni jinsi gani wamejipatia nafasi yao kwenye soko la burudani bongo hii.

Nawakubali sana Ngwasuma ikija suala zima la Sebene, wanavyojituma bila kulewa sifa za mashabiki wao, hebu angalia video hii uone ma stage show walivyolishambulia jukwaa.


Christian Bella Mkali wa Bongo Rhumba

August 26, 2013

Kipimo kikubwa cha mwanamuziki hasa wanaoimbia kwenye bendi ni pale wanapotaka kutoka peke yako (Solo). Nasema ni kipimo kikubwa kwani hata waliona majina makubwa wamejikuta wakibwagwa na soko na mashabiki na wengine wameishia kubadili fani. Nani asiyejua Kilichompata Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Titina Alcapolne na wengineo wakubwa wanje kwa humu ndani kuna watu kama Ndanda Kosovo Kichaa, ambaye kwa wakati fulani jina lake lilikuwa juu akaamua kutoka kivyake lakini hakufanikiwa.

Nimeanza na kukukumbusha hilo kwani kwa mwanamziki kama Christian Bella angeweza kuwa Ferre Gola wa Tanzania na kama napata nafasi ya kuongea naye ningemwambia akomae kwenye nyimbo za taratibu tuu, Bella ni mmoja wa wanamuziki ambaye si tu anakipaji kikubwa cha utungaji bali hata cha kuimba bila kukinaisha. Sio kila mwanamuziki anaweza kuimba wimbo mrefu akakuvutia lakini nachelea kusema kuwa Bella ameonyesha kuwa anaweza.

Aina ya muziki anaopiga kiukweli huwezi kufananisha na wengine kwani anauwezo wa kujitengenezea mashabiki wake tuu, Tanzania hakuna bendi ya muziki wa dansi inayopiga Rhumba kiukweli, na ndio maana kwenye albamu ya Dunia Kigeugeu ya FM Academi nyimbo kama Acha Tamaa zilishika na bado watu wanazipenda mpaka wa leo kwani ni aina ya nyimbo ambazo ni nadra sana kuzisikia. Binafsi natamani sana niendelee kumsikia mtu kama Bella akiendelea na Marhumba haya ya ukweli atupe burudani mashabiki wa Rhumba.

Bella anaweza kabisa kuendelea aina hii ya muziki ambayo itakuwa ni style yake, kiukweli nimemiss kusikia hivi vitu toka kwenye bendi za densi za nyumbani Bongo Rhumba ni style ambayo Bella, au Rogert Hega au Ige Muyamba wanaipatia sana sijui ni kwanini tu hawatii mkazo humo.

Ukisikiliza wimbo huu ambao ameshirikiana na mtaalamu mwingine wa masauti Banana Zollo utakubaliana na mimi kuwa Bella ni kiboko. Nakutakia Jumatatu tulivu.


%d bloggers like this: