Bado “namlilia” Chai Ngenge

Kiukweli naipenda sana Wenge BCBG na huwa siwezi kuficha hisia zangu kwenye hilo, lakini kwa miaka ya karibuni karibu watu wote ambao binafsi nilikuwa nawapenda sana ndani ya bendi hii wameondoka.

Pengo kubwa la kwanza kwangu ilikuwa kuondoka kwa Aimelia ambaye nilimpenda sana alivyokuwa akichanganya sauti yake humo, ila huyu hakuniuma sana kwani JB Mpiana alikuwa na uwezo wa kuliziba pengo lake vilivyo na kwa wasio wajua kwa sauti zao huwezi kujua akiimba JB Mpiana au akiimba Aimelia Lyase Doming’ong’o. Pia kwa mtu kama Titina Alcapone ambaye aliwachezesha vilivyo kwa upigaji wake hatari wa drums, kidoogo naye amepokewa vizuri na Seguine Mignon ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa ndiye mpambe wa kribu kabisa wa JB Mpiana na muda mwingi anakuwa naye na ndiye mtunza siri wake huku wangine wakimtania kuwa Kaka yao akina Daida, waototo wa JB Mpiana.

Pendo jingine ambalo bado naliomboleza mpaka leo ni kuondoka kwa Allain Mpella Afande ambaye kwenye wimbo huo hapo anasikika kuanzia 4:06 na sauti yake mwanana, kiukweli Pengo la Afande halijazibika mpaka leo kwani alikuwa akiimba sauti ya Pili na ya Tatu vilivyo. mbali na wengine ambao waliondoka ondoka hapo katikati kwa sababu moja au nyingine.

Sio siri kuondoka kwa Tutu Kaludji pia kulikuwa tingisho jingine kwa JB Mpiana, lakini kwa wafuatiliaji wa mambo walilijua hili hata JB Mwenyewe alilijua pia na kumpa nafasi zaidi Genta Macine ambaye ndiye atalaku namba moja, nasema hivi kwa sababu habari za Tutu Kaludji kutaka kuondoka zilianza tangu 2010 na Kaludji anasemwa alijikita zaidi kwenye kuimba na ndipo wapambe wakamstua JB Mpiana kuwa jamaa anataka kuondoka na alikuwa na mpango wa awali wa kutoa nyimbo zake jambo ambalo JB hakulifurahia.

Wakati anatunga kibao cha Tchico Londonien inasemwa alitaka kiwemo ndani ya albamu yake na ndipo hapo walipoanza misuguano ya chini kwa chini na Boss wake JB Mpiana, inasemwa mgogoro wao haukuwahi kuripotiwa popote lakini watu wa karibu walijua na walikuwa wakichekeana na kukaa pamoja lakini kila mmoja rohoni alikuwa na yake. JB Mpiana sio mtu wa kisasi na hapendi kusemwa pembeni ili kusimamia hilo JB huwa anavijana wake ambao amewapandikiza kwenye bendi ili kumpa taarifa na mmoja wapo ni Seguine Mignon ambaye anatoka kabila moja na JB Mpiana.

Seguine Mignon (Segee) ndiye mpambe wa JB Mpiana anayeogopwa sana na wana bendi kwani anaushawishi mkubwa sana na amewatupa wapambe wengine mbali, Seguin anaaminiwa sana na JB Mpiana kiasi kwamba hata wakiwa kwenye show chupa ya maji ya kunywa ya Mukulu JB Mpiana anaishikilia na kukaa naye Seguin.

Ukaribu huo ndio uliomgharimu Chai Ngenge ambaye aliwahi kuwa rafiki na swaiba mkubwa sana wa JB Mpiana. Chai Ngenge alikuwa karibu sana kipindi JB Mpiana anapata matatizo na mkewe Amida Shatur na alimfariji mnoo na kumuuunganisha kwa Mchungaji ambaye alisaidia kumpa moyo na mafundisho JB Mpiana jinsi ya kukabiliana na hali hiyo kwanni alimpenda sana mkewe.

Chai alikuwa na mapenzi makubwa sana na Wenge kiasi alijitoa mno lakini ukaribu wa Seguin na JB Mpiana ulimfanya akarudisha moyo nyuma jambo lililomgharimu mwishoni.

Walipokuja nchini nilipata nafasi ya kukutana na Chai Ngenge kwenye Mgahawa wa Food World alipokwenda kununua simu akiwa na wapambe nikajitambulisha na kupiga naye stori sana kiasi alinipa hadi namba yake ya simu tukawa tunawasiliana, shukrani kwa Papaa Julie Weston Ilunga Presidaa na Bana Kongolee na Darisalama ambaye alinikutanisha na wadau hawa mara zote wakija nchini.

Chai ametunga nyimbo kadhaa kwenye kila albamu ya BCBG jambo lililomfanya awe ni mtu muhimu kwenye bendi, sidhani kama JB Mpiana halitambui hili ila hakuna jinsi tayari keshaondoka acha maisha mengine yasonge, nitamuomboleza Chai Ngenge daima.

3 Responses to Bado “namlilia” Chai Ngenge

  1. Hadj Le Jbnique says:

    sometimes it’s like serge mignon anaeivuruga bcbg,na sijui ana nini huyu bwana mdogo maana huwezi amini ukiacha jb kuwa mtu wake wa karibu kiasi hiko pia serge ndio mwanamuziki wa bcbg anaelewana zaidi na werrason!kama mtakumbuka kulikua na issue ya mnenguaji sandra nadhani,ambae alikua bcbg then kukatokezea sintofahamu kati yake na uongozi wa bcbg,akasimamishwa kwa utovu wa nidhamu,bi dada hakukubaliana na hiyo punishment akaamua kuomba jina lake liondolewe kabisa bcbg ili akatafute maisha sehemu nyingine,chaguo lake la kwanza likawa kujiunga maison mere ya werra,kila kitu kuhusu mpango huo kikiwa kimekamilika Serge Mignon akawasiliana na werra na kumwambia asimchukue sandra maison mere,werrason alikubali licha ya ushawishi wa bilionea DIDI KINUANI ambae ni mfadhili mkubwa wa maison mere na werra binafsi lakini werra akaamua kumsikiliza Serge Mignon na kufuta mpango wa kumjumuisha sandra ndani ya maison mere.Pia Burkinafaso Mbokaliya nae sababu za kuondoka hii last time bcbg ni baada ya kugombana na Serge na kumchana live ndani ya jiji la johanesburg bcbg walipokwenda kufanya mixing ya ANTI TERRO kwamba hajui kupiga Drums,pia tutu kaludji nae sababu kubwa pamoja na mambo mengine ya kuondoka bcbg ni maelewano madogo na serge mignon,that is the reason wale watoto kina Abraham mignon,sakoko,Nono fuji n.k. wanamuabudu serge mignon kupita kiasi cuz wanajua once you mess up with him it means you mess up with jb and bcbg as well

  2. Hi to every one, it’s in fact a Bado “namlilia” Chai Ngenge | Spoti na Starehe nice for me to pay a visit this website, it includes precious Information. Togel Online Dewi4d http://dewi4d.org/

  3. Nice details, excellent and precious design, as share good stuff with great concepts and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: