Mkongwe Chai Ngenge ajitoa Wenge BCBG

Wimbo Le duo de Paris toka albamu ya Internet ambao ni utunzi wake Chai Ngenge

********************************

Mdudu wa kuondokewa na wanamuziki unaendelea kuitafuna bendi ya Wenge BCBG chini ya uongozi wake JB Mpiana, baada ya kuripotiwa kuondoka mwanamuziki Djino miezi kadhaa iliyopita, habari za uhakika kutoka ndani ya Club ya Wenge BCBG zinasema kuwa mwanamuziki mkongwe Tshai Ngenge naye ameondoka kwenye bendi hiyo.

Zikieleza chanzo cha kuondoka kwenye bendi ni hatua ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na mwanamuziki huyo hata baada ya kukanywa mara kadhaa bila kujirekebisha “…Chai Ngege alikuwa na tabia ya kuchelewa kwenye mazoezi jambo ambalo lililalamikiwa na kiongozi wa safu ya wanamuziki hao Seguen Mignoni (Segee Minyoo)” kilienza chanzo chetu.

Kitendo hicho kilichukuliwa kama dharau na hasa Chai Ngenge alifanya hivyo akisikia JB Mpiana hayupo au atachelewa kufika mazoezini basi na yeye atachelewa au hata akiwahi atabaki ndani ya gari akiongea na simu zake bila ya kujiunga na mazoezi. Tshai Ngenge ni mmoja wa wanamuziki wakongwe na waliojiunga siku nyingi na JB Mpiana hivyo anachukulia uzoefu wake na ukongwe kuwadharau wengine, kiliongeza chanzo hicho.

Ilipofika siku ya siku wakati BCBG wanajiandaa na safari ya kwenda kwenye show Congo Brazaville wakiwa kwenye mazoezi Chai Ngenge alifika akama kawaida akiwa amechelewa jambo lililomuudhi Seguin ambaye ndiye mpiga drum namba moja wa BCBG na kiongozi wa wanamuziki na ndiye anayesimamamia mazoezi, alimuamuru asijiunge na wenzake na baada ya kujibizana na kutupiana maneno kadhaa ya kasha Tshai Ngenge aliamua kususa na kukaa pembeni akimsubiri Big Boss JB Mpiana aje aamue ugomvi, alipofika mazoezini kumbe JB Mpiana alikuwa tayari ameshapewa mkanda mzima na ikumbukwe kuwa Seguin ndiye “mtoto wake” JB Mpiana na msiri wake mkubwa, hata wakiwa kwenye show JB Mpiana chupa yake ya maji ya Kunywa anakaa nayo Seguin hata Baunsa wake haishiki, hivyo inaonyesha ni jinsi gani anamuamini, na kuna kipindi alikuwa akiishi naye nyumbani kwake, hivyo JB Mpiana aliitisha kikao cha Wakurugenzi na ikaamuliwa Chai Ngenge asimamishwe kwenye Band na kutolewa kwenye Ziara zote za BCBG jambo ambalo mwenyewe aliamua pia kuandika barua ya kujitoa na kubaki na hisa zake tuu kwani Wenge ni Kampuni ambayo wanamuziki wanahisa.

Chai ameshiriki kutunga nyimbo nyingi ndani ya Wenge BCBG kama Le duo de Paris (Internet), Identite d’amour (Kipe Ya Yo), Mbua (Soyons Serieux) na nyingine nyingi.

Kwangu bado Chai Ngenge ni jembe ambalo JB Mpiana alikuwa anahitajika kuendelea kuwa nalo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: