Koffi Olomide anunua Rolls Royce Phantom na kuitambilisha kwa watu wake.

Ukiwataja wanamuziki matajiri basi Koffi ni mmoja wao, akiwa anamiliki 5 Star Hotel na akiwa na hisa kwenye kampuni kadhaa ndani ya Congo na nje ya Congo Koffi anaorodheshwa kuwa ni mmoja wa wanamuziki ambao wamefaidika vilivyo na muziki wao.

koffi-olomide-offre-rolls-royce-femme-L-GjQJ2D

Majuzi Koffi aliingiza gari mpya Model ya 2012 aina ya Rolls Royce Phantom na kuitambiulisha kwa mashabiki.

264517_643109372371271_1893476095_n

Pichani Koffi Olomide akiwa mbele ya gari yake. Koffi ametangaza kung’atuka kwenye shughuli ya Muziki baada ya kutoa albamu yake mpya ambayo iko studio kwa sasa, Hii itakuwa ni Albamu ya 20 ya mwanamuziki huyu ambaye anamaliza akiwa na mafanikio na mpaka sasa albamu zake tatu zimeorodheshwa kwenye listi ya albamu 1000 ambazo unapaswa kusikiliza kabla ya kuondoka duniani (kufariki).

4 Responses to Koffi Olomide anunua Rolls Royce Phantom na kuitambilisha kwa watu wake.

 1. papa richard malewa says:

  Hii habari imeniacha nimeganda sekunde kadhaa kama nimepigwa na shoti ya umeme.

  Hili pengo halizibiki. I hope bado atakuwa anatuletea releases hata kama hatakuwa front line.

  sijaelewa vizuri anaachana na muziki na mambo yake yote au nguvu ya ulingoni imekwisha kwa hiyo atakuwa kama mkurugenzi au producer huku mke wake cindy akiongoza mashambulizi?

  ustaafu kwa amani Koffi kazi uliyoifanya siyo ya kitoto. misukukosuko, drama, migongano , malumbano, mapenzi, simulizi za kusisimua kupitia tungo zake tangu enzi nzile za milima ya djalon, hofu uliyojenga kwa watawala, styles za mavazi, vijana uliowaibuia na kuwapika, manguli uliowachomoa toka bendi zingine na kuleta uhasama, stories ulizotengeneza kwenye front pages za magazeti, interviews za kusisimua kwenye matv, drama against wazekwa, jb mpiana, papa wemba, werrason ahhaaaaa koffi umefanya mengi dunia hiii . You are one of LIVING LEGEND ! kwenye sayari yetu.

  Basi tu kama ulivyowahi lalamika na kama tunavyolalamika waafrika laiti kama vyombo vya magharibi na mapromota wake wangekuwa wanatoa nafasi kwetu africa hakika nafasi yako ingekuwa sawa na akina michael jackson, elvis, madonna, na wengineo wengi.

  Tuliona jinsi ulivyoweza ibua akina fally ipupa, soleil wanga wakiwa wachafu kabisa wamepigika kabisa toka mitaa ya kinshasa sasa wamepaa wamekuwa wanamuziki wakubwa ni kazi ya mikono yako KOFFI.

  Ahhhaaa nina mengi lakini muda sina wa kueleza MR QUDRA KORA MAN LE RWAMBOW DE ZAIRE PAPA NA DIDI STONE PAPA FOLOLO

 2. papa richard malewa says:

  hii habari ya koffi kung’atuka inaweza kutengenezewa stori nzuri ya kuonesha utofauti wa koffi kung’atuka toka kwenye muziki akiwa na hali nzuri tu maisha na vitega uchumi lukuki wakati huo huo huku kwetu kuna Gwiji maarufu kabisa Maalim Gurumo amestaafu muziki huku hali yake ikiwa ni dhofu hali na anahitaji msaada mkubwa sana toka kwa wananchi na wadau wa muziki. inasikitisha sana.

 3. YOHANA MTAWA says:

  Koffi pamoja na kuwa kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, kung’atuka kwako kutatunyima sana utamu na uhondo wa kazi zako za muziki sisi wapenzi wako! But all in all, ni katika mipangilio ya kimaisha. May i wish you all the best!

 4. Anonymous says:

  NAMPENDA SANA KOFFI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: