Changamoto kampeni ya FUTA DELETE KABISA

“…Mapicha haya ndio mwanzo wa kuenea kwenye mitandao, hivyo inapaswa kuelimishwa umuhimu wa wao kwani kuwa na mapicha ya matusi kisheria ni kosa la Jinai mbali tu kuwa ni kosa la kimaadili…”

futa delete kabisa

Nimefurahishwa sana na hii Kampeni ya Futa Delete Kabisa ambayo inaongozwa na Tume ya Mawasiliano sio tu kwa sababu ni Bloga bali kama mtanzania wa kawaida ambaye nilikuwa nakerwa sana ama na meseji ama email ama articles kwenye baadhi ya blogs mbalimbali zikisambaza emails za ajabu ajabu au jumbe zenye matusi au maneno yasisyofaa.

Nasema hivyo kwa sababu kwa ulimwengu ulivyo sasa hivi watoto wadogo wamekuwa exposed kwenye ulimwengu wa teknohama tofauti na enzi zetu sisi jambo linalofanya upatikanaji wa habari usitegemee magazeti, TV na Radio tu kama ilivyokuwa zamani.

Nimeipenda na naunga mkono kampeni hi kwa asilimia mia moja (100%) na iendelee Tanzania nzima. pia napendekeza elimu hii iende mbali zaidi kuelekwa na kuingizwa kwenye somo la elimu ya uraia mashuleni ili waototo waanze kuambiwa tangu wakiwa shuleni ubaya wa kueneza ujumbe ambao unamadhara kwa jamii.

Kwa kampeni iliyopo sasa mimi naona pia pamoja na mambo mengine ilenge kuelimisha watumiaji na wamiliki wa Komputa hasa Komputa Mpakato ambao wengi wao ni wanafunzi kuwaelimisha kusafisha Kompyuta zao ikiwa ni kutoa Picha na Video zisizo faa kwenye kompyuta zao.

Binafsi ni mtaalamu wa mifumo ya kompyuta jambo linalofanya vijana wengi waniletee kompyuta mpakato zao (Laptop) ama nizifanyie matengenezo au kuziwekea programu, kiukweli ukiangalia Kompyuta nyingi zina mapicha ya ajabu ndani yake zikiambatana hata na video ambazo ukiuliza mtu atakwambia amepewa ama kuchukua kwa rafiki yake.

Mapicha haya ndio mwanzo wa kuenea kwenye mitandao, hivyo inapaswa kuelimishwa umuhimu wa wao kwani kuwa na mapicha ya matusi kisheria ni kosa la Jinai mbali tu kuwa ni kosa la kimaadili. hivyo ni jukumu letu kama jamii kukumbushana kuhusu maadili kabla ya wasimamizi wa sheria kusimama kuchukua sheria kwani itakuwa unamshurutisha mtu na inawezekana hata baada ya adhabu asibadilike, jambo litakalopelekea yeye kuendelea kufanya na kusambaza picha zile.

Nasema hivi kwa sababu wanafunzi wanatabia ya kuazimana laptop kwa mfumo huu unaweza kuta picha zinasambaa na wengine wanahamishia kwenye simu na kuzisambaza zaidi. Hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha anaeneza elimu hii ya Futa Delete Kabisa kwa wanaomzunguka kutokana na kilichopo mbele yake kwa wakati huo, vinginevyo tutaishia kukuza jamii ambayo haina maadili.

Advertisements

3 Responses to Changamoto kampeni ya FUTA DELETE KABISA

  1. Yureck Elirehema says:

    NIMEENJOY KUSIKIA HILO 2ENDELEE KUELIMISHANA

  2. Anne Pritzel says:

    many wonderful information and inspiration, both of which I want, thanks to offer this kind of a beneficial information here.

  3. Admiring the hard work you put into your site and detailed information you provide. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Fantastic read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: