Afande Allain Mpela alipovamia jukwaa la BCBG

Kwa wafatiliaji wa muziki wa Congo, Mashabiki wa toka Wenge Muzika mpaka Wenge BCBG watakubaliana na mimi kuwa kuondoka kwa Allain Mpella katika kundi la Wenge BCBG ni moja ya pengo ambalo kiukweli si tu lilimuuma sana JB Mpiana bali mashabiki wote kwa ujumla, hata alipoombwa kurejea bado Afande alionyesha ugumu kufanya hivyo.

Kuna wakati alijaribu kuingia kwenye siasa na kujaribu kugombea Ubunge kwenye uchaguzi wa 2011 lakini hakufanikiwa baada ya mpinzani wake kumshinda kwa kura chache. Afande ambaye baaya ya kuondoka kwa Wenge BCBG alijaribu kutoka kivyake kwa kushirikiana na mdogo wake wa damu aliyejulikana kama Geco Bpuro Mpella ambaye alilelewa na kutambulishwa kwenye muziki kupitia kundi la Quartier Latin chini ya kamarade Koffi Charls Olomide ambaye ametangaza kung’atuka muziki karibuni.

Bado binafsi namkumbuka Mpella hasa nikisikiliza Albamu ya Titanic nyimbo kama Process Mambika, Serge Palmi, na nyinginezo ambazo ziliingarisha sana na kwangu mimi ile inabaki kuwa ni moja ya albamu bora kabisa kwa JB Mpiana tangu ajitenge na Werasson.

Pichani juu Afande alipopanda jukwaani kama mwanamuziki mualikwa wakati JB Mpiana alipotumbuiza huko Kinshasa hivi karibuni. Siki ajinsi JB Mwenyewe alivyokuwa akimuita Afandeee na ye kumuitikia Suvereeeee, JB Alitoa machozi baada ya Afande kukabidhi Mic na kushuka jukwaani, hii ni dhahiri kwani takribani mwaka sasa JB amekua akianza na wimbo Omba kwenye show zake ambapo huko mbeleni anawataja wanamuziki wote na kisha huwa anawalilia sana Afande na Caludji ambao wote waliondoka wakatii bado mashabiki wanawahitaji, Caludji kwa sasa ameokoka na kuachana na nyimbo za kidunia.

Shukrani na salamu za kipekee kwako Papaa James Masele Liberko la Loi nakati ya Shinyanga, huyu ni mdogo wake wa damu Mheshimiwa Naibu Waziri Le Suvereign Mukulu wa Bakulu Steven Masere ambaye ni shabiki nambari One wa JB Mpiana, Presidaa na Bana BCBG Club Mu’ Darisalama. Kitoko Makasi, Merci Mingi.

2 Responses to Afande Allain Mpela alipovamia jukwaa la BCBG

  1. papa malewa says:

    jamaa namkubali saaana. sauti ya malaika wa kinshasa.

  2. Ndekwa Mwangata says:

    Binafsi pia Huwa naumia sana napomkumbuka Allan

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: