Buriani Alici Baba, Mfalme wa Muziki wa Congo

Na José Mkapa lkombe

Kwa mashabiki wa muziki wa Congo jina Alicibaba sio geni kwani ama umelisikia kwenye nyimbo likitajwa au kufahamu shughuli zake, akiwa amekulia kwenye ulimwengu wa muziki wa Congo na kupata umaarufu, Alicibaba amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele majuzi jumanne .

Alici Baba ambaye mashabiki wake wakimuita AKenda kenda, Azonga Zonga, Akota kota , Un Prince à N’Djili, Mfalme wa Congo (un Roi au Congo), Mfalme wa Afrika un Roi en Afrique alifariki August 4 mwaka huu ambapo mwili wake ulikuwa umehifadhiwa kwenye Kliniki ya Ngaliema na kuzikwa juzi August 13 katika makaburi ya Mbenseke Futi, mazishi ambayo yalihudhuriwa na mamia kwa maelfu ya wanamuziki. Kwa mujibu wa washiriki wanasema maziko aliyoyapata Alici Baba ni makubwa mnoo ambapo mamia kwa maelfu ya watu walijitokeza kumuaga Mdau mkubwa wa Werasson Ngiama Makanda.

Mazishi ya “Mfalme” huyo wa Congo na Mji mdogo wa N’Djili yalizua taharuki kwani katika mji huo wa N’Djili kila kitu kilisimama pale msafara ulipopita kwenda mazikoni na mamia ya waombolezaji wakiufata kwa nyuma. Alici Baba ambaye jina lake kamili ni Musuapo Nkie-Kunde Alexis Alici Baba ameacha mjane na watoto kumi na mbili

Advertisements

3 Responses to Buriani Alici Baba, Mfalme wa Muziki wa Congo

  1. eric mtawa says:

    rest in peace alice baba

  2. Papa Richard Malewa says:

    Aisee kumbe zile nyimbo za Alici Baba zilikuwa za huyu Gwiji. Sikujua kabisa. Hebu tuwekeeni tafsiri nzima ya Un Alici Baba. Naupenda sana huu wimbo. Ni wimbo uliobeba kibuisa mpipa kiukweli kweli. Daah inanikumbusha mbali kidogo. Kuna sehemu kama Baby Ndombwe na wenzake wanaimba kama Kiswahili Fulani utasikia ……baba na mama….halafu inaingia sauti nafikiri ya JITRO.

  3. We absolutely love your blog and find many of your post’s to be exactly what I’m looking for. Does one offer guest writers to write content in your case? I wouldn’t mind publishing a post or elaborating on most of the subjects you write related to here. Again, awesome web log!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: