Namlilia Madilu

Na Hadj Le Jbnique,Boston,Ma,USA.

Leo ni siku ambayo ulimwengu mzima wa wazungumza lingala na wapenzi wa muziki wa lingala duniani kote hawataisahau,ni siku ambayo walimpoteza kipenzi chao Madilu Multi System.

Jean de Dieu Makiese a.k.a. Madiluu alizaliwa  May 28, 1952 katika jiji la   Léopoldville ambayo ndio Kinshasa ya leo nakufariki dunia  siku kama ya leo yani August 11, 2007.Madilu alianza kuimba rasmi 1969 akipitia bendi mbalimbali mfano Orchestre Symba, Orchestre Bambula ya Papaa Noel bila kuisahau Festival des Maquisards ya mzee Sam Mangwana. Baadae Madilu alianzisha bendi yake mwenyewe ikiitwa  Orchestre Bakuba Mayopi.Lakini kote huko hakuna aliemfahamu madilu duniani mpaka alipoungana na mzee Franco ambapo ndipo mzee Franco akambatiza  jina hili la Madilu System lililokuja kuwa maarufu ulimwengu mzima akijulika hivyo badala ya jina lake la asili yani Jean de Dieu Makiese.Akiwa na mzee Franco na TP OK JAZZ nyimbo ambayo ilimtoa madilu ilikua ni “Mamou” ambayo ilikuja kuwa nyimbo bora kwa mwaka 1984.Lakini hiyo ilikua ni nyimbo ya bendi ambayo madilu alishiriki tu kuiimba na kuifanya sauti yake isikike na kutambulika ulimwenguni na watu kumjua,lakini madilu alikuja kuuthibitishia ulimwengu kwamba anao uwezo na kipaji cha kutunga na kuimba mwaka 1986 alipotunga yeye mwenyewe wimbo unaotamba mpaka leo kwa bendi mbalimbali kuupiga kama copy “Pesa Position” na baadae wimbo “Mario” na kuendelea na nyimbo kibao ukiwemo “La Vie des Hommes” ambao waliufanya kwa pamoja ( duets) yeye na mzee Franco mwenyewe.

Baada ya kifo cha mzee Franco TP OK JAZZ ilisimama kufanya shughuli za muziki kwa mwaka mzima,lakini baadae TP OK JAZZ Ikarudi upya chini ya Madilu ambae alijaribu kuileta TP OK JAZZ pamoja na kutoa mchango mkubwa kuhakikisha inasimama.Baadae Madilu akarejea kuendeleza solo career yake kama yeye huku akiweka makazi yake ulaya zaidi kwenye miji ya Paris na badae Geneva,Switzerland lakini huku nyumbani Kinshasa akiendelea kuwa na kiwango kikubwa cha mashabiki pia.

Mwanzoni mwa mwaka 2007 sikumbuki sawasawa mwezi gani Madilu alirejea Kinshansa mara moja kwa lengo la kufanya shooting kwa ajili ya video za nyimbo zake.Akiwa katika harakati za kukamilisha kilichomrejesha Kinshasa then arudi zake kwake Ulaya siku ya ijumaa ya August the 10th 2007 Madilu alianguka ghafla na kukimbizwa hospitali ya chuo kikuu cha Kinshasa ambapo asubuhi ya siku iliyofuata yani August 11th,2007,Madilu alifariki dunia.

Madilu alikua kipenzi cha watu wengi hasa tabaka la watawawala wa nchi za AFRIKA kiasi cha kupata mialiko mingi ya kutumbuiza kwenye hafla za marais mbalimbali  wa nchi za Afrika ya kati na magharibi.Mfano ni hii hafla iliyofanyika ikulu ya GABON ambayo ili ni  ANNIVERSAIRE ya Mokonzi wa bakonzi le prezidaa OMAR BONGO na mkewe Mamaa EDITHA SASSOU NGUESSO ambae alikua ni binti wa rais wa Congo Brazzaville DENNIS SASAAOU NGUESSO,walikua wakisherehekea miaka kadhaa tangu waoane ambapo mkitazama vizuri mzee DENNIS SASSOU NGUESSO nae mtamuone hapo kwenye big Party ndani ya ikulu ya Gabon,mamaa Editha mtamuona hapo kwenye dancing floor akiwa amevaa gauni refu la kijana huku akicheza muziki wa madilu na mumewe Omar Bongo.Rais OMAR BONGO na Mkewe huyo nao kwa sasa wote ni marehemu.

Mungu awalaze pema wote watatu,Madilu,mzee Omar Bongo na mamaa Editha.

Advertisements

2 Responses to Namlilia Madilu

  1. Papa Richard Malewa says:

    Aisee wewe ni mukali na uandishi wako umetulia kweli kweli

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: