“100% Mutuashi” Mpya ya Tshala Muana kuenzi miaka 35 ya katika muziki.

Katika kusherehekea miaka 35 ya kuimba, mwanamuziki machachari wa DRC Tshala Muana ametoa Albamu mpya itakayo itwa 100% Mutuashi, MAlkia huyo wa Mutuashi alisema.

Katika kuenzi mwanamuziki huyo Waziri wa Vijana, Michezo, Sanaa, Utamaduni na Jinsia, Familia na Watoto ameandaa sherehe kwa heshima ya malkia huyo kwa ajili ya kumpongeza ( Youth, Sports, Arts and Culture and Gender, Family and Children).

Vundula ni moja ya single zinazopatikana kwenye albamu hiyo ambazo zinafanya vizuri na Malkia huyo ameonyesha kuwa bado yumo. Tshala Muana anajulikana kwa vituko vyake awapo jukwaani, kuna kipindi alikuja Tanzania na Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu John Sigwiyemisi Malecela alikuwa mgeni rasmi ukumbi wa Diamond Jubilee alipotumbuiza mwanamama huyu, nusu azue taharuki alipopanda jukwaa kuu la wageni rasmi na kuanza kunengua jambo lililozsha kelele za kushangiliwa na mashabiki waliofurika kwenye show hiyo.

Tshalla muana ndio alimtambulisha Meje 30 kwenye ulimwengu wa Muziki ingawa mwanadada huyo alianza siku nyingi na pia aliwahi kufanya majaribio kwa mwanamuziki Koffi Olomide akiwa na Cindy na Cindy alishinda, ndipo Tshalla muana akampika na sasa Meje 30 anatisha.

Kwa mujibu wa waandaji wa shughuli hiyo Mheshimiwa Waziri Baudouin Banza Mukalay Nsungu ndiye atakuwa mgeni rasmi na imepangwa kufanyika Augosti 31 katika bwawa la kuongelea Grand Hotel Kinshasa.

Kama kawaida Spoti Starehe itakuhabarisha kilichojiri.

2 Responses to “100% Mutuashi” Mpya ya Tshala Muana kuenzi miaka 35 ya katika muziki.

  1. Such a deep answer! I look forward to fresh updates. Just wanted to say fantastic article! I could not stop from commenting. Thank you for putting this up.

  2. Its my great pleasure to visit your blog and also to get pleasure from your terrific posts here. I like it quite a bit. I can come to feel you paid significantly interest for those posts, as all of them make sense and are pretty valuable.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: