Wamtambua nani hapa?

image

30 Responses to Wamtambua nani hapa?

 1. Anonymous says:

  Jb mpiana , blaise bulla, adolf domingez,didie masala,werason ngiama, dream bend never come back

 2. Anonymous says:

  jb mpiana,bula,adolphe,masela,werrason

 3. Anonymous says:

  Hapa kutoka kushoto kwenda kulia ni JB.MPIANA,BLAISE BULA,ALAIN MAKABA,ADOLFE DOMINGUEZ,DIDIER MASELA na WERRASON MAKANDA.hizo comment 2 zilimemruka ALAIN MAKABA ……mpangalaerasmo.

 4. Anonymous says:

  The best Band of all the time

 5. glady says:

  nimefurahi kuona picha kaka nimefurahi umerudi

 6. Giddo says:

  wera,makaba,dominguez,blaize bula ,mwenye koti nyeusi na mwenye shati nyeupe cjawakumbuka

 7. Papa Kasapira says:

  Wenge Musica BCBG 4*4 The Best in The World.

  1)J’B Mpiana “Papa Cheri” Wenge BCBG
  2)Blaise Bula .Wenge
  3)Adoilf Dominguez”Papa One” Wenge Tonyatonya
  4)Werrason Ngiama”Igwe” Wenge Musica Moison Mere (wmmm)

 8. Papa Kasapira says:

  Papa Cheri Sulutani Sovereign Priemere Bin Adam Mukulu, a natural born leader. The king of live music of all time .papa pius special request tupigie “papito mbala live” in zenith mkuu

 9. Juma Hussein Kitine says:

  Mpiana amefulia, muziki wake si kama zamani kwani anachemsha sana siku hizi au amehamua tu kulipua kwenye hizi albam zake za siku za mwisho mwisho.

 10. Anonymous says:

  hivi kwanini afrique vibes imefungiwa? je kuna mmbadala wake tujulishane wadau.

 11. Anonymous says:

  I wish kipindi hicho walichokuwa juu wangefanya kolabo moja na Koffi Olomide nafikiri wangetengeneza kibao cha karne. Lakini ndiyo hivyo tena walikuwa kama paka na chui.

 12. Hadj Le Jbnique says:

  kumbukumbu nzuri

 13. Anonymous says:

  Vipi kule mtaa wa Afrique vibes hakupitiki kuna anayejua sababu yake? je kuna mtaa mwingine unafanana na huo

 14. Anonymous says:

  kwa hiyo hapo yule Atalaku Robe Wunda, Mkaanga Chips Ekokota, Sauti ya Malaika wa Kinshasa Allain Mpela, Ali “Tumba” Mbonda, Pat Kusangila na Tutu Kaludji na wengineo walikuwa hawapo au bado hawajaingia?

  • Anonymous says:

   Hao unaowataja walikuwa waajiriwa tu, Wenge Musica ilikuwa ikimiliwa na wanamuziki hao sita, wengine walikuwa vibarua.

   • Anonymous says:

    Aisee hii ni habari nzuri sana. kumbe hao manguli sita ndiyo walikuwa shareholders wa bendi.

 15. Anonymous says:

  Hivi kwani nini Wenge walikuwa na udhaifu wa kushoot video Albamu zao au hata Live Perfomance kulinganisha na Koffi Olomide. Kazi za Wenge zimeanza kumiminika kuanzia kile kipindi walichotengana na JB Mpiana kuanza na kazi ya Zenith ndipo mvua ya Wenge Werrason na JP Mpiana zikaanza kumiminika. Lakini kabla ilikuwa nadra sana.

 16. Anonymous says:

  Kuna video moja naifatuta nilisimuliwa na Kaka yangu kuwa wakati wa mwanzo mwanzo mwa Utengano kuna siku JB Mpiana alikuwa anafanya onesho halafu wakawa wanaimba nyimbo zilizotungwa na wale wanamuziki wengine ambao walikuwa wametangana nao basi wale wanamuziki walivamia stejini ukaanza mshike mshike na varangati. Kuanzia hapo ikabidi kila mtu awe anapiga nyimbo alizotunga yeye . Hivi hii kweli Haji JBnique au Papa Pius? maana nasikia kuna msemo wa Kizaire unaosema ” Cha Mutu Cha Mutu” na “Cha Zambe Zambe”. Huu msemo anapenda sana Kuimba Ali Choki, Mzee wa Farasi, Mzee wa Tingatinga.

  • Papa Kasapira says:

   Daa hiyo kali but kuna video yao moja ya live concert i think walikua wanapiga live ufaransa wote walikua wamevalia t shirt za timu ya PGS zenye nembo ya OPEL utaona kabisa kuna mgawanyiko katika band Werrason na Adolf walikua hawajishughulishi kwa lolote na Didier Masela alishika bass guitar mara moja tu.baada ya mda nikasikia wamejitoa

   • Anonymous says:

    Jb mpiana yupo KIN na anajitutumua na mpunda style ambayo imeshindwa kabisa kubamba. Wenyewe tulishuhudia jinsi alivyodhalilika Dar mwaka jana alikuja na bendi yake wakaishia kupiga mziki saa tisa za usiku kusubiria wateja wajae. waliingia mashabiki kiduuuchu na Tanzania wala haikutikisika kwamba ameingia mwanamuziki mkubwa kuja kufanya maenesho nchini.

 17. Anonymous says:

  Bravo!!!! yatosha

 18. Papa Kasapira says:

  KIKOSI KAZI AFTER THE SEPARATION OF WENGE MUSICA BCBG 1997 and the born of WENGE BCBG
  JB Mpiana akiwa kiongozi wa bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB mwenyewe, Alain Mpela”Afande”, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula”Engineer”, wapiga guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo & rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina Al Capon(Drums), Ali Mbonda, Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful Atalakus toka kwa Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.(R Kelly) hiki ndicho kikosi kazi kilichobaki baada ya wasaliti didier masela,werrason na adolf dominquez kujitoa na kuanzisha kundi lao wenge musica moison mere which ambapo after their first album FORCE INTERVENTION RAPIDE na wao wakatengana baada ya kutofautiana na dictator werrason

 19. Anonymous says:

  .Hebu tuweke sawa mambo. Waliojitoa walikuwa jb mpiana na wapambe wake. Na ndio maana jina la bendi la bendi la jb mpiana lilibadilika na kuwa wenge bcbg. Na huku werrason akibakia makao makuu ya wenge au Wenge Maison Mere. Werrason hakuwa kiongozi bali huyo jb mpiana aliyekaribishwa wenge akachonga mzinga. Na udikteta wa jb mpiana ulisababisha akina burkina faso ali mbonda japanois alyase demingongo na baadaye bula kuondoka bcbg. Makaba alimjua vyema jb mpiana na wala hakuwahi kuajiriwa na jb mpiana. Na baada ya utengano ndiyo ulikuwa mwisho wa jb mpiana maana vikopo vyake vilikuwa vinanyooshwa na Werrason na akina Bula. Baada ya utengano Werrason kashinda awards kadhaa ikiwamo za Kora na golden disks kadhaa kitu ambacho jb mpiana hajawahi. Werrason ndiyo habari ya mjini mpaka kwa watoto wa hip hops wa leo. Watu wanachezesha mabega na mikono kifuani na style ya malewa mpaka kwenye taarabu. Jb mpiana alisikika mara ya mwisho mwaka 97 na albam ya ndombolo aliyotengenezewa na akina bula na makaba. Kwa nini aliona wivu kumkatalia Werrason asitoe solo album? Maana alianza makaba na pile au face akaja jb na ndombolo na werrason ilikuwa aje na Kibusa Mpipa lakini moto wake mliuona.

 20. Anonymous says:

  Ubinafsi wa JB mpiana ndo ulioleta majanga Wenge, Werrason angekuwa mbinafsi asingekubali kumuachia JB mpiana uongozi, kwani wasisi halisi aw Wenge ni Werrason na Masela.

 21. mpaka sasa jb mpiana yuko wapi na anafanya nini?

 22. Anonymous says:

  Jb mpiana yupo KIN na anajitutumua na mpunda style ambayo imeshindwa kabisa kubamba. Wenyewe tulishuhudia jinsi alivyodhalilika Dar mwaka jana alikuja na bendi yake wakaishia kupiga mziki saa tisa za usiku kusubiria wateja wajae. waliingia mashabiki kiduuuchu na Tanzania wala haikutikisika kwamba ameingia mwanamuziki mkubwa kuja kufanya maenesho nchini.

  • Papa Kasapira says:

   kiongozi you might be right kwamba style ya mpunda haijafanya vizuri but kwenye swala la kukosa mashabiki kipindi yupo dar hapo ntakubishia,ukweli ni kwamba that day kuna hujuma zilifanyika wote tunajua siku ile mashujaa ndio walikua wanakuja kivingine under chaz baba na kulikua na ushindani kati ya twanga na mashujaa umeme ulikatika na to my suprise jenereta halikuweza kuwaga consipiracy theory ni kwamba twanga walihujumu lile show na kujibu hoja yako ndio maana baada ya jenerata kukataa kuwaka sisi wa jb tuligoma kuondoka mpaka our royal model apige atleast mziki mmoja ndi walipofanikiwa kurudisha umeme show ya jb ikaaza offcourse by that time watu wengi walikua wameshaondoka maana walijua show yote ya uzinduzi haitafanyika tena

 23. Anonymous says:

  Baada ya Wenge kusambaratika JB Mpiana aliamini kuwa yeye ndo angebeba legacy ya Wenge, akaanza kujipima ubavu na Koffi, akawafanyia fitna kina Makaba na Bula wakajitenga, alijaribu kidogo kwenye TH, lakini baada ya hapo akaanza kutoa albam za hovyo kama internet na Ant-Terro. Ghafla upinzani ukaamia kati ya Werra na Koffi, Kama unavyojua Koffi ni bingwa wa kuiga muziki wa wapinzani walio juu, siku za nyuma alitafuta Repa mwenye sauti kama Ekokota akiitwa Bivens, alitamba sana kwenye Magie, Baada ya kugundua Werrason yuko juu, akamuiga kwa kusajili marepa wenye sauti kama za Marepa wa Werra, Kerozene na Brigade kupambana na Bill na Celeo. Akaiga mpaka style ya uchezaji wa show ya Werra Zenith.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: