Demi Tour yakwake Werasson Ngiama Makanda

 

Anaitwa LE ROI DE LA FORRET” NOEL NGIAMA WA MAKANDA a.k.a.WERRASON hii ilikuwa kipindi chake cha mwanzo cha kujitawala alipotoka na album yake ya Kibuisa Mpipa kama sijakosea maana hii ilikuwa ni Bonus Truck. Wakati huo bado akiwa na wataalamu wake kama akina Ferre na bado hajakimbiwa na wanamuziki wengi ambao kwa sasa wanatamba sana.

Wimbo huu aliuimba kwa mahadhi ya Congo Rhumba, mdau wanguHadj le Jbnique (Mnazi mkubwa sana wa JB Mpiana)  ye alinikumbusha mbali sana kuwa album hii ilipikwa na mtaalamu wa Congo Rhumba ajulikanaye kama L.NZIMBI ikumbukwe kuwa huyu ndiye mpishi wa albamu ambayo mpaka leo inauza ya FEUX DE L’AMOUR” yakwake Jemedari SOUVERAIN LEADEUR YA BA WENGEE JB Mpiana ambayo aliitoa kama solo enzi kundi la Wenge Musica BCBG halijaparanganyika.

Huu ni moja ya nyimbo ambazo mimi binafsi Werasson amenifurahisha na kama ningepata nafasi ya kukutana naye na kumshauri ningemshauri a stick kwenye nyimbo hizi za taratibu kama unataka kuamini tafuta kitu inaitwa Blandine, Kiukweli hakuna mtu wa muziki anaweza kukisikiliza kitu BLANDINE asifurahi,pale kazi ilifanywa na ikafanyika,vichwa vyenyewe wmmm wakati huo vilikuwa vinatisha,maanake ulikuwa ni mkusanyiko wa vocals za FERRE GOLA,pia kulikua na JDT,alikuwapo ADJANI,AIMELIA LIAS “DEMINGONGO”,BEBEE NDOMBE na SERGE MABIALA.Pia nakiri mzee mzima LE ROI DE LA FORRET WERRASON alifanya vizuri sana katika album nzima kiujumla lazima tuwe fair katika hilo na kufanya vizuri huko mimi binafsi nashawishika kuamini kwamba kulitokana na kwamba alitulia kwa muda kuitayarisha ndio maaana ikatoka na ubora ule,sio siku hizi kila kukicha album mpya.

 

Wakati huo wa Kibuisa Mpipa, huu ni wimbo ambao huku kwetu hauku heat lakini ni moja ya nyimbo ambazo nazipenda sana kwa Wesasson, Pia kuna vitu kama Koffi Ayiana ambacho niliwahi kukiandikia pia siku za nyuma. Kwa ufupi angalia nyimbo zinazombeba zaidi Werasson ni nyimbo hizi za taratibu zenye mahadhi ya Congo Rhumba ambayo Mkongwe JB Mpiana ni champion kwenye hizo najua ma werasonique mtabisha kwa hili lakini ni wazi na halipingiki.

Truck hii hii ni maalum kwa Werasonique wooote Sadiq Tiger, Papaa Maendeka, Boss Chizenga, Moto Mkubwa Halid Mmanzi, Mdau wangu Steven na wapenzi wote wa Blog hii, Mukubwa Hadji Heshima kwako kiongozi na mnazi wa Wenge

3 Responses to Demi Tour yakwake Werasson Ngiama Makanda

 1. Hadj Le Jbnique says:

  tuko pamoko makamanda wangu,nashiriki sana lakini kwa njia ya kusoma tu,sina muda wa kutulia na kuandika nimebanwa kidogo,lakini mambo yakitulia ntarudi kwa kishindo na nguvu mpya.

 2. It came delivered with Medium Gauge Phosphor-Bronze wound strings.
  Apart from employing an effective guitar humidifier,
  I strongly urge the guitar remain in its’ case you
  should definitely in use. DR Extra Life Acoustic Guitar Strings can be purchased at most music stores or even online outlets including Musician’s Friend for a typical tariff of around
  $25. Secondly the neck can be used by people to tape the notes on the string.

 3. Pasiasi manembe says:

  Nashukru saana kunipasha habari za mwanamziki huyu mahiri na mkongwe Werrason! Na kwa nin watu humwita werrason? Hyo a.k.a inamaana gan? Namkumbuka sana na show yake ya live a Matadi. Endelea kunipa habari za hyu nguli wa mziki wa kongo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: