Happy Anniversary Mdau Mary na Ijumaa Karim

Ijumaa imefika tena napenda kuchukua nafasi hii kumpa salamu za pongezi mdau wangu Mary Ngobei Meldrum wa huko Canada ambaye leo anafikisha miaka 11 ya ndoa yake takatifu ambayo alifunga takribani miaka 11 iliyopita.

Marry ni mwenzetu na mdau mkubwa wa Blogu hii mi binafsi nakupa kibao Feux De L’Amour toka kwa JB Mpiana akimaanisha mioto ya Mapenzi.

Kwa wasiojua lugha iliyotumika humu JB Mpiana alikuwa akiongelea mapenzi ya sasa akiwalalamikia akinadada akisema kuwa yapo wapi mapenzi ya ukweli ya enzi za mababu zetu ambapo watu walikuwa wakipendana kiukweli tofauti na siku hizi ambapo akinadada wamekuwa wakichagua wanaume kila mtu anataka mwanaume aliyesoma, mwanaume alina kazi nzuri, mwenye pesa, inakuwaje kwa wale ambao hawajasoma? Inakuwaje kwa wale ambao hawana kazi nzuri na hawana pesa?

kiujumla ameongelea mtaguso wa mapenzi wa sasa ambapo nadharia nzima ya mapenzi ni unanini? wewe ni nani? na dhana hii ndio inayojenga mapenzi kwenye ulimwengu wa sasa.

Hii si tafsiri sahihi ni majumuisho ili kukupa nini hasa kimeongelewa kwenye wimbo huu.

Respect kwa wasomaji wangu wote, Mamaa Sophia Kessy, Pendejee Maghambo Philipo popote ulipo tuko pamoja, Julie ellyston Suvereign, Batty My Brother pamoja, Mukubwa Edgar Kiiza muzee ya Malaysia, Ally Tandika diwani muzee ya Azam, Mukubwa Six Mzee wa Matombo, Tom Baba Maya aka Chiluba, Mukubwa Gerald Kitima Baba Kara, Dulla Asumani muzee ya Tigo, Werasonique wooote. Pamoja sana.

Nakutakia Weekend njema.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: