Wakijua Kisa cha Alain Mpela kuondoka BCBG ?

image

Binafsi namkumbuka Allain Mpella kupitia verse zake kwenye albamu matata ya Titanic ambapo ameimba sana humo, bwana huyu mbali tu ya kuwa kiongozi wa Bendi baada ya kumeguka kwa Werasson na vijana wake, na JB Mpiana alikuwa akimuamini sana Mpela.

Wengi wa mashabiki hawakujua chanzo halizi cha Allain Mpela kuondoka BCBG akaenda solo na majuzi alijaribu kugombea ubunge huko Congo lakini hakufanikiwa na sasa karejea kwenye muziki tena, Leo tutaangalia kwa makini nini chanzo cha Allain Mpela kuondoka Wenge BCBG.

Wenge walikuwa kwenye maandalizi ya kurekodi albamu yao ya Anti Tero, Wakati huo JB alikuwa anaota ndoto kuwa yeye ndio mpinzani wa Koffi, Mopao alipotoa Monde Arabe (Dunia ya Waarabu) JB akaamua kuja na Anti terorism kutokana na vuguvugu la ugaidi lililougubika ulimwengu wa kiarabu. Anti Tero ambayo ilianza matarisho na tunzi zake hata kundi halijapanguka, mipango iliyoendelea baadaye tena, awali Jb alipanga album hiyo iwe na nyimbo nyingi za Alain Mpela ambae alikua ni kiongozi wa bendi (Chef De Orchestre) pamoja na nyimbo za bendi ya vijana wadogo ya BCBG inayofahamika kama PPU (Presidential Protection Unit) ambayo Alain mpela aliipromote sana na mbili tatu za Jb Mpiana mwenyewe huku member wengine wakitakiwa kuweka tu vocals zao kwenye nyimbo za album hiyo bila wao kuwa na nyimbo hata moja,Alain Mpela alipewa chance ya kuweka nyimbo zake sita (6).

Lakini wakiwa kwenye maandalizi ya album hiyo huku wakisikilizia suala la visa na kuumizwa kichwa ni wapi watakwenda kuirekodi ama kuifanyia mixing album hiyo kama visa itaendelea kusumbua kukatokea sintofahamu kati ya Jb na Alain Mpela, rafiki yake mtiifu ambae alimchukulia kama mdogo wake (ikumbukwe Alain Mpela na mdogo wake Bouro Mpela kuna wakati walikua wanaishi nyumbani kwa Jb kama Herritier watanabe alivyowahi kuishi nyumbani kwa Werrason baada ya Jb kumwambia akasome kwanza shule apate degree ndio arudi BCBG).

Kilichosababisha sintofahamu hiyo ya Jb na Afande Mpela ni simu ambayo ilipigwa na Koffi kwa lengo la kumshawishi Alain Mpela ajiunge na Quartier Latin yake na badala yake simu hiyo ikapokelewa na Jb huku koffi akidhani ni Alain mwenyewe ndie aliepokea simu hiyo hivyo kuendeleza mazungumzo yao yalipokuwa yameishia.

Baada ya simu hiyo Jb alikasirika sana na kumuona Alain Mpela kama bonge la msaliti kwa kuwa licha ya ukaribu wao na yeye kumchukulia kama mdogo wake aki share nae mambo mengi hakuwahi kumtonya chochote juu ya mazungumzo yake na Koffi ambae alikua adui mkubwa wa Jb wakati huo, na Jb ana kitu kimoja mpaka leo, hakuna kitu asichokipenda kama usaliti. Hivyo basi kuanzia siku hiyo Jb na Mpela hawakua brothers tena, inasemekana kuwa mpango huo uliratibiwa kwa karibu na Didie Kinuani ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Koffi na Adui wa JB Mpiana.

Huu ulikuwa mwisho wa ule mpango wa kumpa nafasi Mpela aweke nyimbo zake 6 kwenye ANTI-TERRO Jb akaufutilia mbali na badala yake akamuachia nafasi ya kuweka nyimbo zisizozidi tatu huku kukiwa na mipango ya kumvua u chef d’orchestre.

Kuona hivyo Alain Mpela akasusia kushiriki shows na mazoezi ya BCBG kwa wiki mbili na hatimae akatangaza kujiondoa kundini huku akitoka na single maalum kwa ajili ya kumuimbia na kumsifia adui namba moja wa Jb bilionea Didi Kinuani. Mpaka hapo Jb na kundi wakawa na kazi ya kuziaondoa nyimbo za Mpela ambazo walikua tayari wameshazifanyia sana mazoezi na walikua wakizipiga kwenye shows zao za kila weekend ndani ya Kinshasa na kuanza upya kuandaa nyimbo nyingine na kujipanga upya huku wakiwa hawana mfadhili wala mdhamini kama ilivyo sasa kwa makampuni ya bia ya Congo kutoa sponsorship,wakati huo walikua wakiwategemea matajiri wakubwa wapenzi wa muziki kama huyo Didi Kinuani ambae Jb alikua tayari ameshagombana nae baada ya Dikin kumuiba mke wa Jb mamaa Amida Shatur na kumfanya mkewe.

Alain Mpela “afande” alipoondoka kundini BCBG nafasi yake kama Chef D’Orchestre kwenye bendi ilizibwa na Tutu Caludji ambae awali alikua mkuu wa mambo ya nidhamu kundini ambapo nafasi hiyo na yeye alimuachia mpiga drums Seguin Mignon ambae De La Patria JB amekua akimpenda na kumsikiliza sana akimchukulia kama mdogo wake pia,vilevile Seguin ni mtu wa karibu sana na De La Forret WERRASON na ndio amekua kiungo kati ya JB na WERRA. Hali hiyo ya kuwa na ukaribu na JB ikamfanya Seguin awe na sauti kubwa kiasi cha kwamba ukigombana nae au kama hakutaki lazima uondoke BCBG.

Kiukweli Alain Mpela aliondoka Wenge BCBG akiwa bado na mapenzi makubwa, kwani kwenye moja ya show za Wenge BCBG Mpela alihudhuria na kila ilipofika verse yake alionyesha kukosa raha na wati fulani alitoa machozi na kuripotiwa na vyombo vya habari mapenzi yake kwa BCBG yangalipo.

Leo hii JB Mpiana na Koffi ni marafiki na hii ni baada ya uhasama kuhamia kwa Werasson. hizo ndizo fitna za muziki kama mpira tuu, Merci mingi wadau tukutane wakati mwingine nikuache uwe na wiki njema.

Nakuacha na Kibao Process Mambika utunzi wake Alain Mpela toka albamu ya Titanic ambayo kwangu ni moja kati ya Albamu bora kabisa kupigwa na JB Mpiana tangu waparanganyike na Werasson.

 

Advertisements

6 Responses to Wakijua Kisa cha Alain Mpela kuondoka BCBG ?

 1. Glady says:

  Pls kaka nakuomba utuwekee picha za wasanii waliounga wenge bcbg na waliwai kuweka sauti kwenye nyimbo zao. Pia utuweke kibao danico.

 2. Farid 4x4 says:

  bango bango balobakaa motu akokende
  bango bango balobakaa Afande akei

 3. Prince de La Ville. says:

  Sio fans wa BCBG lakini huyu jamaa nampenda pia namkubali kwani hata mm sikupenda alipoondoka kwa JB MPIANA kuna wakati nilikuwa naiga hata style yake anavyonyoa,yote ilikuwa kujifananisha nae ingawa mm si mwanamuziki ila shabiki wake tu.

 4. Anonymous says:

  Surely Alain mpela has a unique style of singing and to me i believe Alain’s styles can only go very well where there is JB,AIMELIA AND BLAISE BULA, I just miss these guys and this album has the best vocals

 5. Leena Kolar says:

  plenty of wonderful info and inspiration, both of which I need to have, due to present this kind of a beneficial data here.

 6. Hi there! This is my first visit to your blog! We are a team of volunteers and starting a new initiative in a community in the same niche. Your blog provided us valuable information to work on. You have done a marvellous job!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: