Ave Maria na Kesi ya jino la Blaise Bula

Waswahili wanasema mapenzi ni safari ndefu kwenye Wimbo huu ambao uliimbwa na  Wenge Musica BCBG enzi hizo kundi limetimia wakiwamo JB Mpiana, Werason Ngiama Makanda, Blaise Bula, Adolf Dominguez, Alain Makaba na wengineo kila mtu alimtaja mpenzi wake lakini cha kuchekesha mpaka leo hakuna hata mmoja ambaye anaye mpenzi aliyemtaja kwenye wimbo huu, huku JB Mpiana akimuoa HAmida Shatur na Werasson akimuoa Sylvia Mampaka

Katika wimbo huu utasikia kuna mtu anatajwa mwanzo anaitwa Minica Kalala (Monie Kalala), huyu alikuwa binti mrembo na ndiye alikuwa mpenzi wake Blaise Bula kipindi hicho, na mapenzi ya Bula na Monie yalikuwa makubwa kiasi Minie alikuwa akihudhuria kila onyesho la Wenge wakati huo Congo DRC ikiitwa Zaire chini ya utawala wa Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga ambapo mwanaye aliyekuwa akijulikana almaarufu kama Sadamu Hussein akiwa anabeba vichwa vya habari na kuimbwa (Mabanga) na karibu kila bendi ya Zaire wakatihuo, kama ilivyo kwa Ridhiwani kwa sasa (Ingawa haimbwi sana)

Wenge Musica BCBG ndiyo ilikuwa mapenzi makubwa ya vijana wote huku wakiwa hawana mpinzani na kwa wakati huo wengine waliokuwa wakipiga muziki na kuwabamba vijana walikuwa ni Zaiko Langalanga ambao kwa kiasi kikubwa ujio wa Wenge Musica uliwanyang’anya mashabiki lukuki akiwemo First Son Sadamu Hussein.

Hapa nataka kumuongelea Monie Kalala ambaye anatajwa kwenye huu  wimbo wa Ave Marie mwanzo kabisa, huyu binti kwa urembo wake alimvutia Fist Son Sadamu Hussein mtoto wa kigogo, mtoto wa Mobutu ambaye alikuwa mtukutu na mwenye vituko vingi na mpenda starehe ambaye aliitumia nafasi ya baba yake kujitajirisha na kufanya lolote. Ukimuangalia Blaise Bula jino lake limekatika kidogo kwenye mwanya wake inasemwa kuwa ni baada ya kupata kipigo kutoka kwa watu wa Special Force ambao waliamuliwa na Sadamu Hussein baada ya purukushani za kumgombea Monie Kalala.

5 Responses to Ave Maria na Kesi ya jino la Blaise Bula

 1. Glady says:

  Umenifurahisha kaka me nilijua blaise alizaliwa hivyo, asante kwa kutujulisha hilo.

 2. Farid 4x4 says:

  soki nasaki mabee nalingaki yoo,
  nasengi olingisi bolingo nangaa

 3. Anonymous says:

  broo umetisha unatisha nautaendelea kutisha

 4. Prince de La Ville. says:

  Binafsi sina la kusema zaidi ya kkushukuru kaka PIUS kwa kazi unayoifanya ya kutuletea habari za muziki huu kutoka sehemu mbali mbali kwani kupitia SITE hii umenifanya niyajue mengi na kuwatambua baadhi ya wanamuziki ambao nilikuwa siwajui N.K,binafsi nyumbani nina CD na DVD za wanamuziki wa Congo kama Werrason,JB Mpiana,Koffi Olomide,Fally Ipupa,Ferre Gola,Felix Wazekwa N.K,hiyo yote 7bu kuupenda muziki huu wa bolingo kuliko muziki wowote ndani ya TZ mpk CONGO,nakutakia kazi njema bro na uendelee kutupa Vitu kadri uwezavyo kwani tunakubali ufanisi wako,ni hayo 2 kwa leo,by. George a.k.a Papaa na Prince G,mercii mingi Papaa Pius Bamala.

 5. Anonymous says:

  upo juu mzee napata mambo munene mno bg up

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: