Gil Kibens, Profesa wa ukweli “atakayefia” Wenge BCBG.

Gil Kibensi ni Profesa wa ukweli ambaye anafundisha chuo cha Sanaa cha Academi De Beaux Art akiwafundisha wanafunzi, inasemwa kuwa jirani na chuo hicho ndipo waliposoma akina JB Mpiana na Kibensi ni mmoja wa watu ambao waliipenda sana hiyo bendi kabla hajajiunga nayo, ambapo akina JB walisoma chuo kilichoitwa I.S.E

Kibensi ni mmoja wa marafiki wa karibu sana wa JB Mpiana na ndiye alikuwa naye na kumshauri sana JB alipoachwa na mkewe Amida Shatur jambo ambalo linasemwa lilimchanganya sana JB Mpiana. Kibensi na Seguin Mignon wanasemwa kuogopwa sana kwani ukigombana nao maisha yako BCBG tayakuwa hatarini kwa kweli. Kibensi si tu muimbaji bali pia ni music arranger anwasaidia sana kutengeneza nyimbo na ndiye aliyetengeneza kwa kiasi kikubwa na kuiwezesha albamu ya Anti Tero kutoka baada kukumbwa na sintofahamu kibao.

Ikumbukwe kuwa Jules Kibens, Rio, Chai Ngenge na Gentamacine ambaye ni atalaku namba moja kwa sasa. wakati hawa wote wakiwa recruited JB Mpiana alikorofishana na Makaba kutokana na makaba kusema kuwa hawa wote hawakuwa na uwezo jambo ambalo JB alilipinga na kusema kuwa wanaweza, hii ilikuwa wakati wako Paris kwa ajili ya Show ya Zenith.

Mgogoro huo ulidumu mpaka siku ya show yenyewe ndani ya zenith  dakika chache kabla ya kupanda stejini kuanza show kulitokea majibizano ya maneno baina ya marafiki hao yaliyopelekea mpaka JB Mpiana kulia machozi baada ya Alain Makaba kutumia maneno makali sana yaliyofanana na matusi dhidi yake, JB aliumia sana moyoni kwani kazi ya ku recruit aliifanya Blaize Bula, Jb akasusa kupanda jukwaani hali iliyopelekea showa rasmi ichelewe kuanza huku kina Alain mpela na Aimelia wakiwa wanaendelea kuimba nyimbo za utangulizi stejini, ikabidi mkewe Jb, mama Amida Shatur pamoja na rafiki yake JB waliekuwa pamoja maisha ya utotoni JDL ambae wakati huo alikua ni mpiga keyboard wa Wenge El Paris waingilie kati kumsihi JB apande stejini kwani wapenzi hawatawaelewa kabisa hasa ikizingatiwa Blaize Bula nae hayupo kutokana na kuumwa. (JDL kwa sasa yuko na bcbg kama muimbaji). Show ilifanyika na hakuna aliyejua kuwa kuna kitu kimetokea, baada ya kurejea jamaa walikuwa recrited na kuungana na Wenzao kwenye bendi mpaka leo.

Alipohojiwa wakati fulani wenge walipokuja nchini alisema kuwa anafikiri maosha yake ya muziki atayamalizia Wenge BCBG kwani ni bendi ambayo anaipenda na iliyomtambulisa kwenye ulimwengu wa Muziki. Mbali na uimbaji Kibensi ni mtunzi pia msikilize hapo kwenye Love Air wimbo ambao ulikuwa kwenye Albamu ya Internet ambayo binafsi naipenda sana kwa yeyote aliyenayo atakubaliana na mimi Bass Gitaa lililopigwa humu ni hatariiiii. Shukrani za kipekee kwa Papaa Julie Weston Illunga, Presidaa Bana Congolee na Darisalama, Mamaa Glady nakati ya Moshi pole kwa kila kitu mamito, tuko pamoja, La Grand Paa Mussa toka Pride Fm Mtwara na Mamaa Husna La Renee De Africa pamojaa mnooo watu wangu. Nakukumbusha mtu wangu wa nguvu hapo kulia kuna sehemu unaweza sikiliza live Pride Fm, bofya tuu kusikiliza.

One Response to Gil Kibens, Profesa wa ukweli “atakayefia” Wenge BCBG.

  1. Salim says:

    Bcbg the machine of music…… Moto
    Chini. Asante Papaa Pius

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: