Balia Ngando ilimrejesha Blaise Bula uwanjani

Ni mmoja wa wnamuziki ambao kuondoka kwao Wenge BCBG kulinisikitisha sana, ni kutokana na kipaji kikubwa alichokuwa nacho, lakini kuna wakati inafika maishani huna budi kufungua milango mingine, Baada ya mpasuko mkubwa Bula aliondoka kwa JB Mpiana hatimaye sambamba na Allain Mpella, na Aimelia Lyase ambao kila mmoja alienda kuanza kivyake.

Alipewa jina la Engineer Blaise Bulla kwanza ni kwa kipaji chake cha kurekebisha mitambo ya sauti pale kundi likiwa linafunga vyombo kabla ya show kuanza na pili ni kupanga sauti na vyombo, kwa kiasi kikubwa Bula ndiye aliyekuwa akipanga nani aanze, chombo gani kiingie wakati gani, na anasemekana ndiye aliye compose mpangilio wa vyombo kwenye Kalay Boeng.

Huyu bwana ni mmoja ya wanamuziki wachache wa Wenge Familia ambaye akikaza anaweza kuendelea vyema. Swahiba wangu Jema Mandari ye anasema huyu bwana si mchezo ana anakikubali sana kibao hiki, ukisikia utaona unapata taste ya Wenge Musica humu ndani, kwa Solo, Rhythim Gitaa lilivyopigwa na jinsi jamaa walivyopokezana, ukisikiza wimbo huu utaona Bula mwenyewe hajasikika sana, Wimbo ukiwa umeongozwa na Solo na atalaku.

Kwa kifupi nasema bado Bula anakubalika na bado anaweza akafanya mashabiki wakamkubali hana kwa production hii ameonyesha yuko ngangari kinoma. Hii ni baada ya kutoka na ile albamu yake ya iliyokuwa na vibao kama Pondulation ambacho kwa kiasi kikubwa kilibamba.

Pia angalia hii ni Live ya kibao ambacho binafsi nakipenda sana cha Eve Sukari ambacho kilikuwa ni utunzi wake Blaise Bula pia akiwa bado na Wenge Musica BCBG enzi hizo ambapo si mimi wala shabiki yeyote ambaye angekubali hawa jamaa waparanganyike.

Advertisements

2 Responses to Balia Ngando ilimrejesha Blaise Bula uwanjani

  1. Glady says:

    Kaka mambo! Ni kweli kama ingetokea nikaulizwa nini nataka kifanyike kwenye musik wa kongo ningesema wenge musica bon chic bon gere irudi tena nililipenda hilo kundi sana, na kwa upande wa blause bula ndie nilikuwa na mkubali kuliko wengine wote, alitisha asa nikikumbuka vibao kama, likala moto, filandu na vingine kibao. Hongera sana kwa kutujuza.

  2. piusmickys says:

    Thanks Gladys, Bula alikuwa na kipaji kikubwa na alikuwa hana makuu, Nitakuletea Story kwa nini Bula aliondoka kwa JB Mpiana.

    Plz tuwasiliane kwenye simu mambo yakikaa sawa, nakuja Moshi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: