Mashabiki wa Tanzania wabezwa kukaa vitini kwenye show za muziki

[image]

Pichani juu na chini ni mashabiki wakifuatilia show ya Koffi Olomide aliyetumbuiza katika viwanja vya Leaders.

[image]

Picha za Mashabiki wa Tanzania wakifuatilia Show ya mwanamuziki Koffi Olomide ambazo kwa nyakati tofauti zimeleta mijadala kwenye ulimwengu wa muziki wa Congo huku wachangiaji na mashabiki wakitubeza watanzania kuwa hatujui starehe.

Wakiongea mashabiki hao wamesema kuwa ni jambo la kushangaza mwanamuziki kama Koffi au JB Mpiana anapiga kwenye show tena ya wazi kunapangwa vitu akina dada wanakuja na poda zao mpaka wanaondoka wanazo usoni. “…angalia show za JB, Wera au Koffi huko Matadi, Kinshasa na hata za Ufaransa kama utaona viti vimepangwa hivyo kama watu wako Concert ya dini, hii ni Tanzania tuu …” alisema Julie Weston Ilunga, Mzaire anayeishi na kufanya shughuli zake za kibiashara hapa Dar Esalaam, naye Sisco Kapinga aliunga mkono na kusema haelewi kabisa ama mashabiki hawajui kucheza au hawauelewi muziki.

“…Kuna haja ya waaandaaji kuwahamasisha mashabiki na kuwaandaa kisaikolojia ni nini wanaenda kukiona pale” alisema Sisco.

Hali hiyo haikuishia hapo hata kwenye mtandao maarufu wa Vibe Afrika jambo hili lilizungumziwa huku wengi wakionyesha kushangaa sana na utaratibu huu.

2 Responses to Mashabiki wa Tanzania wabezwa kukaa vitini kwenye show za muziki

  1. Prince dela Ville says:

    Hatakama hatujui wanachoimba na midundo hatusikii?Tubadilike ndg zangu tunawavunja moyo pili tunaonekana tumekuja kuja kushangaa na sio kuburudika,Hayo yangu kwa leo,MerHatakama hatujui wanachoimba na midundo hatusikii?Tubadilike ndg zangu tunawavunja moyo pili tunaonekana tumekuja kuja kushangaa na sio kuburudika,Hayo yangu kwa leo,MerHatakama hatujui wanachoimba na midundo hatusikii?Tubadilike ndg zangu tunawavunja moyo pili tunaonekana tumekuja kuja kushangaa na sio kuburudika,Hayo yangu kwa leo,MerHatakama hatujui wanachoimba na midundo hatusikii?Tubadilike ndg zangu tunawavunja moyo pili tunaonekana tumekuja kuja kushangaa na sio kuburudika,Hayo yangu kwa leo,Mercii

  2. Glady says:

    Mimi ningesema watu hawaujui muziki wa kongo, jamani wausikilize muziki wa kongo vizuri wasikilize jinsi vyombo vinapigwa, wasikilize sauti jamani hawa watu wanasauti za ajabu mimi sina hata miaka 30 lkn ni mwanawenge musika wa damu. Watu wanauchukulia nikama ni muziki wa enzi hizo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: