Djino athibitisha kuondoka rasmi Wenge BCBG

February 5, 2013

Lile sakata la mwanamuziki Djino wa Wenge BCBG hatimaye amethibitisha kuondoka katika kundi la Wenge BCBG.

akinukuliwa na Gazeti la  Journal Visa Mwanamuziki huyo amesema kuwa ameamua kuondoka Wenge BCBG kwa sababu hajui hatimaye yake baada ya kusimamishwa katika kundi hilo. Hata hivyo Djino amesema kuwa bado ataendelea kumheshimu Papaa Mpiana kwa kuwa bila yeye ulimwengu usingemjua, “…ndio baba wa muziki wangu, yeye ndio amenitoa na kunitambulisha kwa dunia namuheshimu na siwezi kubadilishana maneno na yeye ni utovu wa nidhamu…”.

Hata hivyo mwanamuziki huyo amesema kuwa chanzo cha yeye kufarakana na boss wake ni mwanamuziki mwenzie Sunda Bass ambaye anatumia ukaribu wake na JB Mpiana kuwaumiza wengine, hivyo amemuomba boss wake huyo wa zamani kutengeneza utaratibu wa kuwasikiliza wanamuziki wengine kabla ya kutoa maamuzi.

Advertisements

Balle de Match kutambulisha mpya ya JB Mpiana na Wenge BCBG

February 3, 2013

clip_image001

Sikiliza balaa la Genta Lisimo humu!!

Mwanamuziki JB Mpiana ambaye alifunga mwaka kama wenzie kwa kuzindua Single yake mpya ijulikanayo kama Balle de Match ambayo aliizindua huko Equatorial Guinea

Hii ilikuwa ni baada ya show ndefu ambazo alizifanya hapa nchini na huko Zambia ambako aliangusha show ya nguvu. Inasemekana kuwa hii ndio itafungulia ujio wa albamu yao mpya ambayo wanamuziki wengine nao wametunga nyimbo kadhaa ndani yake kama Zoule Atshuda alias na Diego Milito. Wimbo Balle de Match ni moto wa kuotea mbali kwani Genta Lisimo amefanya kufuru humo na kwa mara ya kwanza JB ameamua kutumia electric drums kit kwenye Sebene.

Ukisikia Solo lililopigwa humu ni lile Solo kali la Metre Ficare Mwamba akishirikiana na kijana mdogo anayekuja kwa kasi Djany Solo, baada ya Rotarota utamsikia kijana anaingia hapo anagonga mpaka mwisho tofauti na ulilozoea humu Solo limesikika barabara. Hii inaashiria moto uliopo kwenye albamu ya Mpiana ijayo.

Aidha Mpiana amesema kuwa ameichelewesha albamu yake ili kuzipisha albamu za wanamuziki wenzake ambazo nazo zimeingia sokoni kwa sasa, anasema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwani mwisho wa siku mashabiki wanaonunua CD na DVD zao ni hao hao na wanahitaji muda kusikiliza nyimbo za mwanamuziki mmoja mmoja alisema Mpiana.


Kimenuka Wenge BCBG; Djino atimuliwa kundini

February 3, 2013

image

Djino wa BCBG

Habari zilizothibitishwa na JB Mpiana mwenyewe zinasema kuwa uongozi wa BCBG umemtimua mwanamuziki Djino ambaye alikuwa na kundi hilo kwa miaka kadhaa, Djino ambaye amesikika vyema kwenye wimbo wa ZK au Zadio Kongolo, inasemekekana Djino aligombana na mwanamuziki mwenzake Tshai Ngenge na amekuwa na tabia zisizo njema ndani ya kundi zima.

Hata hivyo habari ambazo Spoti na Starehe imezipata zinasema kuwa Djino amesimamishwa jukwaani na hafanyi mazoezi kwa kile kilichoelezwa kuwa alionekana na mwanamuziki Koffi Olomide, Ikumbukwe kuwa mpiga chants na ngoma wa Wenge BCBG wakati huo Titina Acapolne aliingia matatizoni alipoonekana kuwa karibu sana na mwanamuziki Koffi Olomide kiasi cha kumuomba kumsimamia harusi yake, jambo hilo lilipelekea kutokuwa na mahusiano mazuri na hatimaye Alcapolne alijiondoa BCBG na kwa sasa yuko Dubai akifanya shughuli zake huko.

Hata walivyokuwa nchini kariibuni baadhi ya wanamuziki wa BCBG hawakuwa wazi sana kwa nini Djino hakuja nchini, vile vile nikukumbushe pia Mwanamuziki mwingine Sunda Bass naye aliwahi kusimamamishwa kwa takribani miezi nane kundini na aliporejea alikuja na kibao Liberez ambacho kinashika mpaka wa sasa.

Binafsi nilikuwa nampenda sana Djino ambaye alitunga wimbo wa CHERIE ENVELEE ambao uko kwenye albamu ya SOYONS SERIEUX. Wimbo huu mara ya kwanza Djino aliurekodi na bcbg ukiwa ni moja ya nyimbo zilizomo kwenye album lao jipya la Sayons Serieux,dada yake Djino anaekwenda kwa jina la Claudia Bakisa amekuja kuurekodi upya Kama remix,je upi umetoka bomba?

Hii sasa ndio original version iliyoimbwa na Djino mwenyewe,mwana kisangani,huyu ndio anaongea kiswahili kwenye ile video ya jb tolingana kisangani kama mlisikia akisema sema pole pole ndio mwendo na watu wakalipuka, watu wa kisangani wanaongea zaidi kiswahili.

Na huu ni wa Dada mtu Claudia Bakisa

Sikiliza hizi sauti kisha uniambie version ipi ni bomba kwako, The Romantic wa Mapenzi Club mercy mingi papaa kwa hii, Papaa Julie Elystone Le Charismatique Leader, Presidaa wa Congolee ya Darisalama, Uko juu Papaa Salute!!! , hebu sema kidogo hapa.


Lobeso, Atalaku wa WMMM anayeng’ara kwenye Albamu mpya.

February 3, 2013

Kundi la Wenge Musica Maison Merre linaloongozwa na Werasson Ngiama Makanda “Roi de la Foret” nguli mwenyewe liliangusha albamu yake mupya sokoni ikiwa ni siku moja baada ya kusherehekea siku ya Kuzaliwa kwa mwanamuziki huyo na siku ya ufunguzi wa zawadi yaani Boxing day.

Albamu hiyo tangu imeingia sokoni takribani mwezi mmoja sasa inasemwa imefanya vizuri na watu wameanza kuimba ghani za atalaku Lobeso huku ikiendelea kupendwa zaidi, Albamu hiyo ambayo inajulikana kama Satellite +2.

Lobeso amekuwa kinara kwenye albamu hii inasemwa kwa sababu ya kutokuwepo atalaku namba moja jambo lililopelekea Lobeso kushika hatamu wakati wa mazoezi ya nyimbo za albamu hii na sasa iko sokoni.

Naomba nikuwekee moja ya kibao cha Werasson kipya ujionee mwenyewe.


Meneja akanusha Ferre kushikiliwa na Polisi huko Paris

February 3, 2013

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Jet Set Vasco Mabiala amekanusha habari zilizozagaa kuwa Boss wake Ferre Gola amekamatwa huko Paris Ufaransa.

Akiongea na wanahabari jijini Kinshasa Vasco Mabiala amesema kuwa si kweli Ferre Gola amekamatwa na wala hajawekwa ndani kama ilivyoripotiwa awali na kuwa Ferre Gola yuko huko kukamilisha albamu yake ambayo imechelewa kidogo kutoka kutokana na sababu za Kiufundi.

Awali iliripotiwa Kuwa Mwanamuziki Ferre Gola alikuwa ameshikiliwa na Polisi wa Ufaransa kwa kile kilichooelezwa kuwa taratibu za kiuhamiaji. Meneja huyo amesema kuwa Ferre yuko bussy katika Studio za Zet akikamilisha albamu yake hiyo inayokuja kwa jina la Black Box. Aidha meneja huyo alisema kuwa Ferre akimaliza hapo anakwenda Hollywood kufanya shooting ya nyimbo zake sita zilizomo kwenye albamu hiyo, Mabiala amesema kuwa habari hizo zimevumishwa na kundi la vijana walioanzisha vita na wanamuziki wa Congo kwa sababu za Kisiasa bila kufafanua zaidi.


JEAN BEDEL MPIANA WA TSHIKUTA (JB MPIANA)

February 3, 2013

Na Lubonji wa Lubonji

Muite vyovyote BIN ADAM,SOUVERAIN PREMIER,PAPA CHERI,LE MARÉCHAL MUKULU,LA STAR DU RÉEL,HÉEO NATIONAL,SALVADORA DE LA PATRIA,L’HOMME QUI A MIS DE L’EAU DANS LE COCO,L’EAU QUI A SUCRÉ LA BANANE,MOTO PAMBA,MWANA CONGO,L’ENFANT DU PAYS,L’ÉTOILE DE DIEU,MOKONZI YA BA WENGÉ,LEADER CHARISMATIQUE,LEADER YA BA OEUVRES, MOKONZI YA FIKIN…

Leo nitawaletea Historia fupi ya Mwanamuziki JB Mpiana kama ilivyoandika na Shabiki Lubonji wa Lubonji, Kuna mengi sana yameshasemwa kuhusu JB Mpiana lakini hii ni moja ya historia zake ambazo zimewekwa kwenye kumbukumbu na mashabiki wake kwa ushirikiana na vyanzo mbalimbali.

Pichani ni JB Mpiana akiwa na mwanaye Kipenzi Daida Mpiana.

JB MPIANA kazaliwa tarehe 2/06/1967 mjini KANANGA mkoa wa KASAI (katikati mwa Inchi ya CONGO.

Mtoto wa Mzee Mpiana na Mama LUSAMBO Agnès,

Siku mbili baada ya kuzaliwa kwake, wazazi wake wakaamua kuhamia kwenye Mji Mkuu wa KINSHASA.

Mwaka 1981 kama tulivyo fahamishwa kwenye sehemu zilizo pita, JB MPIANA akiungana na wenzake WERRASON na kadhalika, waliunda Group WENGE MUSICA 4×4.

JB MPIANA katokea kuwa mwanamuziki nyota kwenye Group WENGE MUSICA,na hapo baadae kateuliwa kama Raisi wa Group. hadi sasa yeye na WERRASON ndo wanaonekana kama ma Iconic figure wa Group WENGE MUSICA.

Ni mmoja katiyao aliewezesha WENGE MUSICA kuingia katika Historia ya Muziki huko ZAÏRE (CONGO) kwa sababu :

1.Ni wa kwanza katika Generation yake kupewa tuzo binafsi la Dhahabu kutokana na wimbo wake wa MULOLO Mwaka 1988.

2.Kateuliwa mwimbaji bora Inchini ZAÏRE Mwaka 1991

3.Ni wakwanza kati ya wanamuziki wa kizazi kipya huko CONGO kufanya SHOO kwenye Kumbi za kifahari Mjini PARIS (OLYMPIA na ZÉNITH).

4.Ni kijana wa kwanza kwa wale wa umri wake ambae kapewa tuzo la GOLDEN RECORD (DISK)

JB MPIANA ni mmoja kati ya wanamuziki wa huko CONGO amabae kapewa tuzo nyingi huku bado akiwa na Umri mdogo :

-Mwaka 1988 akiwa bado na miaka 21 kapewa tuzo la mtunzi wa wimbo bora (MULOLO)

-Mwaka 1991 akiwa na miaka 24 kateuliwa mwimbaji bora

-Mwaka 1999 akiwa na miaka 32 kapewa tuzo la Golden Record (DISK) kutokana na Album yake ya LES FEUX DE L’AMOUR iliyotolewa mwaka 1997.

JB MPIANA kashika record ya kuwa kijana mwana muziki mwenye kua na Umri mdogo (CONGO) kufanya SHOO kabambe kwenye kumbi za ZÉNITH,OLYMPIA,PALAIS OMNISPORTS DE BERCY,Mjini PARIS.

JB MPIANA kafanya SHOO kabambe pia kwenye kumbi za ELYSÉE MONTMARTRE,BATACLAN,DOCK EIFFEL hapohapo PARIS,

Kwenye PALAIS DE CONGRÈS Mjini LIÈGE (BELGIUM)

Na kwenye ukumbi wa MEDLEY Mjini MONTRÉAL huko CANADA.

Baada ya mgawanyiko wa WENGE MUSICA 4×4,mwaka 1997, JB MPIANA kawa na kundi lake la WENGE MUSICA “LES ANGES ADORABLES”akiwa pamoja na ALAIN MAKABA,BLAISE BULA,ALAIN MPELA,TUTU KALUDJI,ROBERTO EKOKOTA,AIMELIA yaani baadhi ya wanamuziki wote wa WENGE MUSICA asilia.

Papo hapo JB MPIANA na kundi lake wakaenda Ulaya ku rekodi ALBUM ya TITANIC amabayo inadhihirisha mgawanyiko wa kundi la WENGE MUSICA 4×4.

Utamsikia JB MPIANA akisema “IL N’Y A RIEN C’EST L’HOMME QUI A PEUR” HAMNA LOLOTE NIWOGA TUU UNAO WASHIKA.

ALBUM TITANIC ina nyimbo 10 :

1. Titanic Tutu Callugi/Wenge BCBG

2. RDC JB Mpiana

3. Barakuda Alain Makaba

4. Omba JB Mpiana

5. Proces Mambika Alain Mpela

6. Likala Moto Blaise Bula

7. Tour Eiffel Titina Mbwinga Alcapone

8. Champion Kapangala JB Mpiana

9. Liberation Aimelia Lias

10. Serge Palmier Burkina Fasso

Mwaka 1999 kamayalivyo andikwa hapo juu,JB MPIANA kafanya SHOO kabambe Mjini PARIS kwenye Kumbi za ZÉNITH na OLYMPIA.

Baadae kasema hataki tena kudumbwiza kwenye ukumbi bali kwenye viwanja,ndipo mwaka huohuo kashuka Mjini COTONOU huko BENIN na kafanya Shoo kabambe.

Baada ya hapo kaja dumbwiza Mjini KINSHASA kwenye STADE DE MARTYRS watu zaidi ya 85000 waliudhuria…

Mwaka huo 1999 JB MPIANA katoa Album SINGLE yake akaipa jina

Y’A PAS MATCH Y’A PAS PHOTO ikiwa na nyimbo 2 :

1. Y’a pas match, Y’a pas photo JB Mpiana

2. Papito Mbala (Version 2) JB Mpiana

Mwaka 2000 JB MPIANA katoa ALBUM yake ya pili ya SOLO

Pichani JB Mpiana akiwa na Mke wa Debs Demukalinga jijini Dar Es Salaam Hivi Karibuni.

T H ( TOUJOURS HUMBLE) ikiwa na Volume 2 na nyimbo 16 :

Volume 1

No Titre Auteur(s) Durée

1. TH (Toujours Humble) JB Mpiana

2. Walay Danico JB Mpiana

3. Education JB Mpiana

4. Sultan de Bruneil Kaskinto JB Mpiana

5. Dis-moi Amour JB Mpiana

6. Rose verte JB Mpiana

7. Grâce à toi Germain JB Mpiana

8. Jeanpy Pipina JB Mpiana

9. 48 Heures Gecoco JB Mpiana

10. Bye Bye Julie JB Mpiana

Volume 2

No Titre Auteur(s) Durée

1. Mohamed Kaniansy JB Mpiana

2. Aminata Sylla JB Mpiana

3. Kinshasa JB Mpiana

4. Bye Bye Julie (version disco) JB Mpiana

5. Lauréat’s 2000 JB Mpiana

6. Acappella

Sifa nyingi zilimwendea JB MPIANA kutokana na ALBUM hii na ikamwezesha kupata kwa mara ya pili tuzo la GOLDEN RECORD (DISK) pia na tuzo nyingine nyingi :

-Mwimbaji bora,-Album bora,-Wimbo bora “48 Heures GECOCO”

-Mtunzi Bora “wimbo Grace à toi Germain”

-Mwanamuziki Bora.

Masterpiece hii ilifanya JB MPIANA aweke Mguu wake kwenye World Music, na pia kajifungua kwenye aina mbalimbali ya Muziki kama vile : RAP,SALSA,

Hebu pata uondo kwa kusikiliza nyimbo zifwatazo (WALAY DANICO,EDUCATION,SULTAN DE BRUNEI,DIS MOI AMOUR,LA ROSE VERTE,BYE BYE JULIE,AMINATA SYLLA.

Mwaka 2000 mwezi wa nane hadi kufikia mwaka 2001 mwezi wa Inne,

JB MPIANA na kundi lake wakaanza kufanya SHOO mbalimbali mjini KINSHASA,mwishowe wakafaanikiwa kusafiri na kwenda Nchi mbalimbali duniani ambako walifanya zaidi ya SHOO 30. walienda FRANCE,BELGIUM,HOLLAND,GERMANY,SWISS,IRELAND,UK, na CANADA.Wakamalizia dhiara yao Nchini CHAD amabapo walifanya SHOO kabambe 3.

Itaendelea Jumatano…


%d bloggers like this: