PAPY KAKOL wa WMMM achezea kichapo toka kwa Les Combattant

February 22, 2013

 

image

Pichani mwanamuziki Papy Kakol akiwa anavuja damu baada ya kupata kipigo kutoka kwa vijana wanaojiita “Wapiganaji” wa Congo wanaoupinga utawala wa Rais Kabila

Mwanamuziki Mpiga tumba machachari wa WMMM Papy Kakol amesurika kifo baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa vijana wanamageuzi wanajulikana kama Les Combattants ambao wameapa kuwakomesha wanamuziki wote waliompigia kampeni Rais Kabila uchaguzi uliopita.

Tangu ufanyike uchaguzi mkuu wa DRC na kumrejesha madarakani Rais Kanila, imekuwa sio Neema kabisa kwa wanamuziki wa Congo ambao walikuwa wakitegemea show za nje hasa Belgium na Ufaransa ambako walikuwa wakipata show nyingi.

Kilichowaponza wanamuziki wa Congo ni kitendo chao cha kumpigia kampeni Rais Kabila jambo ambalo limeaudhi sana vijana wa Congo walioko nje hasa wa Ufaransa na Belgium wanaopendelea mageuzi nchini Congo na kutofurahishwa na uongozi wa Rais Kabila wanaojiita  LES COMBATTANTS yaani wapiganaji.

image

Pichani Kakol akisindikizwa na Polisi wa Ufaransa chini ya Ulinzi mkali

 

Kakol alikuwa nchini Ufaransa alipokwenda kwa shughuli zake na kutaka kumuombea msamaha Boss wake Werasson jambo lililowaudhi mnoo hawa wapiganaji, wapo wanaohusisha na sababu binafsi huku wakisema kuwa Werasson hapendwi sana na Le Combattant wa Ufaransa ambao inasemekana wanamchukia, “Kupigwa kwa Kakol si kwa sababu ya WMMM kumsupport Kabila ila ni kwa sababu binafsi, Ni sababu za kushtua ambapo Gola Ferre aliruhusiwa kufanya Show katika Paris kwa sababu yeye ni kuonekana kama kupambana na Werrason. Bet yangu ni kwamba watu bana chuki na Werrason wanaweza kuruhusiwa kufanya lakini kama ni pro-Werrason, basi itakuwa combattants wanawakataa  Hiyo ni nini mimi naona…” alisema Franko Pepe wa Vibes De Africa  kwa kiswahili cha kubabaisha nilipochat naye jana.

Habari zinasema kuwa hata Felix Wazekwa ambaye ni Shemeji ya Kabila naye yumo matatani, na maa ya mwisho alikuwa nchini Ufaransa kumalizia Albamu yake na hakuna aliyejua isipokuwa familia yake na marafiki wa karibu. Wapo wanaowahusisha Les Combatant na JB Mpiana kuwa wao wanamkataa zaidi Wera na kumkubali JB angawa Wenge BCBG nao walishiriki lakini kwa BCBG Belgium ndio kuna walakini zaidi ukilinganisha na Ufaransa.

Kwa wanaojua Kifaransa haya ni Majibu ya Kakol kwa kilichotokea bado nimeomba mtu anisaidie kutohoa ili niwajuze hapa.

Advertisements

MSIKILIZE JDL LOKO TRABENDO NA KITU DJIKIDJIKI

February 22, 2013

Siku kama ya leo Rafiki zangu Musa na Husna wa 87.8 Pride Fm ni siku wanagonga Rhumba tuu zilizotukuka, nawakubali sana hawa jamaa na kutamani km ungewaaikiliza wiki nzima kiukweli wamekiweza kipindi chao cha African Vibes ambacho wanapiga muziki wa Kiafrika tuu, nikuache na wimbo toka kwake JDL Loko wa kundi la Wenge BCBG akikwambia Djiki Djiki.


%d bloggers like this: