Sara Fiona akimshirikisha Koffi Olomide

February 19, 2013

Ni mara chache kusikia Koffi ameshirikishwa kwenye wimbo wa mtu, tena hasa ikiwa mwanamuziki mwenyewe ni mchanga au asiyejulikana kama alivyo Sarah Fiona ambaye wengi wetu hatumjui, anaitwa Mopao Mokonzi Koffi Olomide Papaa na Didi Stone,Papaa na Sean James hapa yuko kivingine akiwa mwanadada mrembo Sarah Fiona wanakwambia J’ai tout Quit akimaanisha nimeacha Yoote.

Ndani ya wimbo huu Mopao analalamikia mapenzi jinsi alivyojitoa kwa mpenzi lakini mpenzi mwisho wa siku kambwaga, anasema “J’ai tout quittée pour lui et il m’a quitté”….tafsiri ya haraka haraka “Nimeacha kila kitu kwa ajili yake lakini mwisho wa siku kaniacha”, Ukiangalia Video hii utakubaliana na mimi kuwa Koffi anajipanga sana kwenye utengenezaji wa Video na inasemwa kuwa anaongoza kwa kutumia pesa nyingi kwenye uzalishaji wa Video zake.

Advertisements

Djino atangaza Albamu yake iko jikoni

February 19, 2013

Wiki mbili baada ya kutangaza kuachana na bendi ya Wenge BCBG mwanamuziki Djino hatimaye ametangaza kuwa Albamu yake ya Commandant de bord iko njiani kutoka.

Djino alithibitisha kuondoka BCBG baada ya kutokea sintofahamu kati yake na kiongozi wa bendi hiyo JB Mpiana. Djino ambaye amefanya kazi na BCBG zaidi ya muongo mmoja na kusikika kwenye albamu karibu zote za Wenge BCBG alitamba na Kibao cha Zadio Kongolo ZK ambcho kiko kwenye mahadhi ya taratibu na hivi majuzi kwenye albamu ya Soyons Serieux alitunga na kuimba kibao kingine humo kibao ambacho kilirudiwa na dada yake.

Wapo wanaosema kuwa kitendo chake cha kutaka kutoa Albamu yake ndio kilicho anza kumchefua boss wake huyo na ilipopatikana sababu aliamua kumsimamisha kabla ya yeye mwenyewe kutangaza kujitoa.

Albamu ya Djino yenye nyimbo nane inatazamiwa kutoka baada ya kumalizaka kazi ya uchanganyaji inayofanyika nchini ufaransa. Akiongea Djino amesema sasa ananafasi ya kufanya kazi vizuri Albamu yake ambayo awali alibanwa na muda kwa vile Wenge kama kampuni ilimhitaji pia, vile vile Djino alimuasa kiongozi wao JB Mpiana kuwa makini na kuwa na tabia ya kusikiliza wanamuziki wa chini kwani wale walio karibu naye wanachukua faida ya ukaribu wao na kuwaharibia wengine.

Djino alikorofishana na mwanamuziki Sunda Bass kabla ya kusimamishwa


%d bloggers like this: