Meneja akanusha Ferre kushikiliwa na Polisi huko Paris

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Jet Set Vasco Mabiala amekanusha habari zilizozagaa kuwa Boss wake Ferre Gola amekamatwa huko Paris Ufaransa.

Akiongea na wanahabari jijini Kinshasa Vasco Mabiala amesema kuwa si kweli Ferre Gola amekamatwa na wala hajawekwa ndani kama ilivyoripotiwa awali na kuwa Ferre Gola yuko huko kukamilisha albamu yake ambayo imechelewa kidogo kutoka kutokana na sababu za Kiufundi.

Awali iliripotiwa Kuwa Mwanamuziki Ferre Gola alikuwa ameshikiliwa na Polisi wa Ufaransa kwa kile kilichooelezwa kuwa taratibu za kiuhamiaji. Meneja huyo amesema kuwa Ferre yuko bussy katika Studio za Zet akikamilisha albamu yake hiyo inayokuja kwa jina la Black Box. Aidha meneja huyo alisema kuwa Ferre akimaliza hapo anakwenda Hollywood kufanya shooting ya nyimbo zake sita zilizomo kwenye albamu hiyo, Mabiala amesema kuwa habari hizo zimevumishwa na kundi la vijana walioanzisha vita na wanamuziki wa Congo kwa sababu za Kisiasa bila kufafanua zaidi.

Advertisements

One Response to Meneja akanusha Ferre kushikiliwa na Polisi huko Paris

  1. Prince George says:

    Heshima kwako bro PIUS na wadau wa blog hii pendwa,naomba nifanyie utatafiti kwa huyu FERRE GOLA kuhusu mwimbaji wake anaitwa VIBRATION kama amefukuzwa au amesimamishwa?7bu kuna Concert live imefanyika mwishoni mwa mwaka uliokwisha (2012) PLANETTE SONO BEACH huko Congo hakuwepo kwenye show hiyo,napata wasi wasi 7bu FERRE GOLA alionekana akiwafanyia usaili waimbaji wapya,wale wa zamani walikuwepo ambao nawafahamu kwa majina ya kisanii “waimbaji” kiongozi wa bendi LIKINGA,NICODEMES,SESELE,GUY DIGITAL NA SHIKITO,NA SOLO GUITAR MAKAUSHI pasipo kuwepo Atalaku wawili (2) na mpiga tumba mmoja(1)Solo Guitar no (2)ambao majina yao siyafahamu,kama nilivyosema mimi ni shabiki mkubwa wa huu muziki wa Congo na nimfuatiliaji mzuri lkn kuna mengi siyajui ndio maana kupitia Spoti na starehe naamini nitafahamu tu!ni hayo tu kwa leo,Mercii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: